Kagera: Mtoto wa siku mbili atupwa chooni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,106
10,176
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kagera limefanikiwa kumuokoa mtoto mchanga aliyekuwa ametupwa chooni jana tarehe 01 Desemba, 2021 huko wilayani Karagwe kata ya Bugene katika Mtaa wa Lukajage.

Mtoto huyo wa Kiume anayesadikiwa kuwa na umri wa Siku Mbili alitupwa katika choo hicho na mtu ambaye hakufahamika mara moja na sasa yupo katika Hospitali ya Kayanga Wilayani Karagwe akiendelea na matibabu. Jeshi la Polisi Mkoani Kagera linaendelea na uchunguzi ili kumbaini mama wa mtoto huyo.

Kaimu Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji (M) Kagera Mkaguzi Thomas Majuto amesema, walipata taarifa kwa njia ya simu na kuwahi kufika eneo la tukio kisha kufanikiwa kumuokoa Mtoto huyo. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)


Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji S/Sgt Karata Ramadhani Karata akimpatia huduma ya kwanza mtoto mchanga aliyemuokoa kutoka katika shimo la choo alikokuwa ametupwa huko Mkoani Kagera, Wilaya ya Karagwe Kata ya Bugene tarehe 01 Desemba, 2021

MICHUZI Blog
 
Back
Top Bottom