Kaka yangu Polepole,haya uliyoyasema yana baraka za chama chako? Maana...

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,280
25,859
Yakuwashughulikia-kwa kuwaadhibu kichama Paul Makonda na Nape Nnauye yana baraka ya CCM yako? Kaka yangu Humphrey Polepole,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,umekaririwa ukiahidi kuchukuliwa hatua kwa makada hao wa CCM. Itawezekana?

Maana,kwasasa CCM ni kama haipo. Hata mchakato wa uchaguzi mkuu wa ndani ya chama unafanywa kimyakimya. CCM haifanyi mikutano ya hadhara;haijiimarishi kwa kutafuta wanachama wapya na kadhalika. Ipo kama haipo. Hayo ya akina Nape yatawezekana?

Au ndiyo ulikuwa ukitimiza wajibu wako wa kiitikadi na uenezi?
 
Kwani ilichukua muda gani kutoka CCM kuahidi kuwashughulikia kina Lowassa na Kundi lake.

CCM Ina organs za kisomi...CCM ni taasisi...CCM hutunza kumbukumbu zake za vikao.

Uchunguzi ukifanyika na mwenye kosa akabainika basi ataadhibiwa tu...ATAKATWA TU bila kujali haiba na wadhifa wake chamani...msijidai kama hamuijui CCM.
 
Inaonekana kila mtu anamuiga Magufuli. Habari za kungoja baraka zitachelewesha habari za "Hapa Kazi Tu".
 
Hiyo unayoongelea wewe ni CCM iliyopita, siyo hii inayoendelea ,ndiyo maana watu wanamashaka na kauli za huyo Mzee kijana H.Polepole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…