Kama kuna jambo linahitaji Mipango, Uthubutu, Hekima na Busara kweli kweli basi ni siasa

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
19,919
21,918
Ukiwa na mipango lakini ya hovyo hovyo isiyoeleweka wala kutekelezeka utapuuzwa tu na Wananchi. Utajipigia kelele kelele mwenyewe wee bila kuungwa mkono na yeyote.

Ukikosa hekima na busara katika kuwaza, kusema na kutenda, huku ukiendekeza kiburi, chuki na visasa dhidi ya wengine, majivuno, ubishi, dhihaka na tamaa ya madaraka, utadharauliwa na kwakweli utakataliwa tu na wananchi kwenye sanduku la kura bila mbambamba yoyote.

Uthubutu na kujizatiti kwa maneno na matendo katika kutekeleza mipango, sera na dira mahususi ya chama au taasisi ni miongni mwa vivutio muhimu sana kwa wananchi kumuamini kiongozi mwanasiasa mwenye haiba na hulka hiyo.

Kujipa umuhimu usiostahili na kutegemea huruma ya Wananchi kwa kwa kukiuka sheria kwa makusudi na kuchokoza vyombo vya ulinzi na usalama ili vilazimike kushughulika nawe wewe ni siasa zisizo na matokeo chanya kwa nyakati za sasa.

Ni muhimu sana, kushawishi Wananchi kwa mipango mizuri mbadala, sera nzuri na muhimu kwa maendeleo yao, dira na uelekeo wa wazi wa kueleweka n.k

Yote hayo yakifanyika kwa hekima na busara, uwezekano wa kueleweka kwa Wananchi na pengine kuungwa mkono na wananchi ni mkubwa sana.

Majivuno, kiburi na ujuaji wanaenda kuumbuka Serikali za mitaa mwishoni mwa mwaka huu 🐒

Mungu Ibariki Demokrasia ya ya Tanzania.
 
ukiwa na mipango lakini ya hovyo hovyo isiyoeleweka wala kutekelezeka utapuuzwa tu na wananchi...
utajipigia kelele kelele mwenyewe wee bila kuungwa mkono na yeyote...

ukikosa hekima na busara katika kuwaza, kusema na kutenda, huku ukiendekeza kiburi, chuki na visasa dhidi ya wengine, majivuno, ubishi, dhihaka na tamaa ya madaraka, utadharauliwa na kwakweli utakataliwa tu na wananchi kwenye sanduku la kura bila mbambamba yoyote...

uthubutu na kujizatiti kwa maneno na matendo katika kutekeleza mipango, sera na dira mahususi ya chama au taasisi ni miongni mwa vivutio muhimu sana kwa wananchi kumuamini kiongozi mwanasiasa mwenye haiba na hulka hiyo..

kujipa umuhimu usiostahili na kutegemea huruma ya wananchi kwa kwa kukiuka sheria kwa makusudi na kuchokoza vyombo vya ulinzi na usalama ili vilazimike kushughulika nawe wewe ni siasa zisizo na matokeo chanya kwa nyakati za sasa..

ni muhimu sana,
kushawishi wananchi kwa mipango mizuri mbadala, sera nzuri na muhimu kwa maendeleo yao, dira na uelekeo wa wazi wa kueleweka n.k

yote hayo yakifanyika kwa hekima na busara, uwezekano wa kueleweka kwa wananchi na pengine kuungwa mkono na wananchi ni mkubwa sana..

majivuno, kiburi na ujuaji wanaenda kuumbuka serikali za mitaa mwishoni mwa mwaka huu 🐒

Mungu Ibariki Demokrasia ya ya Tanzania
Oppressors playing Victims!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom