Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,588
- 1,190
Kituo Cha Afya Usinge kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, Mkoani Tabora, kimefanikiwa kufanya upasuaji wa dharura kwa wajawazito, ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kilipoanza kutoa huduma za afya mwaka 2023.
Kituo hicho kinachohudumia zaidi ya wakazi elfu 69 wa Kata ya Usinge na vijiji jirani kimefanikisha hatua hiyo kufuatia uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ya awamu ya sita kwa kununua vifaa tiba na vitendanishi vilivyogharimu zaidi ya shilingi milioni 214.
Kufuatia hatua hiyo mganga mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt.Honoratha Rutatinisibwa amenukuliwa akisema kuwa "Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji huu mkubwa alioufanya katika Sekta ya Afya na kusogeza Huduma za afya karibu na wananchi katika eneo letu".
Sasa wenyeji katika kata ya Usinge na vijiji jirani watafaidika na huduma za dharura za Upasuaji kwa wajawazito ambolo lilikuwa hitaji lao kwa muda mrefu na hivyo kupunguza au kuzuia kabisa matukio ya vifo vya wajawazito na vichanga wakati wa kujifungua.