A
Anonymous
Guest
Huu ni mwezi wa tatu sasa tunafuatulia malipo hayo, awali tuliambiwa tujaze fomu za kuonesha uhitaji wetu wa malipo hayo lakin juzi tumepewa majibu yaliyotolewa kwa barua, yametukatisha tamaa.
Tumejibiwa na Mkurugenzi kuwa tutapatiwa endapo hali ya kifedha itakapotengemaa, sasa tunajiuliza lini hali ya kiuchumi itakaa sawa?
Tunaomba kilio chetu kifike kwa Wizara ya Afya kuwa Watumishi tunahitaji malipo hayo kwa kuwa tunajua ni haki yetu, watusaidie kupata, yatatusaidia kujikimu kwani wengi wetu ndio kwanza tunaanza maisha na tulitarajia kutumia kulipa kodi na mahitaji mengine ya msingi.
Pia soma ~ Ajira mpya kada ya afya halmashauri nyingi hatujapokea fedha za kujikimu toka November 2024