Kagera, Mwanza, Geita, Kigoma na Singida zaongoza umasikini wa kipato

Safety last

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
4,236
1,411
Mikoa ya Kagera Mwanza,Geita,Kigoma na Singida imetajwa jana Bungeni kama mikoa ambayo wananchi wake ni maskini wa kipato kiasi wanashindwa hata mlo wa siku.

============

Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amewasilisha bungeni Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa Fedha wa 2016/17, huku akitaja mikoa mitano inayoongoza kwa umaskini nchini.

Dk Mpango alisema mikoa hiyo imebainika katika Tathimini ya Hali ya Umaskini kimaeneo iliyofanyika kwa kutumia takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 na utafiti wa Hali ya Kipato na Matumizi katika kaya ya mwaka 2012.

Aliitaja mikoa hiyo na asilimia ya umaskini kwenye mabano Kigoma (48.9), Geita (43.7), Kagera (39.3), Singida (38.2) na Mwanza (35.3).

Kwa upande wa wilaya umaskini mkubwa upo katika Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma na Biharamulo mkoani Kagera na takribani asilimia 60 ya watu wapo chini ya mstari wa umaskini wa mahitaji ya kimsingi.

“Hii ina maana kuwa maeneo ya vijijini hususan pembezoni bado Watanzania wengi wanaishi kwenye umaskini na uwezo wao wa kupata mahitaji ya msingi mdogo,” alisema.

Dk Mpango aliitaja mikoa mitano yenye ahueni ya umaskini wa kipato kuwa ni Dar es Salaam (5.2), Kilimanjaro (14.3), Arusha (14.7), Pwani (14.7) na Manyara (18.3).

Pia, Dk Mpango alisema utafiti wa Hali ya Afya ya Mama na Mtoto, uliofanyika mwaka 2015 unaonyesha idadi ya wasichana waliopata watoto katika umri wa miaka 15 hadi 19 imeongezeka na kufikia asilimia 27 mwaka 2015 kutoka asilimia 23 mwaka 2010.

“Kuongezeka kwa wasichana wanaopata watoto wakiwa na umri mdogo, yaani miaka 15 hadi 19 siyo dalili nzuri kwani inaashiria kuongezeka kwa utegemezi na kudumaza jitihada za kuondoa umaskini katika jamii,” alisema.

Kuhusu wastani wa pato la kila mtu, Dk Mpango alisema pato la wastani la mtu limepungua kutoka Dola 1,047 za Marekani kwa mwaka 2014 hadi Dola 966.5 mwaka 2015.

Alisema hali hiyo imetokana na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania. “Hivyo ni dhahiri kuwa bado kunahitajika msukumo zaidi wa kuongeza ukuaji wa Pato la Taifa ili kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya kufikia Dola 3,000 za Marekani kwa pato la kila mtu na kuwa nchi ya uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025,” alisema.

Kuhusu urahisi wa kibiashara, Dk Mipango alisema taarifa ya urahisi wa kufanya biashara ya Benki ya Dunia (WB) ya mwaka 2015 , Tanzania ilipanda kwa nafasi moja katika vigezo vya urahisi wa kufanya biashara kwa kushika nafasi ya 139 kati ya nchi 189 duniani ikilinganishwa na nafasi ya 140 mwaka 2014. Alisema mwaka wa fedha 2016/17, Serikali imetenga Sh11.8 trilioni sawa na asilimia 40 ya bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
 
Lindi na mtwara sumbawanga wamekuwa lini matajiri

The future of Tanzania is in Lindi, Mtwara, Rukwa, Katavi, Ruvuma, Iringa, Njombe and Mbeya....Nenda katika mikoa hii na ufanye utafiti wako uone ni nini namananisha....in 30 years to come Kilimanjaro, Arusha and Kagera zitadidimia chini katika kiwango cha kutisha, hakutakuwa na uwekezaji tena wa ndani...Mikoa hiyo niliyoitaja mwanzo ina 'virgin' land ambayo haijawa exploited...vijana wake ni wachapa kazi...Tatizo la Kilimanjaro ni kuwa hakuna ardhi ya kutosha, wakazi wake wanahamia mikoa mingine, na kuwekeza katika mikoa mingine... Mkoa kama KIGOMA ni potential lakini unaathiriwa na wakimbizi...
 
Mikoa ya Kagera Mwanza,Geita,Kigoma na Singida imetajwa jana Bungeni kama mikoa ambayo wananchi wake ni maskini wa kipato kiasi wanashindwa hata mlo wa siku.
source;Bungeni na magazeti
Hizi porojo zisizo na chanzo cha uhakika haziwezi kujadiliwa na Great Thinkers.
 
Huyo mwalimu wako wa uchumi hapo ndo amekufundisha hivyo.......kumbuka marekani ni wawekezaji wakubwa kwenye mataifa maskin,je marekani imekuwa maskin,imepitwa na Africa? ukijibu swali hilo utakuja kujua kuhusu future ya mikoa ya kaskazini itakuwaje.......
 
Tafuta na takwimu Mikoa hii huwa inachagua upande gani wakati wa uchaguzi mkuu tuone kama kuna chochote cha kuchangia kwenye uzi huu
Kagera na mtwara wameanza kujitoa kwenye makucha ya kuichagua ccm ila kabla ya miaka 10 iliyopita walikuwa ni iyela iyela iyela
 
Aise Dodoma haipo, huu mji unaendelea kwa mwendokasi ktk kila nyanja shda ya maji imekuwa historia hasa maeneo ya mjini, mji umepangika sijui mwaka gani foleni ndo ztaanza
Hayo ndiyo maendeleo na sifa nyingine ni kuichagua ccm kwa kishindo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…