Juhudi za Lizaboni na MCC yake kumzuia Nape asiteme cheche zimegonga mwamba

Nibozali

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
572
1,055
Siku chache zilizopita aliandika lizaboni kumsihi Nappe asiifunue CCM yangu inayonuka uozo wa namna mbalimbali, lakini kijana kwa kujiamni na kusimamia kiapo cha chama chetu kusema kweli uongo kwangu mwiko, akafunguka.

Anaandika Lizaboni

Kwako Comrade Nape.

Nakusalimu kiongozi, pole na hongera majukumu ya kulitumikia Taifa.

Kiongozi ninakuandikia waraka huu lengo ni kutaka kujua kweli inayosambaa mitandaoni kuwa mnamo tarehe 8 Aprili, 2017 utakwenda jimboni kwako, na moja ya shughuli utakayoifanya ni kuongea na wapiga kura wako. Mimi sina shaka na wewe kuongea na wapiga kura wako hata kidogo, kwani ni kawaida kwa mbunge kuongea na wapiga kura wako. Kama ni kweli umepanga kufanya hivyo naomba uzingatie yafuatayo:

i. Naomba nikusihi sana tumia busara katika kuongea, kama busara itakushinda usiongee. Kuna tetesi kuwa endapo utafanya hivyo, ama ni wewe mwenyewe au jirani zetu, wameandaa kikundi cha kushangilia na kikiwa na mabango ambayo sio mema sana kwa chama chetu. Kama ni wewe jiulize mara mbili mbili.

ii. Umesema unakwenda kusema kweli, hakikisha kweli iwe kweli, kweli kweli, hata upande wako useme kweli yako, yaani udhaifu wako, usiseme udhaifu wa watu wengine tu, ukidhani wewe huna mawaa.

iii. Siku unaongea na waandishi wa habari uliowaandaa, ulisema umekipigania Chama, hili mimi sina shaka nalo hata chembe. Naomba nikukumbushe tu, ukirudia kusema hili, pia waambie hiyo ndio ilikuwa ajira yako katika Chama, na ulikuwa unalipwa ili ukipiganie Chama chetu. Kukipigania chama kwako wewe kunatofautiana sana na mabalozi ambao walipigana kufa na kupona ili chama kishinde, pasi malipo yoyote, lakini wewe ulikuwa unalipwa mshahara na stahiki zingine. Ingelikuwa ajabu kweli kweli kama Katibu wa Itikadi na Uenezi asikipiganie chama chake.

iv. Comrade, nakukumbusha tu wakati kulikuwa na dalili za wewe kuanza kupishana na Mwenyekiti wetu, kuna kundi la watu lilitokea likawa “linakutia hasira” kundi hili lilidiriki hata kukuambia ujiuzulu. Kundi hilo hilo ulipotolewa katika nafasi ya uwaziri, lilianza kukuzomea, likikuambia kwamba wewe ulikuwa mtesi wa wengine sasa nawe yamekukuta. Lilishadadia kusema Bunge live, sheria ya mtandao, mafisadi kukatwa 2015 ni wewe ulisababisha hivyo, ngoja uonje joto la jiwe. Kundi hili hili tena ndilo linaloeneza hiki unachotaka kufanya, nadhani hapa uwe mbayuwayu.

v. Nakusihi sana, mimi bado naona kuna nafasi ya kuwekana sawa, kama ulivyosema siku ile wakati unatolewa, kwamba hukuulizwa wakati wa kupewa Uwaziri, ni sawa. Lakini ulipopewa hukuitwa waandishi wa habari wala hukufanya maandamano jimboni kwako. Tumia busara Comrade, sasa kama kila kiongozi akitolewa katika nafasi yake akaitisha vyombo vya habari, itakuwaje? Kumbuka ulipokuwa mwenezi, ambapo ulipowatambua mawaziri mizigo, wengine walitolewa, lakini hawakuitisha vyombo vya habari.

Sina mengi Comrade, ni mimi mmoja wa watu waliokipigania chama na bado nasonga mbele kukipigania Chama pasi malipo yoyote kaka, tofauti na wewe uliyepigania chama wakati unalipwa mshahara mzuri tu na marupurupu.

Wasalaamu
 
Hakuna uozo uliofunuliwa, zaidi ya we we kufunua jina lake na kujiita wewe,
 
Yaani mkuu username pamoja na avatar yako ni dhihaka tupu.
 
Lizaboni anafanya kazi kwa kujitolea yaani bila malipo!Ana stahili pongezi dah.....hehehe

Ova
 
Mimi namshauri NAPE azungumzie masuala ya maendeleo katika jimbo lake, lakini akijisahau na kuanza kutoa impression as if alionewa kwa kuondolewa kwake Wizara ya Vijana na michezo basi akumbuke kwamba akianza kushutumu watu au kuwananga kwa njia moja au nyingine hilo linaweza kumfanya ajimalize kisiasa, NAPE achukulie kuondolewa kwake kazini kama ni ajali kazini basi, atulie kama wenzake walio wahi kuondolewa kazini, atafute shughuli nyingine ya kufanya mbona ziko nyingi tu.
 
Mimi sikuona cha maana alichoongea Nape kule Mtama,zaidi alitukumbusha UKOLONI wa kuwakanyaga makalio mama zetu
 
Nape ndo basi tena. Kwa wanao mshangilia wasubiri vingine. Kumbuka nape hapo mtana hana upepo mzuri. Na hizo muvi zake za jana ni za upepo uvumao kwa kasi. Uzamini alio upata hawezi upata tena 2020. Time will tell.
 
Weeee Nibozali wewe sio ndio Lizaboni au unafikiri tumesahau double account zako
 
Nafikiri watu hamjajua nini hasa kinampa hasira Nape, Nape kachukizwa sana na kitendo cha yeye kutumiwa wahuni na DAB na kushikiwa bastola kisha eti Polisi na vyombo vyote vimeshindwa kumkamata muhusika. Hiyo kwake ni dharau kubwa sana.

Pamoja na kushika madaraka ndani ya serikali na kukipigania chama chake kwa kiwango kile anaweza kufanyiwa mchezo mchafu kama ule hadharani? Tena ulioandaliwa na watu washamba kabisa ndani ya chama na serikali? Kwa kweli ana haki ya kutema nyongo yote. Na upande wa upinzani wana haki ya kumuunga mkono aseme kwani walishatahadharisha kuwa wakimaliza upande wao watarudi kutafunana wenyewe kwa wenyewe.

Nape ili anyamaze, yule kijana ambaye polisi wamemkana sio wao akamatwe na aseme alitumwa na nani. Maana pale Protea Hotel alikuwepo RPC wa Kinondoni, sasa mahali alipo RPC kiongozi anatolewa bastola kutishiwa (ingewezekana kuuwawa kama mwenye bastola angefanya uzembe kama wa Ditopile) halafu eti mtu anapotea hajulikani? Sasa watu wanamjua mbona polisi haiombi msaada kwa hao wanao mjua akamatwe?
Nape sio mjinga, endelea kutema nyongo kijana.
 
Acha ajimalize, kuna inputs za Nape kwenye uharibifu wa taifa hili.
 
Waganga njaa kama akina Lizaboni hawawezi kumzuia Nape kuongea. Nape is identified with the modern ccm. Sio hawa wanaosubiri hand out ya sh elfu saba kwa siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…