Kaimu Katibu Mkuu UVCCM, Shaka; Atabiri Maalim Seif na Lowassa kurudi CCM

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka leo akiwa katika kata Mudida ameendelea na kazi za kisiasa akishiriki mikutano ya ndani ya kampeni ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida Kaskazini unaotarajiwa kufanyika Januari 13 Mwaka huu

Mapema asubuhi amepokewa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Singida Vijijini William Nyalandu , Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Singida Vijijiji Amos Kimasi na Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Singida Vijijini Neema Isambaa na Katibu wa UVCCM wilaya ya Singida vijijini Zainab Abdallah.

Amepokewa katika ofisi za CCM Kata ya Mudida na baadae akazungumza na wanachama wa CCM na jumuiya zake Mkoani hapa.

Katika msafara wake amefuatana na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida Denise Nyihara, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Singida Mjini Lucia Mwilu na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Singida Hemed Ferej.

Wengine ni Katibu wa CCM Singida Mjini Sylvester Yared , Naibu Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Singida Yagi Maulidi Kiharatu.

Akishiriki kwenye mkutano huo wa ndani Shaka amesema CCM itaendelea kufungua milango ya kuwakaribisha wanachama na viongizi toka upinzani wenye nia ya dhati katika kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli.

Amesema Wapinzani hawarudi CCM kwa kushinikizwa na Mtu yeyote bali utendaji wa Serikali ya awamu ya tano ndiyo unaowavutia na kuwajengea matumaini mapya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Aidha Kaimu Katibu Mkuu UVCCM, Shaka amewatolea wito Wanasiasa wawili wa upinzani Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, warejee CCM kwakuwa mahali waliko hakufanani na heshima zao.

Amesema Maalim Seiif kabla hajaenda upinzani amewahi kuwa Waziri wa Elimu, Waziri Kiongozi wa SMZ na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM huku Lowassa akibahatika kuwa Waziri Mkuu, Mbunge, Waziri na Mjumbe wa Kamati Kuu hivyo hadhi zao hazifanani na maeneo waliko .

"Wasione aibu au noma kurudi katika chama walichokitumikia toka wakiwa vijana wadogo na kuwafikisha mbali kisiasa kwani waliokuwa wakiyatamani yatokee sasa yanatekelezwa kwa ufanisi na serikali zote mbili "Alisema Shaka.

Shaka alisema ikiwa Maalim Seif na Lowassa kwa nyakati tofauti wamejenga uthubutu wa kusifu utendaji wa Rais Dk Magufuli kwa hatua anazizichukua ikiwemo kupambana na rushwa , ufisadi na ubadhirifu, hawana haja ya kubaki upinzani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Singida Mjini Lucua Mwilu amesema wapinzani wamekuwa na tabia kama chura kwani hutokea nyakati za masika ila vipindi vya kipupwe na kiangazi hapotea.

Shaka amesema uhodari wa upinzani ni kuziponda Serikali bila ya kuwa na hoja za maana wakati hawana ubavu wa kutenda jambo lolote.

"Kazi yao ni ulalamishi na kususa wakati Serikali ndiyo inayojenga zahanati, barabara, kupeleka miradi ya maji, umeme na kusaidia Wakulima na Wafanyakazi" Alisema Shaka
 
Shaka anatabiri baada ya January inafuats February

Lowassa hajawahi kuhama CCM

Wanamtandao wenzake walichangishana kununua Chadema ili wagombee Urais tu kwa kuwa CCM ilimkataa
 
Atarejea mara mbili?!!.......huyu mla urojo hajitambui!
 
Hii hatua ni nzuri kuelekea kufa kwa vyama
vyote vya upinzani.Watu wengine wanashangilia
lakini tunasahau kuwa wakati wa chama kimoja
hakuna aliyekuwa na haja ya kuangalia/kusikiliza bunge
labda wenye ndugu bungeni maana kulikuwa hakuna mawazo
mbadala.
Naona Tunaelekea huko,na kwa sasa hatuwezi
kuona madhara yake mpaka hapo
Mh.Magufuli atakapomaliza muda wake
chama kikashika hatamu,wafanyakazi hewa
wakarudi,wanafunzi hewa wakarudi,mishe mishe za bandarini
zikarudi n.k bila wapinzani,watakaoitwa tumbiri bungeni
kwa kusema ukweli,na bila wapinzani wa kuibua ESCROW account issues
Hapo ndipo tutakaposema heri nyakati zilizopita.

Ni bora upinzani ungeendelea,ukapewa nafasi ya kuhoji
ila ukakosa la kuhoji kwa sababu ya nyanja zote kuhimalishwa na serikali
na usimamizi mzuri wa bunge unaoongozwa na chama chenye wabunge wengi.

Mimi nitaendelea kuunga mkono mambo yote mazuri
yanayotendeka chini ya uongozi wa rais magufuri
lakini nikiangalia hotuba zake zote najiridhisha kuwa
bila yeye na bila upinzani imara mara baada ya muda wake tutarudi tulikotoka.
Waliouza viwanda vya mwalimu Nyerere hawajafa
kama wamekufa bado wenye mawazo kama hayo
bado wanaishi watauza na hivi vya mh.Magufuri
kama hawatadhibitiwa.
Kwa maoni yangu upinzani ulitakiwa kuimarishwa
badala ya kufa.Ukiachia vile vyama vinavyoonekanaga
kwenye chaguzi tu,baada ya chaguzi huvisikii.
 
Hii hatua ni nzuri kuelekea kufa kwa vyama
vyote vya upinzani.Watu wengine wanashangilia
lakini tunasahau kuwa wakati wa chama kimoja
hakuna aliyekuwa na haja ya kuangalia/kusikiliza bunge
labda wenye ndugu bungeni maana kulikuwa hakuna mawazo
mbadala.
Naona Tunaelekea huko,na kwa sasa hatuwezi
kuona madhara yake mpaka hapo
Mh.Magufuli atakapomaliza muda wake
chama kikashika hatamu,wafanyakazi hewa
wakarudi,wanafunzi hewa wakarudi,mishe mishe za bandarini
zikarudi n.k bila wapinzani,watakaoitwa tumbiri bungeni
kwa kusema ukweli,na bila wapinzani wa kuibua ESCROW account issues
Hapo ndipo tutakaposema heri nyakati zilizopita.

Ni bora upinzani ungeendelea,ukapewa nafasi ya kuhoji
ila ukakosa la kuhoji kwa sababu ya nyanja zote kuhimalishwa na serikali
na usimamizi mzuri wa bunge unaoongozwa na chama chenye wabunge wengi.

Mimi nitaendelea kuunga mkono mambo yote mazuri
yanayotendeka chini ya uongozi wa rais magufuri
lakini nikiangalia hotuba zake zote najiridhisha kuwa
bila yeye na bila upinzani imara tutaruditulikotoka.
Waliouza viwanda vya mwalimu Nyerere hawajafa
kama wamekufa bado wenye mawazo kama hayo
bado wanaishi watauza na hivi vya mh.Magufuri
kama hawatadhibitiwa.
Ndugu unamiaka mingapi?ulitaka waangalie kupitia mbalamwezi?
 
Hivi Kurudi kwao CCM kutaongeza viwanda vingapi?!
WaTz tunashabikia upumbavu huu mpaka lini?! Mafanikio ya nchi siyo nani yuko Chama gani!!
 
Sijakuelewa mkuu,labda uliza kwa kiswahili.
Unieleweje wakati umefumba macho?ebu amka unawe uso halafu usome tena ulichoandika..na kisha nilichoandika,!!mnazaliwa kwenye Pampers halafu mnajifanya mnaijua hii nchi eeh.!
 
Kwa Lowassa hakuhitaji utabiri kujua kuwa ana Rudi CCM kinachotakiwa ni kujiuliza je CCM watakubali kumpokea mtu ambaye walikuwa wanamuita fisadi alipokuwa CHADEMA
 
Back
Top Bottom