Kama akiteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,802
3,244
MAWAZO YA HUYU DADA kama akiteuliwa kuwa MKUU WA WILAYA

Mkuu wa wilaya ni kiongozi mkuu wa serikali katika wilaya na jukumu lake la kiutawala ni kuhakikisha mifumo ya utawala katika eneo lake inafanya kazi vizuri na kwa ufanisi.Kiongozi huyu huteuliwa na Rais na ndiye mwakilishi wa Rais katika wilaya.

Baadhi ya majukumu yake ni; kusimamia shughuli za maendeleo katika wilaya, Huyu ndiye mkuu wa ulinzi na usalama katika eneo lake

Kwa sababu Mh Rais ndiye anayeteuwa wakuu wa wilaya nami nimeona nimuombe aniteuwe ili nitoe mchango wangu kwa watanzania, na kwa bahati nzuri kuomba siyo dhambi na ndiyo maana hata Biblia imeruhusu watu kuomba "Mathayo 7:8 kila aombaye hupewa..."

Mh Rais kama ukiniteuwa kuwa mkuu wa wilaya nitafanya yafuatayo:

1. Nitasimamia uboreshaji wa viwanja vya michezo na burudani katika wilaya nzima

Nitakacho kifanya ni kukaa na wadau wa michezo na watendaji wote wa kata zote hapa wilayani na kuweka mkakati wa kuboresha haya maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa ajili ya michezo . Tutajenga wigo na baadhi ya miundo mbinu katika viwanja lengo ni kuhamasisha Matamasha, Mashindano na ligi za mpira na michuano mbalimbali ifanyike na watu watoe kiingilio na wakitoa kiingilio serikali itapata kodi waandaaji nao watapata pesa pia wanamichezo watapata kipato.

Kuweka wigo katika viwanja kutasaidia sana mapromota kuaandaa matamasha na tamasha likiandaliwa biashara nyingi zinafanyika katika eneo husika na hivyo kipato kitaongezeka lakini pia viwanja vikiwa safi watoto wetu watapata mahali pa kufanyia mazoezi na hatimaye vipaji vingi vitaonekana

2. Nitahamasisha ujenzi wa viwanda vidogo 100 kila mwaka katika eneo langu

- Nafahamu Mimi kama mkuu wa wilaya nina nafasi ya ushawishi ndani na nje ya wilaya yangu. Nitapambana kuwatafutia mikopo ya viwanda vijana wangu walioko katika vikundi ili waweze kujiajiri wenyewe na hivyo kuondoa utegemezi na hata na wao kuanza kuchangia serikali kwa kulipa kodi.

Mfano wa viwanda hivyo ni viwanda vya kukoboa na kusaga nafaka, viwanda vya kukamua mafuta, viwanda vya juice, viwanda vya kutengeneza vifaa vya ujenzi, mashine za kuchomelea, viwanda vya kutengeneza viatu, kushona nguo, kusafisha na kukata mbao, kuoka mikate na maandazi.

Katika kufanya hivyo nitakuwa nimetengeneza ajira na kuongeza mapato ya serikali.

3. Kila kata nitahakikisha inakuwa na chuo cha ufundi

- Kwa kushirikiana na wadau na wapenda maendeleo tutaanzisha mkakati wa kujenga vyuo vya ufundi ili kuwawezesha vijana wetu ambao hawakupata nafasi ya kuendelea na masomo katika ngazi zingine wanakuja kujifunza ufundi katika vyuo vyetu tofauti hapa wilayani na hatimaye kujiajiri wao wenyewe.

Mfano wa vyuo na mafunzo yatakayofundishwa ni, ufundi wa magari, ufundi wa umeme, ufundi wa nyumba, ufundi wa kushona, upambaji, chuo cha kilimo,ufugaji wa kuku, ufugaji wa nyuki, kompyuta, simu, bajaji na pikipiki, ufundi wa samani n.k katika kufanya hivyo tutakuwa tumetengeneza ajira kwa vijana wetu.

4. Nitahakikisha wilaya yangu inakuwa namba moja kwa uzalishaji wa bidhaa au mazao Fulani

kuwa mzalishaji namba moja wa bidhaa fulani kuna faida nyingi sana kama vile kupata wageni wengi kuja kununua au kujifunza jinsi ya wao kuzalisha. Katika kuja kwao biashara nyingi zitachangamka na watu wetu watapata ajira.

Mfano tunaweza kuwa wazalishaji namba moja wa mafuta ya kupikia, Asali, kuku wa kienyeji au bidhaa yoyote ambayo tutaona inafaa.

Kuna mikoa ambayo ni maarufu kwa bidhaa Fulani kama vile Tabora wao ni Asali na Tumbaku nk, Singida mafuta ya alizeti na kuku wa kienyeji ni maarufu sana.

5. Wilaya yetu itakuwa ndiyo center ya kuotesha na kuuza Miche ya matunda

- Tutaweka hamasa na mkakati mkubwa katika kuotesha, kukuza, kupanda na kuuza Miche ya matunda na lengo letu sisi ndiyo tuwe wauzaji namba moja wa Miche ya matunda katika mkoa mzima.

kitakachofanyika ni kuhamasisha kila shule,chuo na vikundi mbalimbali waoteshe Miche ya matunda na kwa kuanza tutaanza na Miche milion moja(1,000,000) halafu kutakuwa na idala ya masoko itakayoundwa na wao wenyewe waoteshaji lengo ni kutafuta masoko na kila mche unaweza kuuzwa kwa 1000 au 2000 hivyo ukipiga hesabu utapata jibu.Katika kufanya hivi itasaidia vijana wetu kujiajiri na pia kuitangaza wilaya yetu.

Kwa leo ngoja niishie hapa nisikuchoshe, maana hoja ziko nyingi ila na wewe kama unawazo siyo vibaya ukiniongezea ili tukazijenge wilaya zetu ndani ya miaka 2 tu iwe tayari imeonekana. Asanteni sana.

Ikulu Mawasiliano
Ikulu Tanzania
 
Kwenye maisha yako Ogopa sana ukisikia kitu kinachoitwa Mfumo

Kwenye huo mfumo unaweza kuingia positive ukageuka ukiwa negative k.m B...she, K...ngwala

Unaweza kuingia kwenye mfumo ukiwa mweupe ukatoka mweusi k.m K...sheki, M....sya

Unaweza kuingia ukiwa Msafi ukatoka ukiwa umechafuka k.m S.....aye.

Mbaya zaidi unaweza kuingia ukiwa mzima ukatoka ukiwa marehemu k.m M........i

Kitu pekee kule ni kuingia ukiwa maskini hohehahe ukatoka bilionea k.m G.....lo, N.......pe, B.......she, na kwenye kundi hili ndio wengi

Acheni wazee walambe Asali kama sio kuhamishia Mzinga kabisa chumbani
 
Ningeshauri unge edit uzi wako ukapunguza ahadi ulizonadi kwetu kama vile sisi ndo tunaweza kukuchagua vile,walioko madarakani wanajua kabisa ya kuwa ji ngumu kutekeleza hilo pindi upatapo nafasi na hii inaonesha ya kuwa una hamu na madaraka ili umalize matatizo yako
 
Ningeshauri unge edit uzi wako ukapunguza ahadi ulizonadi kwetu kama vile sisi ndo tunaweza kukuchagua vile,walioko madarakani wanajua kabisa ya kuwa ji ngumu kutekeleza hilo pindi upatapo nafasi na hii inaonesha ya kuwa una hamu na madaraka ili umalize matatizo yako
Bahati mbaya sio mimi
 
Ni wakati muafaka wa kufikiria kuelekea mfumo wa serikali za majimbo. Kila jimbo like na serikali yake ikiongozwa na gavana anaechaguliwa na wakazi wajimbo hilo.
 
Back
Top Bottom