David Kafulila CEO wa PPP-Cetre nchini na Nehemia Mchechu Msajili wa hazina nchini mnatuchanganya Watanzania,
Kafulila na Waziri Mchengerwa kwa nyakati tofauti tofauti walifafanua vizuri ya kwanini wanatamani mradi wa DART uendeshe kwa Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi.
Kwa hali ya mwendokasi ilivyo sasa Kila mmoja alikubaliana na Bw Kafulila pamoja na Waziri Mchengerwa kuwa ili kupata ufanisi unaotakiwa mradi huu lazima pawepo na Mbia kwani ni kama uendeshaji wa faida umetushinda Watanzania.
Kafulila alituhakikishia kupitia PPP Mbia tayari ameshapatikana na kilichobaki ni kusaini mkataba ili mwekezaji ashushe zaidi ya Mabasi 177 ya kuanzia.
Watanzania tulio wengi tuliona ni bora zaidi kama mtu au kampuni itanunua Mabasi kwa Fedha zake na kuja kuyaendesha kwa Ubia na Serikali na Serikali kupata vipato mbalimbali ikiwemo Kodi, Hakika hili lilikuwa ni jambo jema kwa Taifa.
Tujiulize, Mbona ABOOD, KATARAMBA na wenzao ndivyo wanavyofanya kwani wanatoka huduma Kwa wananchi bila kuiingiza Serikali kwenye madeni ya kujitakia kama haya ya Mchechu na NMB.
Sasa Msajili wa hazina Bwana Nehemia Mchechu anataka kukopa pesa $30M zaidi ya TZS 80 milioni, tukumbuke hii hapa ni kabla ya riba ili kununua mabasi ambayo tumeambiwa tayari mwekezaji anakuja na mengine mapya 177 ya kuanzia,
Kwa msiofahamu bei ya kila basi ni karibu $300,000 kwa maelezo ya Waziri Mchengerwa, sasa kama Mabasi ni 100 íli kuyanunua lazima tukope sawa na jumla ya $30 milioni ambazo ni sawa na TZS 80 bilioni sijajua kuhusu riba kwa kuwa huu ni Mkopo wa kibiashara.
Sasa Kafulila alisema Mbia anunue aendeshe, leo Mchechu amesema serikali inunue iendeshe kitu ambacho imeshashindwa hapo kabla ndio ikawa sababu ya kutafutwa kwa. Mbia huyu.
Leo tena tunaambiwa ununuzi wa mabasi mapya tena kwa mkopo wa kibiashara, ila nchi ngumu sana hii.
Waziri wa Fedha hebu simamia hii na toa ufafanuzi kwani jambo hili linampiganisha Mhe Rais, ili ijulikane kama tunakopa kununua mabasi 100 basi hatuna haja ya Mbia wa mabasi 177 kama tunaleta Mbia hatuna haja tena ya kukopa NMB.
Pia soma <<Kafulila: Tunatekeleza agizo la Waziri Mchengerwa ndani ya muda mfupi ujao DART itasaini mkataba na Mbia nia ni kupunguza gharama Kwa wananchi>>>