BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 497
- 1,202
Jamii Forums pazeni sauti kuna mtoto wa kidato cha pili amebakwa na Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera wakati akifundishwa tution.
Mtoto ni Mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Kagondo.
Kwa sasa mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana anatamba.
Atuhumiwa aliyefanya kitendo hicho anafahamika kwa jina moja Jovine
============
Mama wa mtoto huyo ambaye anatambulika kwa jina la Kokwenda, anaelezea ilivyokuwa:
“Ni kweli tukio hilo lilitokea tarehe 2 Januari 2023, alikuwa akijifunza masomo ya ziada tangu tarehe 13 Desemba 2022.
“Aliyekuwa akimfundisha anatambulika kwa jina la Jovin, ni mtu mzima flani hivi, siku ya tukio baada ya huyo baba kumfanyia unyama binti akarudi nyumbani akiwa analia.
“Nikaenda kuripoti Polisi, wakatuelekeza kwenda Hospitali baada ya kutupatia PF3, tukaenda kufanya vipimo, tukapata majibu, kwa kuwa ilikuwa jioni ikabidi tusubiri kesho yake ndio tukapeleka majibu Kituo cha Polisi cha Mutwe ambapo ndipo eneo tunaloishi.
“Polisi wakaanza kumtafuta mtuhumiwa, alikamatwa kama baada ya siku tatu hivi, ilikuwa Ijumaa, akawekwa ndani kwa siku mbili akatolewa kwa dhamana.
“Baadaye mtuhumiwa alipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Muleba, nilikutana na mpelelezi akaniambia ataniita kunijulisha kinachoendelea, walisema hii kesi inasimamia na Jamhuri hivyo watatuita tutakapohitajika.
“Sijui kinachoendelea kwa kuwa sijaambiwa chochote.
“Mwanafunzi hakuwenda shule kwa wiki kadhaa tangu kutokea kwa tukio hilo, baadaye mwalimu Mkuu akaniambia kutokana na kilichotokea anashauri tumhamishe shule mtoto kwa kuwa inaweza kumuathiri kisaikolojia.”
Kuhusu mtuhumiwa, mama wa mwathirika anasema "Mtuhumiwa alinitafuta mwanzoni ili tuyamalize lakini sikumsikiliza, tangu alipokamatwa hakuwahi kunitafuta tena."