Kafulila utuelewe; hatukatai kununua umeme japo tuna ziada ya uzalishaji; hofu yetu ni kuambiwa tuna transmission cost kubwa na mbadala ni Ethiopia

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
12,867
22,957
Nadhani hawa watu wanaojiita viongozi wetu aidha wana tatizo la kujieleza, au wanapenda kufanya mambo kwa kuficha ficha vitu. Sasa huyu Kafulila, ambaye siku hizi amejifanya msemaji wa serikali au Raisi Samia, anauliza kuna ajabu gani Tanzania kununua umeme toka nje wakati tuna ziada, akitoa mifano ya nchi kadhaa zinazofanya hivyo. Nadhani toka ahamie CCM Kafulila anajitoa akili kwa kasi sana.

Kafulila asidhani kwamba sisi hatuelewi logic ya kununua umeme toka nje wakati tuna ziada. Tatizo limeanza kwa Raisi Samia na wasemaji wake pale waliposema tutanunuua umeme toka Ethiopia kwa sababu ya transmission losses cost kwenda mikoa ya Kaskazini ni juu sana. Mtu yeyote mwenye akili atakushangaa ikiwa utatoa sababu kama hiyo kwa nini tununue umeme toka Ethiopia.

Kama tungeelezwa tutanunua umeme toka Kenya kwa ajili ya mikoa ya kaskazini sidhani kama kungekuwa na maswali mengi.

Sasa nyie wanasiasa (sijui kama Kafulila bado ni mwanasiasa) kama mmeamua hamtaki mikataba ya mambo kama haya iwekwe wazi, acheni kuja na majibu mepesi mepesi na ya kisiasa kwenye masuala kama haya. Leteni majibu ya kisayansi.

Kwa mfano, ukisema tunanunua umeme toka Ethiopia, wenye akili wanaelewa kwamba transmission losses kati ya line za Tanzania na Ethiopia ziko hivi;
  • Ethiopia HVDC line transmission losses ~1-2% per 100 km
  • Tanzania HVAC lines transmission losses ~3-5% per 100 km
Sasa mtu atataka umweleweshe, ni kwa vipi gharama za transmission losses kwa umeme toka Ethiopia zitakuwa chini ya zile za Tanzania. Halafu kuna mtu wa serikali na cheo kikubwa anajiona kuwa na akili anaposema kama kuna hasara sio juu yetu ni ya Ethiopia. Wa-Ethiopia ni wajinga kiasi gani ambao wako tayari kuuza umeme kwa hasara? Hivi mnawaokota wapi watu kama hao na kuwapa nafasi walizonazo serikalini?

Na ukisema tutanunua umeme toka Ethiopia kwa gharama nafuu kwa kila uniti, mtu atataka kujua, je mkataba huo ni wa muda gani, na una kipengele cha gharama kutopanda kwa muda gani. Maana Ethiopia sio wajinga. Leo wanaweza kukuambia tutakuuzia kwa gharama nafuu, na baada ya muda wanakuambia tunapandisha bei ya umeme kwa zaidi ya 100%, na wewe unakuwa umeshajifunga kwenye mkataba labda wa miaka 50. Ukijitoa unaambiwa na mahakama za kimataifa uwalipe fidia Ethiopia kwa kuvunja mkataba. Kwani ujinga wa kulipa fidia mikataba tunayovunja umetokea mara ngapi hapa Tanzania? Sasa hilo ndio linafanya tusiwaamini wewe Kafulila, Raisi Samia, na wasemaji wa serikali na wizara ya nishati.

Kama hamtaki tuseme juu ya hili, wekeni huo mkataba wazi tuuchambue basi. Hamjajifunza tu kutokana na yaliyotukia mkataba wa bandari kwa DP world? Mnaficha ficha nini?
 
Alichosema Kafulila

1741763503611.png
 
By the way, suala la kununua umeme nchi nyingine linaleta mtafaruku kati ya USA na Canada, ambapo Canada imetangaza kuongeza bei ya umeme inaoiuzia USA kwa 50%.

Japo sikubaliani na Trump katika mambo mengi, sikiliza alihosema juu ya kuwa tegemezi wa nchi nyingine katika masuala ya umeme;

"Why would our Country allow another Country to supply us with electricity, even for a small area? Who made these decisions, and why? And can you imagine Canada stooping so low as to use ELECTRICITY, that so affects the life of innocent people, as a bargaining chip and threat?" Trump vented on his Truth Social app.

Canada inauza umeme kwa kaya karibu milioni 1.5 huko USA katika miji ya Minnesota, Michigan na New York.

Bwana Kafulila, unapaswa kuelewa kwamba kama Kigoma wanapenda kula numbu, si mikoa yote watazipenda numbu!
 
Nadhani hawa watu wanaojiita viongozi wetu aidha wana tatizo la kujieleza, au wanapenda kufanya mambo kwa kuficha ficha vitu. Sasa huyu Kafulila, ambaye siku hizi amejifanya msemaji wa serikali au Raisi Samia, anauliza kuna ajabu gani Tanzania kununua umeme toka nje wakati tuna ziada, akitoa mifano ya nchi kadhaa zinazofanya hivyo. Nadhani toka ahamie CCM Kafulila anajitoa akili kwa kasi sana.

Kafulila asidhani kwamba sisi hatuelewi logic ya kununua umeme toka nje wakati tuna ziada. Tatizo limeanza kwa Raisi Samia na wasemaji wake pale waliposema tutanunuua umeme toka Ethiopia kwa sababu ya transmission losses cost kwenda mikoa ya Kaskazini ni juu sana. Mtu yeyote mwenye akili atakushangaa ikiwa utatoa sababu kama hiyo kwa nini tununue umeme toka Ethiopia.

Kama tungeelezwa tutanunua umeme toka Kenya kwa ajili ya mikoa ya kaskazini sidhani kama kungekuwa na maswali mengi.

Sasa nyie wanasiasa (sijui kama Kafulila bado ni mwanasiasa) kama mmeamua hamtaki mikataba ya mambo kama haya iwekwe wazi, acheni kuja na majibu mepesi mepesi na ya kisiasa kwenye masuala kama haya. Leteni majibu ya kisayansi.

Kwa mfano, ukisema tunanunua umeme toka Ethiopia, wenye akili wanaelewa kwamba transmission losses kati ya line za Tanzania na Ethiopia ziko hivi;
  • Ethiopia HVDC line transmission losses ~1-2% per 100 km
  • Tanzania HVAC lines transmission losses ~3-5% per 100 km
Sasa mtu atataka umweleweshe, ni kwa vipi gharama za transmission losses kwa umeme toka Ethiopia zitakuwa chini ya zile za Tanzania. Halafu kuna mtu wa serikali na cheo kikubwa anajiona kuwa na akili anaposema kama kuna hasara sio juu yetu ni ya Ethiopia. Wa-Ethiopia ni wajinga kiasi gani ambao wako tayari kuuza umeme kwa hasara? Hivi mnawaokota wapi watu kama hao na kuwapa nafasi walizonazo serikalini?

Na ukisema tutanunua umeme toka Ethiopia kwa gharama nafuu kwa kila uniti, mtu atataka kujua, je mkataba huo ni wa muda gani, na una kipengele cha gharama kutopanda kwa muda gani. Maana Ethiopia sio wajinga. Leo wanaweza kukuambia tutakuuzia kwa gharama nafuu, na baada ya muda wanakuambia tunapandisha bei ya umeme kwa zaidi ya 100%, na wewe unakuwa umeshajifunga kwenye mkataba labda wa miaka 50. Ukijitoa unaambiwa na mahakama za kimataifa uwalipe fidia Ethiopia kwa kuvunja mkataba. Kwani ujinga wa kulipa fidia mikataba tunayovunja umetokea mara ngapi hapa Tanzania? Sasa hilo ndio linafanya tusiwaamini wewe Kafulila, Raisi Samia, na wasemaji wa serikali na wizara ya nishati.

Kama hamtaki tuseme juu ya hili, wekeni huo mkataba wazi tuuchambue basi. Hamjajifunza tu kutokana na yaliyotukia mkataba wa bandari kwa DP world? Mnaficha ficha nini?
Wanaotuongoza hawana Akili TIMAMU kama ss wananchi hilo ndio tatizo kubwa kwa Tanzania yetu.
 
Hivi, mtu anapokuwa na akili timamu akakubali kuongozwa na mtu asie na akili, nani hapa tatizo? Labda tatizo ni sisi Watanzania tunaokubali kuongozwa na watu wasio na akili
 
Back
Top Bottom