Kabla hujafanikiwa wewe ni lazima mtu huyu afanikiwe kwanza

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
KABLA HUJAFANIKIWA WEWE NI LAZIMA MTU HUYU AFANIKIWE KWANZA

Ndio kila mmoja wetu anapenda mafanikio makubwa kwenye maisha.

Lakini jambo moja la ukweli ambalo huenda hujawahi kulipa uzito ni kwamba mafanikio yako hujiletei wewe mwenyewe.

Kwa dunia tunayoishi ambayo kila kitu unamtegemea mwingine, huwezi kusema kwamba utajipa mafanikio yako wewe mwenyewe.Mafanikio yako yatatoka kwa watu wengine.

Yaani wengine ndio watakufanya wewe ufanikiwe, japokuwa malengo, mipango na juhudi utaweka wewe mwenyewe.

Hivyo basi kabla wewe hujafanikiwa kuna mtu au watu ambao inabidi wafanikiwe kwanza. Na watu hawa watafanikiwa kupitia wewe. Yaani wewe utawafanya hawa wafanikiwe, halafu na wao watakufanya ufanikiwe.Ni raha iliyoje!

Sasa je ni nani unatakiwa kumfanya afanikiwe?Kwako wewe ni yule ambaye anategemea kile unachokifanya.

Kama unafanya biashara basi biashara yako imwezeshe mteja wako kufanikiwa na mteja atakuwezesha wewe kufanikiwa. Kwa kuendelea kuwa mteja wako na kuwaambia wengine pia.

Kama umeajiriwa hakikisha unamwezesha mwajiri wako kufanikiwa na yeye atakuwezesha wewe kufanikiwa pia. Na pia wale wanaopokea huduma unayotoa wawezeshe kufanikiwa, na wao watakuwezesha pia.

Kama mwanamuziki hakikisha huwaangushi mashabiki wako kwani ndio wateja wakubwa wa kazi zako fanya kazi kwa makini na kutolipua.

Kama mwanasiasa hakikisha unatimiza ahadi zako ulizoweka wakati wa campaign unaona jinsi ambavyo tupo kwenye dunia ya kuwezeshana?

Haya nimeshakuwezesha wewe kwa kukupa maarifa ya kutumia nguvu ya uwezeshanaji. Niwezeshe na mimi kuwafikia wengi zaidi, kwa kushare na marafiki zako wote link ya makala hii ili nao wajifunze.

Na tuendelee kuwezeshana, ili kwa pamoja tufikia mafanikio makubwa.
 
Ukubali ukatae ukweli utabaki kama ulivyo. Mwajiri akiridhishwa na juhudi zako atakutuza kwa njia yoyote....ndo mwanzo wa mafanikio yako baada ya yeye kufanikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…