Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 291
- 772
KAMA HIVI NDIVYO UNAVYOISHI MJINI NI BORA URUDI TU KIJIJINI UKAISHI KULINGANA NA KIPATO CHAKO.
Yawezekana hii isiwe makala nzuri kwa waishiyo mijini huku wakijisifu kila siku na kuwabeza waishiyo vijijini ila ukimakinika na kuchukulia chanya basi kuna jambo utajifunza. Kuishi mjini ni ndoto ya wengi nafikiri inaweza kuwa zaidi ya asilimia hamsini ya watu wanatamani kuishi mjini na hasa kwenye miji ile mikubwa lakini uhalisia ukoje huko mjini kwa wengi wao? Kuwa kwenye changamoto mjini sio sababu pekee ya kusema uhame urudi kijijini/mkoani la hasha. Hapa namaanisha kwa wale ambo mjini hawapawezi kabisa ila wanapang'ang'ania tu kwa sababu zisizo na msingi.
Bila shaka utakuwa umewahi sikia ama kuona baadhi ya watu waishio mijini wakiwabeza watu waishio vijijini ama mikoani kama wasemavyo watu wa Dar es salaam na kibaya zaidi hudiliki kusema watu wa vijijini ni washamba na wasio wabunifu wa maisha, Sio uongo kuwa kuishi mjini kunakomaza akili kulinganisha na kuishi kijijini kutokana na harakati kuwa nyingi mjini na panahitaji wepesi sana katika maamuzi ili uweze kumudu mjini lakini kwenye maamuzi hayo hayo kuna watu wapo mijini kuongeza idadi tu ya watu ila ki uhalisia wanaishi maisha magumu sana kwa lugha isiyo rasmi ni kuwa walikurupuka kuja mjini ilihali hawana mipango ya kuwafanya wanufaike na maisha ya mjini.
Ikiwa unaishi mjini kwa sababu moja wapo kama nimevyoelezea hapa chini basi haraka toka mjini urudi mkoani/kijijini ama jitafakari zaidi ubadili mtindo wako wa maisha.
Kuishi mjini ki ulimbukeni; Unaishi mjini kutaka tu uonekane nawe unaishi mjini yaani ukisimama na kujitambulisha ama kutambuliswa unaishi mjini hiyo ndiyo furaha yako kuu bila kujali hali ngumu unayokutana nayo huko mjini na kama hii ndio sababu pekee ya wewe kuishi mjini basi haraka ondoka mjini kwa sababu unaongeza tu idadi ya watu na usipokuwa makini maisha yatakuchapa na kujikuta kwenye hali mbaya kimaisha mpaka kwa uzao wako pia, kwa sababu utatumia gharama kubwa kuwafanya watu wajue kuwa unaishi mjini ilihali hiyo gharama ungeitumia kuboresha maisha yako huko mjini, kila siku utakuwa mtu wa kuchapisha maudhui mitandaoni ya kukuonyesha upo mjini ambapo vocha zitateketea tu bure na hakuna unachokiingiza tofauti na sifa ambazo hazikuingizii pesa.
Kuishi mjini kwa sababu umepazoea; Kuna mtu maisha ya mjini kwake ni magumu sana na kikawaida tayari yamemshinda ila ukimpa fursa za kurudi mikoani/kijijini anaweza hata kukutukana na ukitaka kujua sababu anakwambia kapozea mjini hivyo itampa sana tabu kuanza tena upya huko mikoani kama wewe ndio huyu jua kabisa mjini hapakufai ondoka haraka la sivyo jiandaye kuzeeka maskini.
Kuendelea kuishi mjini kwa maisha magumu ukiogopa kuchekwa endapo utarudi mkoani/kijijini; Huyu pia hafai kuishi mjini kwa sababu hatofautiani sana na mtu limbukeni na asiye na malengo,Huyu yupo tayari kufanya maamuzi ila anaogopa macho ya watu ilihali mjini pememshinda kuishi sasa nawe jiandaye kuishi maisha magumu sana kwa sababu huna mbinu za kutatua changamoto ili umudu maisha ya mjini bali upo tu kuonekana mtoto wa mjini ilihali maisha yamekushinda.
Kuishi mjini huku unategemea mshahara tu kama chanzo pekee cha pesa na huna chachu yoyote ya kuongeza vyanzo vingine vya pesa; hili kundi lina watu wengi sana na hapa ndipo utakuta mtu anaishi mjini kimateso sana na hana mpango wowote wa kujinasua na mateso hayo, kwa mfano unategemea mshahara tu ndio ulipe kodi ya nyumba,ukupe nauli zako za kila siku kukupeleka kazini, ukupe ada ya watoto tena shule za mjini hawana huruma kama huna ada mtoto watamfukuza tu sasa hapo kweli utaishi maisha ya furaha? Sio kwamba kila siku utakuwa mtu wa kulalamika tu kwanini mishahara haipandi.
Kama wewe ndio huyu ondoka haraka mjini urudi mkoani kwenye nyumba nzima unapanga elfu hamsini na bado zipo jirani na unapofanyia kazi hivyo huna haja ya kulipa nauli, haya kwako yatakuwa maamuzi sahihi kwa sababu huko mjini pia umekaa tu hutaki biashara hivyo ni bora urudi kuishi kwa kutegemea msh