Juma Mgunda ameridhika kuwasaidia kufundisha Simba SC na kusahau kuwa ana 'profile' kubwa katika Ligi ya Tanzania

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,573
13,408
Imekuwa kama dharau kwa mzawa kocha Juma Mgunda kila timu inapopoteana (mwendelezo mbovu) na makocha wa kigeni kutimuliwa timu ya Simba sc huwa inamkubuka Juma Mgunda na kumpa timu tena.

Nani asiyejua uwezo wa Juma Mgunda katika ligi hii? Juma Mgunda siyo wakufanya kibarua cha saidia fundi ila anastahili kupewa timu kama kocha mkuu, na kitu kikubwa ni Juma Mgunda kuendelea kudumaza uwezo wake kwa kuendelea kung'ang'ania Simba SC na ndiyo maana anatumika kama mpira kisha anawekwa kwenye dastbini

Ndiyoo!!!! Mgunda siyo kocha wa kwenda kufundisha wanawake au kwenda kufundisha vikundi vya vijana tena vijana wenyewe wanatengenezwa kisiasa tu lakini ukija kwenye uhalisia ni uongo mtupu

Mgunda atapewa heshima yake endapo ataondoka simba sc na kwenda kufundisha timu nyingine za ligi kuu kama coastal, namungo nk, maana anweza kua kocha mkuu kwenye timu yoyote ukitoa simba na yanga

Maoni yangu: Binafsi ninaheshimu sana uwezo wa Mgunda ila kitendo cha kupewa timu kila makocha wanapoondoka siliungi mkono na kumuona mgunda hana msimamo bali anafurahi sana kiuwa saidia fundi.
 
Kama analipwa kama walivyokuwa wanamlipa Benchika Haina shida
 
Hivi kuna watu waliomuonyesha dharau Mgunda kama Yanga? Kutoka kumkejeli kwa jeans yake, kumuita andazi na juzi aliporudishwa tena kejeli za "mpira wa nazi". Haya yote hayatoki kwa watu wa Simba.
 
Naunga mkono hoja. Pengine unaweza hisi mgundq na matola wanahujum timu
 
Hivi kuna watu waliomuonyesha dharau Mgunda kama Yanga? Kutoka kumkejeli kwa jeans yake, kumuita andazi na juzi aliporudishwa tena kejeli za "mpira wa nazi". Haya yote hayatoki kwa watu wa Si

Mgunda ana familia inamtegemea.

Akienda Coastal hupokea milion 48 Kwa mwaka.

Akishika dayworker Simba anapata milion 15 Kwa mwezi ambayo ni Zaid ya milion 180 Kwa mwaka.

Kupanga ni kuchagua.
ALISHAWAHI KUKAA MWAKA SIMBA SC
 
ALISHAWAHI KUKAA MWAKA SIMBA SC
Simba ilipomchukua Mgunda kabla ya Robertinho ndiyo ilimuheshimisha. Kabla ya hapo hakuna aliyekuwa anamzingatia kihiivyo kwenye masuala ya ukocha.

Na pamoja na kwamba nakuunga mkono kwamba huwa si kawaida makocha wanaofundisha wanawake wanapelekwa kwa wanaume au vice versa, lakini usidharau sana mpira wa wanawake maana nako kuna pesa sana siku hizi.
 
Imekua kama dharau kwa mzawa kocha Juma mgunda kila timu inapopoteana (mwendelezo mbovu) na makoca wa kigeni kutimuliwa timu ya simba sc huwa inamkubuka Juma Mgunda na kumpa timu tena

Nani asiyejua uwezo wa juma mgunda katika ligi hii? juma mgunda siyo wakufanya kibarua cha saidia fundi ila anastahili kupewa timu kama kocha mkuu, na kitu kikubwa ni juma mgunda kuendelea kudumaza uwezo wake kwa kuendelea kung'ang'ania Simba sc na ndiyo maana anatumika kama mpira kisha anawekwa kwenye dastbini

Ndyoo!!!! Mgunda siyo kocha wa kwenda kufundisha wanawake au kwenda kufundisha vikundi vya vijana tena vijana wenyewe wanatengenezwa kisiasa tu lakini ukija kwenye uhalisia ni uongo mtupu

Mgunda atapewa heshima yake endapo ataondoka simba sc na kwenda kufundisha timu nyingine za ligi kuu kama coastal, namungo nk, maana anweza kua kocha mkuu kwenye timu yoyote ukitoa simba na yanga

Maoni yangu : binafsi ninaheshimu sana uwezo wa mgunda ila kitendo cha kupewa timu kila makocha wanapoondoka siliungi mkono na kumuona mgunda hana msimamo bali anafurahi sana kiuwa saidia fundi
Wewe kama kocha, kufundisha timu ndogo ndogo (ligi kuu) ukalipwa 5M na kufundisha timu ya wanawake ukalipwa 15M

UTACHAGUA WAPI?

Anachokifanya Mgunda ni kama alichofanya Feitoto


Maslahi kwanza CV baadae
 
Simba na yanga ndio zinalipa hela nzuri sana kwa makocha ndio maana wanakomaa nazo

Simba na yanga zinavumiliwa sababu ya mishahara mikubwa
 
Back
Top Bottom