Kama fununu za Sven kurudi ni kweli basi ni aibu sana kwa CEO Barbara

njaakalihatari

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
4,081
8,671
Dah, hizi fununu za kishingo zinanikera sana, huyu na Zoran walikimbia majukumu wakijua makundi ni shughuli nzito. Kishingo kafika makundi kakimbia, Zoran angekuwepo hata makundi Simba isingefika.

Hata kama uamuzi wa kuleta kocha ni wa wote kwenye bodi, ila CEO ndiye atabeba lawama au pongezi kwa maamuzi ya aina hiyo. Na kwa rekodi za Barbara hata mazungumzo yake ni mtu ambaye anawafurahia sana makocha wenye ngozi nyeupe, yaaani ni bora arudi hata Gomez au Pablo walioweza kufika robo fainali.

Halafu kwa pesa ambayo Sven kaishika Moroko na Saud Arabia, Simba inaweza fika lile dau lake? Jamani kama ni kweli hizo fununu achaneni nazo, kwa kifupi mpeni Mgunda timu, mlipeni pesa kama alivyokuwa analipwa Zoran au Punguzeni milioni 3 mumuongezee Matola.

Zoran hapo Premiere De Agosto alienda kama mtaalamu wa viungo, kapenya penya kwa majungu na kuwa kocha mkuu, kwa kutumia timu aliyokuta imetengenezwa na watangulizi wake akafika nusu fainali Klabu Bingwa 2018, mambo yalipoanza kuwa magumu akakimbia.

Sven alifukuzwa Chipolopolo Zambia akaja Simba ambayo ilikuwa ni timu yake ya kwanza kufundisha, mbali na timu za taifa. Kafika makundi kakimbilia Rabatt, huko nako akawakimbia kaenda Saud Arabia kafukuzwa kabisa.

Mgunda/Matola/Mwarami embu muwaamini basi hata kama mkataba wa miezi sita hadi ligi iiishe. Halafu ghafla nimeukumbuka huu uzi. Acheni shobo na Wazungu, kutwa kuwasema vibaya kwa waandishi huko nje ya nchi halafu mnashoboka shoboka tu au ni 10%?

43638658
kohler.JPG
 
Hizo ni tetesi tu, kwasasa Mgunda ameshaambiwa aseme anachotaka apewe, kama ni mchezaji mpya ataongezewa dirisha dogo.
 
Taarifa rasmi za club zinasema Simba imesimamisha mchakato wa Kocha, Mgunda ndio kocha...Wewe unataka tujadili stori za vichochoroni
Imetoka wapi hiyo taarifa rasmi? kigugumizi cha kutoa picha akisaini kiko wapi,? na wewe unaona kabisa wana imani naye 100% au wanasubiria mechi ya jumapili? angekuwa mzungu huyu angekuwa keshapewa hata range rover ya kutembelea mda huu kwa kushinda mechizote 4 za CAFCCL
 
bongo hakun tetesi 98% n kwel
ukisoma body language ya Barbara wakati wa kutangaza michakato ya utafutaji makocha akizungumzia makocha wa ulaya wlaiotuma CV huwa anakuwa excited kabisa yaani hadi ile pretty face yake ina glow ni wazi huwa anaona raha ngozi nyeupe ikisamama kwenye benchi pale

Mgunda anawapa wakati mgumu sana kwa sasa ,WAMPE TEAM HARAKA SANA OFFICIALLY NA MAFAO MAZITO ..NYUMBA MASAKI, GARI KALI NA MARUPURUPU MENGINE NA MSHAHARA MNONO KAMA WALE MATAAHIRA YA KIZUNGU
 
amin mkuu
 
Acha kujiweka kwenye driving wheel ya Simba. Huna lolote la msaada kwa timu zaidi ya porojo na majungu hapa. Acha viongozi wapange na kuamua iwapendezavyo kwani ndio tuliowakabidhi timu.

Akija Kishingo ni sawa tu. Hawa caretaker coaches wanakuwa na mafanikio ya muda mfupi sana kabla ya kuanza kuharibikiwa (unajifanya kumsahau Ole Gunar wa Manchester United?

Umewasifia Gomez na Pablo ukasahau kuwa hao wamebebwa na msingi alioucha Kishingo. Kumbuka kuwa Kishingo ndiye kocha aliyekuja kumaliza tatizo la Simba kufungwa goli tano tano ugenini.

Wewe huyohuyo pamoja na Gentamycine mliwashambulia sana viongozi walipompa kazi hiyo Mgunda. Kifupi hamfai kuwa washauri wa Simba kwa lolote kwani mnaendeshwa na upepo unapoelekea. Tumechoshwa na kelele zako za hapa jukwaani. Simba itafanikiwa bila msaada wako.
Imetoka wapi hiyo taarifa rasmi? kigugumizi cha kutoa picha akisaini kiko wapi,? na wewe unaona kabisa wana imani naye 100% au wanasubiria mechi ya jumapili? angekuwa mzungu huyu angekuwa keshapewa hata range rover ya kutembelea mda huu kwa kushinda mechizote 4 za CAFCCL
 
Acha kujiweka kwenye driving wheel ya Simba. Huna lolote la msaada kwa timu zaidi ya porojo na majungu hapa. Acha viongozi wapange na kuamua iwapendezavyo kwani ndio tuliowakabidhi timu.

Akija Kishingo ni sawa tu. Hawa caretaker coaches wanakuwa na mafanikio ya muda mfupi sana kabla ya kuanza kuharibikiwa (unajifanya kumsahau Ole Gunar wa Manchester United?

Umewasifia Gomez na Pablo ukasahau kuwa hao wamebebwa na msingi alioucha Kishingo. Kumbuka kuwa Kishingo ndiye kocha aliyekuja kumaliza tatizo la Simba kufungwa goli tano tano ugenini.

Wewe huyohuyo pamoja na Gentamycine mliwashambulia sana viongozi walipompa kazi hiyo Mgunda. Kifupi hamfai kuwa washauri wa Simba kwa lolote kwani mnaendeshwa na upepo unapoelekea. Tumechoshwa na kelele zako za hapa jukwaani. Simba itafanikiwa bila msaada wako.
Wewe ukimsifia kishingo na kusema hawa caretakers ni miyeyusho unaona NI SAWA KABISA NI OPINION...mimi nikisema kinyume NI MAJUNGU NA KUJIFANYA NAJUA
Waliokabidhiwa nchi wanakosolewa sembuse waliokabidhiwa team,wasisemwe wao nani? malaika? embu acha uchawa we jamaa
Huyo kishingo unayemsifia si alikimbia ghafla akadanganya ni issue za kifamilia za binti yake ghafla akaonekana moroko?
Umesoma kilichopo kwenye hizo attachments, hao wazungu kutwa kuwasema hao viongozi vibaya kwa waandoshi huko nje na kutukana viwanja vyetu na mazingira ya huku, hadi kocha wa makipa Damon naye mmbeambea tu
PUNGUZENI SHOBO
 
Kishingo alikimbia majungu ya watu kama wewe. Mtu ana implement tactical football, mnaanza kumkaangia sumu mara oooh tupishe, tunataka Simba yenye mpira wa Samba. Aliona kabisa hamjui mlitakalo, akaamua awapishe kwanza. Kwa taarifa yako Kishingo ataifaa sana Simba kwa sasa.
 
Kishingo alikimbia majungu ya watu kama wewe. Mtu ana implemented tactical football, mnaanza kumkaangia sumu mara oooh tupishe, tunataka Simba yenye mpira wa Samba. Aliona kabisa hamjui mlitakalo, akaamua awapishe kwanza. Kwa taarifa yako Kishingo ataifaa sana Simba kwa sasa.
yameisha hayo majungu? huoni unatukana watu wa ndani ya simba unaoddai walimpiga majungu? au wewe ukitoa maoni yako ndiyo sahihi wengine ni kinyume chake
 
wewe acha kabisa mkuu kocha ni Mgunda hata tukitolewa caf bado atabaki Mgunda.
Gadiola mnene bado yupoyupo.
 
Imetoka wapi hiyo taarifa rasmi? kigugumizi cha kutoa picha akisaini kiko wapi,? na wewe unaona kabisa wana imani naye 100% au wanasubiria mechi ya jumapili? angekuwa mzungu huyu angekuwa keshapewa hata range rover ya kutembelea mda huu kwa kushinda mechizote 4 za CAFCCL
Uwe na focus, unazungumzia Sven au unazungumzia Mgunda kupewa Range?
Kuhusu taarifa mbona imetolewa na Ahmed mara kibao tu, au unataka mpaka akuletee wewe
 
Back
Top Bottom