CARDLESS
JF-Expert Member
- Apr 2, 2017
- 7,820
- 15,871
Maisha yamebadilika sana, watu wameongezeka sana, utandawazi nk.
Vyuo, vimeongezeka na wahitimu wameongezeka maradufu.
Hali ya Ajira ni changamoto sana kwa vijana hawa. Hali hii imepelekea mrundikano mkubwa wa wahitimu mbalimbali nyumbani.
Katika hali kama hii ndipo suala la usaili liliasisiwa, kuchuja na kupata wahitimu bora zaidi ili waweze ajiriwa.
Katika nchi yetu hii, kumezoeleza kada za Elimu na Afya wanaajiriwa bila kufanya usaili wowote. Hali imepelekea matatizo mengi zaidi.
Moja, nani anaona mchakato wa ajira kama ulienda kwa haki? Waliochaguliwa ni kweli walichaguliwa kwa haki kuliko walioachwa.
Mbili, Umahiri wao unatambulikaje kwa kuamua kuajiri bila kuwasaili? Watoto wetu watapata waalimu bora? Sisi tunapata huduma bora za afya kwa mtindo huu.
Tatu, wana uhakika gani kuwa huyu anayeajiriwa kama anaweza kumudu kuishi na watoto wa watu.
Vijana wanakosa kazi kwa visingizio ambavyo sio sahihi, haiwezekani mtu au kundi dogo la watu linachakata majina watakayo na kuchapisha kuwa hawa wamepata ajira hawa wamekosa.
Kwanini Walimu na Wahudumu wa Afya wasifanya usaili?
Serikali sasa ianze kuwafanyia usaili Kada za Elimu na Afya ili kuondoa malalamiko na kumpa kila mtu haki ya kujitetea juu ya kile alichosomea.