Kalamu yangu, Elimu yangu

Makau Js

Member
May 25, 2017
93
233



Elimu ni moja ya silaha bora kabisa ambayo mwanadamu anatakiwa kuitumia katika kuibadilisha jamii iliyokata tamaa na kuifanya kuwa jamii yenye tumaini jema.

Elimu bora ni ile inayotumika kumfuta machozi maskini kwa njia ya kumpa faraja na kumpa tiba ya matatizo yake yote kutumia misingi yote mitatu,Elimu,Dini na utu.

Chuo kikuu ndio sehemu sahihi ya mwanafunzi kuvuna maarifa,ustaarabu,uungwana ,utu na kujiaanda kuwa mwanachuo aliye komaa kiakili,tabia ,haiba ufahamu ,maarifa na kuwa na msingi mzuri kwa jamii,familia na taifa ili kutengeneza Tanzania bora yenye vijana wenye mtazamo chanya katika kukuza uchumi,siasa safi na maendeleo yenye tija.

Wanavyuo wengi sana wa kizazi hiki ,tumeishi kwenye makosa siku zote kwenye taaluma zetu na mbele ya taifa letu ,mbele ya jamii yetu na mbele ya macho ya wazazi wetu,kiasi ambacho imelazimu watu wengi kunena kwa vinywa vyao kuwa Elimu ya sasa haina mashiko sababu ya utovu wetu wa nidhamu ,haiba mbaya na uchanga wa maarifa,na mwenendo mbovu wa tabia zetu mbele ya jamii na taifa kwa ujumla.

Wanavyuo wengi tumefanya vyuoni kuwa sehemu ya kwenda kumalizia balehe zetu, wakati chuo kikuu ni sehemu sahihi ya kijana kwenda kupevuka kiakili,mtizamo na kuongeza upeo wa ubunifu na nguvu ya ushawishi katika maswala yenye tija kwa taiafa na jamii kwa ujumla.Tanzania inazeeka kwa kuwa na idadi ndogo ya vijana wenye njaa ya mafanikio .

Tanzania inakaukiwa wanavyuo wenye nguvu ya hoja,Tanzania inapoteza siku hizi vijana wenye mvuto wa mawazo na ubora wa akili ,Tanzania inapoteza vijana wenye kauli thabiti za kizalendo zenye kunena matamu na mazuri ya Tanzania ,nchi tamu yenye utajiri mkubwa na harufu ya Amani na upendo.

Nini kifanyike.

1.Tunatakiwa kutengeneza Brand mpya ya wanafunzi wa vyuoni kuanzia muonekano ,haiba,mavazi ,fikra uwajibikaji,nidhamu kwa jamii na watu wote wanaotuzunguka ilia kurejesha heshima ya kuitwa msomi na kufanya vyuo vyote kuwa sehemu ya watu wanaoheshimika.

2.Kutengeneza utaratibu mzuri wa kuwa na nidhamu katika nyanya ya mauhusiano yenye tija ili kutengeneza ndoa za wasomi wenye mfano wa kuigwa na sio kuendeleza kuwa na kizazi cha Abortion,kuepuka ndoa changa na kutengeneza kizazi cha single parents.

3.Kuikimbia starehe na anasa,na kutengeneza utaratibu mzuri wa kujiaanda na maisha bora na matamu na kutengeneza utamaduni wa kufanya savings tukiwa tungali vyuoni ,na kujifunza kuwekeza pesa katika vitu vyenye tija.

4.Kutengeneza utamadani wa kusoma vitabu ili kuongeza maarifa,ubunifu na kupanua ubongo wa maarifa katika Nyanja tofauti hii inatakiwa kutengeneza makundi kama UDSM books club,IFM books club vikundi vya kusoma vitabu na kuazima vitabu.

5.Kujifunza kutumia social media kama nyenzo ya kuvuna maarifa na kusambaza maarifa na kubadilisha mawazo,kuepukana na utumwa wa kuwa na addictions za social media kutuma picture ngono na kujadili mambo yasiyo na tija.

Muombe Mwenyezi –Mungu akukutanishe na vitabu vilivyobeba maarifa unayoyahitaji ili upate maarifa unayotakiwa kuwa nayo.A true education is rooted in a good family ,upbringing and parental love and guidance.
 
Umeongea mambo muhimu sana ambayo yanagusa nyanja mbalimbali katika jamii yaani kijamii, kitaasisi na hata maisha katika familia.
Asante mkuu Makau Js
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…