Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 127
- 362
Leo Julai 7, ni Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani ambayo ilipitishwa rasmi Novemba 2021, kupitia azimio namba 41 C/53 la Umoja wa Mataifa likiwa chini ya UNESCO.
Siku hii ilikuwa rasmi kwa lengo la kutambua mchango wa Kiswahili katika kukukuza tamaduni mbalimbali, kujenga hamasa na kukuza mazungumzo ya Kistaarabu duniani.
Maadhimisho haya yatapatia msisitizo umuhimu wa kujenga mifumo ya elimu yenye mnepo kwa kutumia utajiri uliomo kwenye utamaduni wa lugha ya Kiswahili.
Washiriki watafanya hivyo wakimulika masuala ya msingi kama vile:
Kwa nini elimu ya sanaa ni muhimu na ni kwa vipi inaweza kusaidia kuendeleza lugha ya Kiswahili?
Hali ya sasa ya ujumuishaji wa elimu ya sanaa kwenye nchi zinazozungumza lugha ya Kiswahili.
Je, inawezaje kuimarishwa zaidi ili kukuza utambulisho wa kitamaduni wa Kiswahili na urithi?
Ni changamoto zipi na mahitaji yapi yanahusiana na kujumuisha elimu ya sanaa ya kiswahili katika mitaala ya shule.
Je, ni manufaa yapi yamebainika kwa ujumuishaji wa aina hiyo?
Ni kwa vipi wasanii na wabobezi wa utamaduni wanaweza kuchangia kwenye kuendeleza na kuhifadhi lugha ya kiswahli, na ni dhima ipi wanayo katika kukuza ubunifu na kuimarisha utofauti wa kujieleza kitamaduni?
UMOJA WA MATAIFA