Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,330
- 4,692
Bweni la wavula katika shule ya msingi na sekondari Istiqaama inayomilikiwa na taasisi ya dini ya Kiislamu iliyoko kata Nshambya katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, limeteketea kwa moto jana jioni na kusababisha mali zote za wanafunzi zilizokuwa katika bweni hilo kuteketea.
Akizungumza katika eneo la tukio kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji katika mkoa wa Kagera Zabron Muhumha amesema kuwa bweni hilo lenye vyumba nane lina uwezo wa kulaza wanafunzi 70 na kwamba hakuna madhara kwa binadamu.