Kagera Sugar yamfuta kazi kocha wake Mellis Medo

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
722
1,178
Klabu ya Kagera Sugar imefuta kazi kocha wake Mellis Medo baada ya matokeo mabaya ya timu hiyo msimu huu.

Kagera imechukua maamuzi hayo baada ya kocha huyo kuongoza timu hiyo kwenye mechi 14 za Ligi Kuu Bara tangu alipotangazwa kuwa kocha wa timu hiyo, Oktoba 17,2024.

Medo ambaye alitua Kagera akitokea kwa ndugu zao Mtubwa Sugar ndani ya mechi 14, amefanikiwa kushinda mechi mbili pekee akipoteza saba huku akitoa sare tano.

Awali timu hiyo ilikuwa chini ya Mganda Paul Nkata ambaye alitangulia kufukuzwa akiwa amewaongoza wakata miwa hao kwenye michezo saba ya kwanza, akishinda mmoja pekee.

Ingawa Kagera bado haijatangaza rasmi lakini Mwananchi linafahamu kwamba kocha huyo ameshaondolewa kwenye timu hiyo ambayo imerudi nyumbani kuanza maisha mapya bila ya Medo.

Chanzo: Mwananchi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom