Kaka nilikutana na huyu mwanamke akiwa amepigika nikamzoa Hadi Akawa mtu katika watu

Magical power

JF-Expert Member
Sep 27, 2022
1,990
5,249
Kaka nilikutana na huyu mwanamke akiwa amepigika nikamzoa Hadi Akawa mtu katika watu,
1735382527475.jpg
alikuwa anatembeza soksi na nguo za nd0ani mtaa Kwa mtaa amepauka miguu ndara zimekatika.

Nilimpa Msaada nikamnunulia sendo hapo ndipo ikawa mwanzo wa kufahamiana niliona mwanga ndani yake na nilitarajia kujenga nae maisha .

Tulifahamiana Baada ya siku kadhaa alipo nieleza hali ya kwao nilipanga nae safari mpk huko nilikuta hali ni mbaya kwel kweli nilijitutumua niliezeka nyumba ya baba yake kijijini kwa hiari kabisa

Upendo wake kwangu uliongezeka aliniambia, sehemu ya maisha yake iliyobaki hapa duniani atamalizia na mimi

Kwa nia njema na upendo nilionao kwake, nilihakikisha kuwa nimsaidia .Hapo ndipo nilipogundua alikuwa chuo mwaka wa kwanza baba yake alifariki akakosa wakumuendeleza akasitisha masomo nikasimamia Hilo jukumu Kwa Nia ya dhati kabisa

Akasoma Bada ya kumaliza amepata ajira visingizio vikaanza mara kazin haruhusiwi kutumia simu muda wote mara haruhusiwi kuonekana na mwanamume nyumbani kwake ikiwa hana cheti Cha ndoa .usku hapokei simu nikasema isiwe tabu nikaenda kwao kuonana mama yake ili nipate baraka za kuoana ,mama yake akashangaa sana ananiambia mwanae anasema tulishaachana muda sana ananiambia Binti yake ameposwa muda na mwanaume mwingine.

Nawaza sana nashindwa nifanyeje.
 
acha nyege .muchukulie kawaida ujue unalipa wewe ulipokuwa dem ulimwengu mwingine ulikula ada za watu ni muda wa wewe kulipia furahia ushalipa deni hudaiw tena kunywa ulanzi nitalipia
 
Back
Top Bottom