Kama chanzo cha uhai kinaweza kubadilika basi uhai wenyewe hauna msingi thabiti hadi sasa. Je, ni upi msingi wa uhai?

Thecoder

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
1,386
3,732
Bila shaka mko salama waungwana...

Kikawaida neno msingi na chanzo ni maneno mawili ambayo ukiangalia kwa jicho la kawaida ni kama yanafanana hivi lakini ni maneno yaliyo na utofauti mkubwa.

Kwa maana chanzo huwa kinatengeneza muendelezo usio na ukomo lakini msingi huwa unatengeneza muendelezo mgumu ambao huwa haueleweki pasipo kurudi tena kwenye msingi kwa maana nyingine ni kwamba msingi ndio unaounda vyanzo mbalimbali.

Ndio maana mkusanyiko wa vyanzo vingi vya habari fulani unaweza kuleta mkanganyiko wa mambo hasa inapotokea vyanzo vyote vinaongelea habari moja ila vinatofautiana katika taarifa zao, hii hufanya mtu ashindwe kuelewa aamini chanzo kipi kati ya hivyo, na ili kuondoa huu mkanganyiko basi mtu hupaswa arudi kwenye msingi wa habari yenyewe na baada ya kufanya hivyo basi ni rahisi kujua kati ya vyanzo hivyo ni kipi na kipi kimeandika habari kwa kuzingatia msingi wake.

Kwahiyo kuna nyakati neno chanzo hutumika zaidi kwenye mambo ambayo msingi wake haujulikani au uhakika wa moja kwa moja juu ya msingi wake haupo lakini msingi ndio ambao unabeba chanzo.

Lakini pia chanzo wakati fulani huwa kinakua na mbadala wake wakati msingi huwa hauna mbadala (ndio maana habari unaweza kuipata jamiiforum, milard ayo na media zingine ila msingi wa habari hiyo hauwezi kubadilika).

Kwamfano wewe ni chanzo cha watoto wako kuzaliwa na wao ni chanzo cha wajukuu zako kuzaliwa lakini pia wajukuu zako ni chanzo cha vitukuu kuzaliwa na hii itaendelea namna hii bila ukomo na wewe hujawa msingi kwasababu nyuma yako alikuwepo baba yako ambae alikua chanzo cha wewe kuzaliwa ila pia Kabla ya baba yako alikuwepo babu yako ambae yeye alikua chanzo cha baba yako kuzaliwa na hii itarudi nyuma katika umbali usio julikana na ndio maana tumetumia neno chanzo.

Lakini pia mtu ni roho, na kama hii ndio basi hizo roho ambazo wewe umezileta hapa duniani haimaanishi kwamba wewe ndio mtu pekee ambae unao uwezo wa kuleta roho hizo isipokua wewe uliwin tu kwenye ile probability ila usingezileta wewe basi angekuwepo mtu mwingine ambae angeweza kuzileta, na vivyo hivyo wewe kwa baba yako na baba yako kwa babu yako na kadhalika.

Kwahiyo neno chanzo linapotumika katika eneo lolote ujue tayari kuna hali isiyo na ukomo imetengenezwa kwa kwenda mbele au kwa kurudi nyuma kwa maana ule msingi kamili wa jambo hilo haujulikani au kuna namna mbadala ya jambo hilo kwenye kutokea kwake au kufanyika kwake ukiachana na namna hiyo ambayo imetumika.

Okay, wacha twende mbali kidogo, watu husema Mungu ni chanzo cha uhai, hii tayari ni sentensi ambayo haina ukomo, kwa kurudi nyuma au kwenda mbele, lakini pia kwa kusema hivi unamaanisha asingekua yeye basi chanzo cha uhai kingeweza kupatikana kwa namna nyingine.

Angalia hii, wewe ni chanzo cha mkeo kuolewa au tuseme ni chanzo cha ndoa yenu ila sio msingi wa hiyo ndoa kwa maana hata kama wewe usingemuoa basi angeweza kuolewa na mtu mwingine, na huyo mtu mwingine nae angekua tu chanzo ila wala sio msingi kwa maana huyo mtu mwingine asingemuoa basi angeolewa na mtu mwingine tena, kwahiyo hii unaona inakua ni infinity loop.

Kwahiyo kama Mungu ni chanzo cha uhai basi msingi wa uhai bado haujulikani na ukomo wa uhai huo huo haujulikani pia (naomba usome ukiwa katika utulivu wa akili ili unielewe vizuri hapa).

Hii inamaanisha nini? Hii inamaanisha kwamba ni eidha Mungu ni neno moja linalotumika kuwakilisha jamii ya viumbe fulani kama vile neno binadamu linavyotumika kutuwakilisha Mimi na wewe au ukiachana na Mungu basi kuna viumbe vingine venye uwezo wa kutoa uhai (wacha tusonge taratibu huku tukiongeza tafakuri juu ya tafakuri hapa).

Kama Mungu ni kiwakilishi cha jamii ya viumbe fulani kama lilivyo neno binadamu basi neno la tumfanye mtu kwa mfano wetu halitakua na maana yoyote iliyojificha zaidi ya lilivyo na limekuwepo pale kama uthibitisho wa kwamba Mungu ni neno la jumla linalowakilisha jamii fulani kama ilivyo kwa neno binadamu.

Na kwa uthibitisho zaidi wa jambo hili ni pale Mungu anaposema aabudiwe yeye na wala sio miungu mingine, hii inamaana anajua ya kwamba katika jamii ya kimungu hayupo peke yake.

Ni sawa na wewe utengeneze robot lako ikiwa wewe ndio mkuu wa mradi licha ya kwamba ndani yake kutakua na ma-engineer wengine ambao ni binadamu na ghafla ukaanza kuona yule robot anaanza kuwatii watu wengine kuliko wewe mkuu wa kitengo lazima urudi umwambie unaefaa kunyenyekewa ni wewe na wala sio binadamu wengine.

Kama hiyo haitoshi lakini pia kuna maeneo kadhaa Mungu alijitokeza kwa kujitambulisha ya kwamba yeye ni Mungu wa vita mara Mungu wa maarifa na kadhalika, hii sio bahati mbaya na wala huna haja ya kuilazimisha ikae kwa namna tofauti na hiyo kwa maana hivyo ndivyo ilivyo na hii inaweza kuthibitisha kwamba Mungu ni sawa na kusema binadamu (yote ni maneno yanayowakilisha jamii ya viumbe fulani).

Na kwa hoja hiyo sasa, ndio maana ukisema Mungu ni chanzo cha uhai inamaana si Mungu wote ambao walishiriki kwenye mradi wa kumpa uhai binadamu ila ni jopo tu la Mungu kadhaa ndio ambao walifanya hii project na ndio maana neno chanzo limetumika kwa maana ya kwamba kama hao waliokaa wasingekaa basi Mungu wengine wangeweza kukaa na kumpa uhai binadamu kama wangeamua kufanya hivyo.

Lakini kama tukiendelea kubaki na msimamo wetu wa kwamba Mungu ni mmoja na wala sio jamii ya viumbe fulani basi hapa tunaweza kuibua hoja mpya ya kwamba kumbe ukiachana na Mungu katika puzzle hii pia kunao uwezekano wa kuwepo jamii fulani ya viumbe wenye uwezo wa kutengeneza watu au kumpa mtu uhai, na kama kweli chanzo cha uhai kinaweza kubadilika kinamna hii basi uhai wenyewe hauna msingi thabiti.

Na hii ndio sababu ya neno chanzo kutumika badala ya neno msingi.

Najua kuna mtu hapa anaweza asielewe ila kama unataka uelewe zaidi unaweza Kutafakari kwa kina juu ya neno chanzo na msingi kisha ukishapata point urudi usome tena hili andiko.

Kwa mfano huwa tunasema chanzo cha mapato wala sio msingi wa mapato kwa maana kuna njia nyingi ambazo mtu anaweza akazitumia ili zimuingizie mapato.

Chanzo cha furaha yangu ni wewe, kwa maana usipokua wewe basi anaweza akawa mtu mwingine ambae anaweza akanipa hii furaha unayo nipa kwakua duniani binadamu haupo peke yako.

Chanzo cha Mimi kupata kazi ni wewe, hii inamaanisha hata usingekua wewe ningepata kazi kwa maana nisingekutana na wewe basi ningekutana na mtu mwingine ambae angekuwa chanzo kama ambavyo wewe umekua(kwa maana wewe si mtu wa kwanza na wa mwisho kuwa na connection au roho ya upendo wa namna hii).

Tengeneza msingi wa maisha yako, kwasababu wewe pekee ndio mwenye uwezo wa kutengeneza maisha yako na wala hakuna mbadala wa wewe.

Kwahiyo ukisoma kwa umakini na Kutafakari hapa, utagundua ya kwamba ndani ya chanzo kuna msingi, na msingi mmoja unaweza ukatengeneza vyanzo mbalimbali (usichanganyikiwe sasa na wewe, ili uelewe hapo rudi mwanzo mwa andiko nilikwambia msingi ndio hutengeza complex things na ili uweze kuondoa ucomplex ni lazima uanze kuyagawa mambo hayo kwenye namna fulani rahisi ili uufikie msingi wake).

Ndio maana mtu akifariki huwa wale watu wanaomfahamu wanapopata taarifa huwa wanauliza chanzo cha kifo chake ni nini, kwa maana wanajua kifo kinaweza kusababishwa na mambo mengi ya msingi ambayo ndio huweza kuunda chanzo.

Kwahiyo kama haujui msingi wa jambo fulani huwezi kusolve puzzle yake, na hapa duniani mambo mengi yapo kwenye puzzle na puzzle ni muunganiko wa mambo mbalimbali ya msingi na ili uweze kusolve puzzle nyingi za kilimwengu lazima uuelewe vizuri msingi wake ni nini.

So, kama Mungu ndio chanzo cha uhai basi hii tayari inakua ni complex puzzle kwa maana iko na vyanzo vingi hadi kufikia ule msingi wake na ili tuweze kuisolve lazima tuujue msingi wake ni upi.

Je, msingi wa uhai ni nini?

NITARUDI.
 
Lakini pia chanzo wakati fulani huwa kinakua na mbadala wake
mimi ni chanzo cha watoto wangu kuzaliwa hivyo biological watoto wangu wanabeba DNA zangu hivyo kama mimi sitahusika kuwa tengeneza hakuna mtu mwingine ataye watengeneza
Mungu ni chanzo cha uhai
Mungu ni msingi wa ulimwengu wote kupitia kwake ndo tunapata vyanzo vya maisha kama light, maji, oxygen, atoms na particles zake
Kama hiyo haitoshi lakini pia kuna maeneo kadhaa Mungu alijitokeza kwa kujitambulisha ya kwamba yeye ni Mungu wa vita mara Mungu wa maarifa na kadhalika, hii sio bahati mbaya na wala huna haja ya kuilazimisha ikae kwa namna tofauti na hiyo kwa maana hivyo ndivyo ilivyo na hii inaweza kuthibitisha kwamba Mungu ni sawa na kusema binadamu (yote ni maneno yanayowakilisha jamii ya viumbe fulani
Hii haimanishi mungu wapo wengi hapa anasema sifa zake kutokana na jamii tofauti anazoziambia, kwa mfano mimi nikiwa baba mwenye nyumba ina maana namiliki kila kitu wakija watu wanakagua choo nitajiita baba mwenye choo wakija watu wanaotafuta vyumba mimi ni baba mwenye vyumba wakija watu wa kiwanja mimi pia ni baba mwenye kiwanja kwa kuwa vyote vipo kwenye miliki yangu
Ni sawa na wewe utengeneze robot lako ikiwa wewe ndio mkuu wa mradi licha ya kwamba ndani yake kutakua na ma-engineer wengine ambao ni binadamu na ghafla ukaanza kuona yule robot anaanza kuwatii watu wengine kuliko wewe mkuu wa kitengo lazima urudi umwambie unaefaa kunyenyekewa ni wewe na wala sio binadamu wengine.
aliye na blueprint na anayejua wapi materials zilipo ndio mwenye robot, sawa mtu au kitu chochote kinaweza tengeneza human being ila unajua recipe zote zilizotumika unajua kutengeneza atoms kama sio basi anayejua na akafanikiwa ndio the boss
 
Bila shaka mko salama waungwana...

Kikawaida neno msingi na chanzo ni maneno mawili ambayo ukiangalia kwa jicho la kawaida ni kama yanafanana hivi lakini ni maneno yaliyo na utofauti mkubwa.

Kwa maana chanzo huwa kinatengeneza muendelezo usio na ukomo lakini msingi huwa unatengeneza muendelezo mgumu ambao huwa haueleweki pasipo kurudi tena kwenye msingi kwa maana nyingine ni kwamba msingi ndio unaounda vyanzo mbalimbali.

Ndio maana mkusanyiko wa vyanzo vingi vya habari fulani unaweza kuleta mkanganyiko wa mambo hasa inapotokea vyanzo vyote vinaongelea habari moja ila vinatofautiana katika taarifa zao, hii hufanya mtu ashindwe kuelewa aamini chanzo kipi kati ya hivyo, na ili kuondoa huu mkanganyiko basi mtu hupaswa arudi kwenye msingi wa habari yenyewe na baada ya kufanya hivyo basi ni rahisi kujua kati ya vyanzo hivyo ni kipi na kipi kimeandika habari kwa kuzingatia msingi wake.

Kwahiyo kuna nyakati neno chanzo hutumika zaidi kwenye mambo ambayo msingi wake haujulikani au uhakika wa moja kwa moja juu ya msingi wake haupo lakini msingi ndio ambao unabeba chanzo.

Lakini pia chanzo wakati fulani huwa kinakua na mbadala wake wakati msingi huwa hauna mbadala (ndio maana habari unaweza kuipata jamiiforum, milard ayo na media zingine ila msingi wa habari hiyo hauwezi kubadilika).

Kwamfano wewe ni chanzo cha watoto wako kuzaliwa na wao ni chanzo cha wajukuu zako kuzaliwa lakini pia wajukuu zako ni chanzo cha vitukuu kuzaliwa na hii itaendelea namna hii bila ukomo na wewe hujawa msingi kwasababu nyuma yako alikuwepo baba yako ambae alikua chanzo cha wewe kuzaliwa ila pia Kabla ya baba yako alikuwepo babu yako ambae yeye alikua chanzo cha baba yako kuzaliwa na hii itarudi nyuma katika umbali usio julikana na ndio maana tumetumia neno chanzo.

Lakini pia mtu ni roho, na kama hii ndio basi hizo roho ambazo wewe umezileta hapa duniani haimaanishi kwamba wewe ndio mtu pekee ambae unao uwezo wa kuleta roho hizo isipokua wewe uliwin tu kwenye ile probability ila usingezileta wewe basi angekuwepo mtu mwingine ambae angeweza kuzileta, na vivyo hivyo wewe kwa baba yako na baba yako kwa babu yako na kadhalika.

Kwahiyo neno chanzo linapotumika katika eneo lolote ujue tayari kuna hali isiyo na ukomo imetengenezwa kwa kwenda mbele au kwa kurudi nyuma kwa maana ule msingi kamili wa jambo hilo haujulikani au kuna namna mbadala ya jambo hilo kwenye kutokea kwake au kufanyika kwake ukiachana na namna hiyo ambayo imetumika.

Okay, wacha twende mbali kidogo, watu husema Mungu ni chanzo cha uhai, hii tayari ni sentensi ambayo haina ukomo, kwa kurudi nyuma au kwenda mbele, lakini pia kwa kusema hivi unamaanisha asingekua yeye basi chanzo cha uhai kingeweza kupatikana kwa namna nyingine.

Angalia hii, wewe ni chanzo cha mkeo kuolewa au tuseme ni chanzo cha ndoa yenu ila sio msingi wa hiyo ndoa kwa maana hata kama wewe usingemuoa basi angeweza kuolewa na mtu mwingine, na huyo mtu mwingine nae angekua tu chanzo ila wala sio msingi kwa maana huyo mtu mwingine asingemuoa basi angeolewa na mtu mwingine tena, kwahiyo hii unaona inakua ni infinity loop.

Kwahiyo kama Mungu ni chanzo cha uhai basi msingi wa uhai bado haujulikani na ukomo wa uhai huo huo haujulikani pia (naomba usome ukiwa katika utulivu wa akili ili unielewe vizuri hapa).

Hii inamaanisha nini? Hii inamaanisha kwamba ni eidha Mungu ni neno moja linalotumika kuwakilisha jamii ya viumbe fulani kama vile neno binadamu linavyotumika kutuwakilisha Mimi na wewe au ukiachana na Mungu basi kuna viumbe vingine venye uwezo wa kutoa uhai (wacha tusonge taratibu huku tukiongeza tafakuri juu ya tafakuri hapa).

Kama Mungu ni kiwakilishi cha jamii ya viumbe fulani kama lilivyo neno binadamu basi neno la tumfanye mtu kwa mfano wetu halitakua na maana yoyote iliyojificha zaidi ya lilivyo na limekuwepo pale kama uthibitisho wa kwamba Mungu ni neno la jumla linalowakilisha jamii fulani kama ilivyo kwa neno binadamu.

Na kwa uthibitisho zaidi wa jambo hili ni pale Mungu anaposema aabudiwe yeye na wala sio miungu mingine, hii inamaana anajua ya kwamba katika jamii ya kimungu hayupo peke yake.

Ni sawa na wewe utengeneze robot lako ikiwa wewe ndio mkuu wa mradi licha ya kwamba ndani yake kutakua na ma-engineer wengine ambao ni binadamu na ghafla ukaanza kuona yule robot anaanza kuwatii watu wengine kuliko wewe mkuu wa kitengo lazima urudi umwambie unaefaa kunyenyekewa ni wewe na wala sio binadamu wengine.

Kama hiyo haitoshi lakini pia kuna maeneo kadhaa Mungu alijitokeza kwa kujitambulisha ya kwamba yeye ni Mungu wa vita mara Mungu wa maarifa na kadhalika, hii sio bahati mbaya na wala huna haja ya kuilazimisha ikae kwa namna tofauti na hiyo kwa maana hivyo ndivyo ilivyo na hii inaweza kuthibitisha kwamba Mungu ni sawa na kusema binadamu (yote ni maneno yanayowakilisha jamii ya viumbe fulani).

Na kwa hoja hiyo sasa, ndio maana ukisema Mungu ni chanzo cha uhai inamaana si Mungu wote ambao walishiriki kwenye mradi wa kumpa uhai binadamu ila ni jopo tu la Mungu kadhaa ndio ambao walifanya hii project na ndio maana neno chanzo limetumika kwa maana ya kwamba kama hao waliokaa wasingekaa basi Mungu wengine wangeweza kukaa na kumpa uhai binadamu kama wangeamua kufanya hivyo.

Lakini kama tukiendelea kubaki na msimamo wetu wa kwamba Mungu ni mmoja na wala sio jamii ya viumbe fulani basi hapa tunaweza kuibua hoja mpya ya kwamba kumbe ukiachana na Mungu katika puzzle hii pia kunao uwezekano wa kuwepo jamii fulani ya viumbe wenye uwezo wa kutengeneza watu au kumpa mtu uhai, na kama kweli chanzo cha uhai kinaweza kubadilika kinamna hii basi uhai wenyewe hauna msingi thabiti.

Na hii ndio sababu ya neno chanzo kutumika badala ya neno msingi.

Najua kuna mtu hapa anaweza asielewe ila kama unataka uelewe zaidi unaweza Kutafakari kwa kina juu ya neno chanzo na msingi kisha ukishapata point urudi usome tena hili andiko.

Kwa mfano huwa tunasema chanzo cha mapato wala sio msingi wa mapato kwa maana kuna njia nyingi ambazo mtu anaweza akazitumia ili zimuingizie mapato.

Chanzo cha furaha yangu ni wewe, kwa maana usipokua wewe basi anaweza akawa mtu mwingine ambae anaweza akanipa hii furaha unayo nipa kwakua duniani binadamu haupo peke yako.

Chanzo cha Mimi kupata kazi ni wewe, hii inamaanisha hata usingekua wewe ningepata kazi kwa maana nisingekutana na wewe basi ningekutana na mtu mwingine ambae angekuwa chanzo kama ambavyo wewe umekua(kwa maana wewe si mtu wa kwanza na wa mwisho kuwa na connection au roho ya upendo wa namna hii).

Tengeneza msingi wa maisha yako, kwasababu wewe pekee ndio mwenye uwezo wa kutengeneza maisha yako na wala hakuna mbadala wa wewe.

Kwahiyo ukisoma kwa umakini na Kutafakari hapa, utagundua ya kwamba ndani ya chanzo kuna msingi, na msingi mmoja unaweza ukatengeneza vyanzo mbalimbali (usichanganyikiwe sasa na wewe, ili uelewe hapo rudi mwanzo mwa andiko nilikwambia msingi ndio hutengeza complex things na ili uweze kuondoa ucomplex ni lazima uanze kuyagawa mambo hayo kwenye namna fulani rahisi ili uufikie msingi wake).

Ndio maana mtu akifariki huwa wale watu wanaomfahamu wanapopata taarifa huwa wanauliza chanzo cha kifo chake ni nini, kwa maana wanajua kifo kinaweza kusababishwa na mambo mengi ya msingi ambayo ndio huweza kuunda chanzo.

Kwahiyo kama haujui msingi wa jambo fulani huwezi kusolve puzzle yake, na hapa duniani mambo mengi yapo kwenye puzzle na puzzle ni muunganiko wa mambo mbalimbali ya msingi na ili uweze kusolve puzzle nyingi za kilimwengu lazima uuelewe vizuri msingi wake ni nini.

So, kama Mungu ndio chanzo cha uhai basi hii tayari inakua ni complex puzzle kwa maana iko na vyanzo vingi hadi kufikia ule msingi wake na ili tuweze kuisolve lazima tuujue msingi wake ni upi.

Je, msingi wa uhai ni nini?

NITARUDI.
Mungu ni chanzo cha uhai na hakukuwa wala hakuna kitu kingine kinacheza kuwa chanzo cha uhai
 
Mungu ni msingi wa ulimwengu wote kupitia kwake ndo tunapata vyanzo vya maisha kama light, maji, oxygen, atoms na particles zake
Nishawishi angalau hata kwa andiko.
mimi ni chanzo cha watoto wangu kuzaliwa hivyo biological watoto wangu wanabeba DNA zangu hivyo kama mimi sitahusika kuwa tengeneza hakuna mtu mwingine ataye watengeneza
Watoto wako wanabeba DNA yako ila DNA yako iko kwa baba yako na ya baba yako iko kwa babu yako na ya babu yako iko kwa baba yake so hii tayari ni infinity loop, ila ukichukulia kwenye upande wa mtu ni roho pia wanao ni roho so kama wewe usingezileta basi kuna mtu mwingine angezileta isipokua uliwin kwenye ile probability.
aliye na blueprint na anayejua wapi materials zilipo ndio mwenye robot, sawa mtu au kitu chochote kinaweza tengeneza human being ila unajua recipe zote zilizotumika unajua kutengeneza atoms kama sio basi anayejua na akafanikiwa ndio the boss
Kwahiyo hii point yako inakubaliana na Mimi ya kwamba Mungu ni neno la jumla kama ambavyo neno binadamu lilivyo sio.
 
Back
Top Bottom