Kama hujawahi kufika jiji la Tanga, basi haya ndio mambo yanayopatikana huko

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
1,448
3,644
Ijue Tanga Mjini Na Maajabu Yake.

Katika maisha yako jitahidi sana walau siku moja ufike Tanga, utakuja kunishukuru… Haya jionee maajab ya jiji la Tanga

1. Ikifika Saa 3 usiku Hakuna Daladala Utaona Barabarani.

2. Jiji Lina Watu 390K Lakini Ifikapo Saa 4 Huoni Watu Nje Usiulize Kwanini Jiongeze.

3. Ugali Wa 1500 Unapata Mboga 7 Usisahau Uono (Dagaa Mchele) Buree.

4. Tanga Ndio Jiji Pekee Kuna Baiskeli Za Kukodi Yaani Kama Bodaboda Vile Zina Kiti Chenye Sponge Hadi Raha.

5. Club Za Tanga Zinapiga Taarabu Unashangaa Shauri Yako.

6. Self Tanga Ni 50K Chumba Kikubwa Na Choo Ndani Tena Vimenakshiwa Vizuri Kabisa.

7. Wakazi Wa Tanga Hawapandi Boxer,TVS Wanapikipiki Zao Special Zinaitwa "Huoniao" AKA Kibao Mbuzi.

8. Breakfast Ya 1000 Tanga Unashiba Vizuri Kabisa Kifupi Ukila Mchana Kisa Njaa Ujue Una Minyoo Au Ulafi.

9. Ndio Jiji Lisilo Na Kelele Wala Vurugu Pako Kimyaaa Hadi Raha.
Kijana Wa Tanga Akishakuwa Na Uhakika Wa Kula Na Sehemu Ya Kukaa Anawaza Kuongeza Mke Sio Biashara Wala Kuwekeza Hayo Mtajua Wenyewe.

10. Ukitaka Binti Wa Kitanga Aje Geto Mwambie Apande Pikipiki Utamlipa Boda Halafu Akifika Mnunulie Chips Yai Na Soda Broo Umemaliza Kazi.

11. Tanga Ndio Jiji Lenye Soda Au Tuseme Juice Ya Kipekee Inayoitwa "Healtho" Au "Anjari" Ni Tamu Sana Zipo Aina Kama 5 Hivi Huko Bakhresa,Mo,Coca,Pepsi Hata Hawasikiki Sana.

12. Ukiwa Tanga Jaribu Kuishi Na Watu Vizuri Kuoa Na Kuolewa Usipate Shida Wao Ndio Watakutafutia.

13. Raskazone,Donge,Tanga Beach Ndio Ushuani Huko Wanaishi Vigogo AKA Mafogo.

14. Tanga Mjini Kuna Super Market 1 Tu Inaitwa Mkwabi 🤣🤣 (Labda Kama Zimeongezeka)

15. Wasambaa Ndio Kabila Linaloheshimika Zaidi Tanga Mjini Na Ndio Kabila Superior.

16. Kuhusu maji ya kunywa hapo usiseme kule huna haja ya kununua maji dukani maana maji ya bomba tu yanatosha kukata kiu yako kifupi hayana shida kabisa hadi raha.

17. Ukiwa na binti wa kitanga uwe na pumzi ipasavyo usipoangalia utatolewa jasho mwanaume alaa.

18. Tanga Kuna Traffic Light sehemu 2 Tu Pale Toyota Kuelekea Bombo na Maeneo ya Mkwakwani.

19. Tanga hakuna Bolt, Uber Wala Farasi ni Mwendo Wakuita Kibao Mbuzi au Upande Daladala.

2o. Daladala Ipo Radhi Imsubiri Mtu Tena Ikibidi Ipige Reverse Imfwate Alipo.

Sema katika yote Tanga ni jiji lililopangika vizuri kuanzia uswahilini, mjini kati mpaka huko kwa matajiri!!

#VisitTanga
 
JE WAJUA HAYA KUHUSU TANGA?

1. Reli ya Kwanza Tanzania Bara - Tanga 1893.

2. Shule ya kwanza ya Sekondari- Tanga 1890 (Tanga Old School).

3. Shule ya Kwanza (Anglikana) Tanzania 1848 - Tanga Magila Muheza.

4. Taasisi ya Kwanza ya Utafiti wa Malaria Duniani - Tanga Muheza, Ubwari 1949.

5. Hospitali ya Kwanza (1st Modern Hospital) - Tanga, Cliff Block 1895

6. Hoteli ya Kwanza ya Kisasa Tanzania - Tanga, Kaiserhof Hotel 1906.

7. Upandaji wa Mkonge wa Kwanza Afrika - Tanga, Pangani 1900.

8. Nembo ya Benki Kuu ya Tanzania ni msukumo kutoka kwa Kiwanda cha Mkonge Tanga kwani kilichangia zaidi ya asilimia 60 ya Pato la Taifa.

9. Tanga lilikuwa jiji la kwanza kuwa Manispaa mwaka 1891.

10. Tanga ilikuwa na Soko la kwanza la kisasa nchini Tanzania - 1903 Soko la Uzunguni.

11. Risasi ya kwanza ya Vita Kuu ya Kwanza ya Afrika ilipigwa Tanga - Novemba 1914.

12. Tanga ilikuwa na kanisa la kwanza Tanzania - Magila Msalabani Muheza - 1840s.

13. Tanga ilitoa padre mzaliwa wa kwanza (Mlutheri) nchini Tanzania, Jacob Lumwe (1880 - 1970).

14. Zaidi ya 95% ya Kata za Jiji la Tanga zina maji ya kutosha, hivyo kuwa jiji pekee nchini.

15. Tanga ina mfumo wa maji taka kongwe na unaofanya kazi Afrika Mashariki.

16. Tanga inashikilia rekodi ya jiji lenye mpangilio mzuri zaidi Afrika Mashariki.

17. Tanga inashikilia rekodi ya kuwa na maktaba ya kwanza ya umma nchini Tanzania miaka ya 1950.

18. Tanga ina mtambo wa kwanza wa kufua umeme nchini Tanzania tangu mwaka 1905 huko Muheza Amani.

19. Bandari ya Tanga ndiyo bandari inayohudumu kwa muda mrefu zaidi Afrika Mashariki (Rejelea Mtandao wa Bandari ya Tanga).

20. Tanga ina mnara wa saa kongwe zaidi nchini Tanzania (pengine Afrika) 1901
LA MWISHO KABISA:

Tanga ina KARIBU haina KWAHERI.🤣💕👍✌🏽💋
 
Back
Top Bottom