Jr. Farhan wa Clouds Tv huna uelewa wowote katika mahusiano ya mapenzi; huwezi kumhudumia Mwanamke uliyezaa naye baada ya kuachana naye ukabaki salama

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
25,488
61,136
JR. FARHAN WA CLOUDS TV HUNA UELEWA WOWOTE KATIKA MAHUSIANO YA MAPENZI; HUWEZI KUMHUDUMIA MWANAMKE ULIYEZAA NAYE BAADA YA KUACHANA NAYE UKABAKI SALAMA.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Sijui ulikuwa unatafuta sifa au kiki au vipi. Kama ni Kiki basi upo sahihi na hongera. Lakini kama ni kweli upo serious na ndivyo akili yako ilivyofikiri basi nasikitika kukuambia kuwa huenda unaupeo mdogo wa kufikiri, au huna ujualo kwenye mahusiano ya mapenzi, au umeanza mapenzi ukubwani.

Ushauri uliotoa wa Wanaume kuhudumia watoto wao ninakuunga mkono kwa asilimia mia moja. Lakini hukuweka msisitizo kwenye ushauri huo zaidi ushauri wa pili kuhusu kumhudumia Baby Mama anayemtunza mtoto ndio ulitilia mkazo kumaanisha ndio lengo la ujumbe wako.

Sasa sisi wanaume tunakuambia ya kuwa wewe bado huna ujualo katika sekta hiyo. Na zaidi umepuyanga.
Ati sababu kubwa ulizotoa ni kuwa Mwanamke kuhangaika na mtoto sijui kukojolewa, sijui kumbembeleza, hivi ulitaka nani afanye hayo kama sio Mama yake. Kama mama ameshindwa kuwa mama apeleke mtoto kwa Babaake.
Sisi wanaume tupo tayari kulea watoto wetu na hayo majukumu tunayaweza kwa asilimia zote.

Nikirudi kwenye hoja, nakupinga wazo lako ambalo nimeliita la kijinga au la mtoto ambaye bado hajabalehe kwa sababu zifuatazo;

1. Kuwa Mwanamke sio ulemavu, Mwanamke lazima naye afanye kazi ya uzalishaji.
Kuzaa hakumaanishi Mwanamke anageuka kilema.
Dunia ipo kwenye harakati za kupunguza utegemezi alafu kuna mijitu inaakili za kizamani. Lazima nguvu kazi zote za nchi zitumike.
Wapo wanawake wamezaa na sio mtoto mmoja na wanafanya kazi za uzalishaji na wanatunza watoto wao. Sio watoto tuu bali familia na ukoo wao.

Ndio maana vijana siku zote nawaambia epuka kuoa Mwanamke asiye na akili(mwenye mawazo ya kuhudumiwa hudumiwa kama mlemavu) na asiyefanya kazi.

Fikiria Wanawake nchi hii wapi 31milioni alafu kuna mijitu inahamasisha utegemezi. Inamaanisha nguvu kazi Milioni 31 iwe tegemezi hapo nini kitatokea kama sio taifa kuwa maskini.

Dada mmoja wa kizungu ambaye ni Rafiki yangu aliwahi kuniambia kuwa moja ya mambo yanayoikwamisha Afrika ni pamoja na mitazamo mibovu ya jamii kuhusu wanawake. Na wanawake wenyewe wamebweteka. Hawataki kufanya kazi wanataka kuhudumiwa kama maiti.
Huu ujinga ukomeshwe.

Wanaohudumiwa ni Watoto na wazee full stop.

Farhan unapozungumzia jambo hasa ukijijua upo kwenye nafasi ya kufahamika, jaribu kuangalia mbele zaidi na sio kuangalia ilipoishia pua yako.

2. Hakuna mahusiano mapya yatakayokubali umhudumie Baby mama Wako.
Kama vile sisi wanaume tusivyokubali wanawake wawasiliane na ma-ex wao ndio hivyohivyo Wake au wachumba wapya tulio nao hawatakubali tutoe huduma kwa Wanawake tuliozaa nao.
Watakubali tuwahudumie watoto ikiwezekana tuwalete nyumbani hao watoto lakini kamwe hakuna Mwanamke atakubali umhudumie Mwanamke mwingine hasa uliyekuwa naye kwenye mahusiano ati kwa kisingizio cha M/Watoto

Kwanza hakuna mwanaume kamili anayeweza kuwaza mawazo ya namna hiyo. Hakuna na hayupo isipokuwa mwanaume Mpumbavu.

Unapohudumia Mwanamke ULIYEZAA naye hiyo inatoa tafsiri hasi kwa Mchumba au mke mpya uliyenaye. Kwanza kiasili tuu hiyo itamaanisha kuwa bado anampenda na kumjali jambo ambalo nafasi hiyo unatakiwa umpe mkeo au mchumba mpya.

3. Hakuna mwanaume atakayekubali umhudumie mke au mpenzi wake kisa ulizaa naye watoto.

Kuoa single mother anayehudumiwa NI jambo lisilowezekana.
Kwanza utabidi mwanaume utoe zaidi ya kile anachotoa mzazi mwenzake, na pia Mwanamke huyo awe tayari kuachia hizo pesa ili abaki na wewe. Sioni kama kuna Mwanamke atakayekuwa tayari kuachana na pesa. Anaweza kukudanganya kuwa hapokei tena hizo pesa lakini kwa siri akawa anapokea.

Kuna jitu jinga litasema, mwanaume unatakiwa utoe pesa zaidi kwa mkeo au mchumba wako ili asitake pesa za Watu
Na mimi Taikon nasema, mwanaume Usitoe pesa zaidi ya uwezo wako kisa kumridhisha Mwanamke, kama hatosheki na pesa zako mwambie atembee na wala usibembeleze. Usijitese kwa ujingaujinga.
Ujinga waachie Wajinga.

4. Mwanamke atatumikia Wanaume wawili au zaidi wale aliozaa nao.
Fikiria Mwanamke amezaa na wanaume watatu alafu wewe ukamuoa. Hao wanaume wote wanamhudumia Baby mama wao.
Unafikiri nini kitatokea wewe popoma?
Pengine kwa akili za Watu Wengine zilivyo ndogo hawawezi jua nini kitatokea.
Ila elewa kuwa hakutakuwa na Familia tena, hakutakuwa na ndoa tena.
Mwanamke atazaa zake na wanaume hata saba kisha atawaacha wote na kusubiri maokoto.

Farhan, elewa kuwa hata huyo mchumba uliyenaye usidhani kuwa amefurahia kauli yako ya kijinga kama hiyo. Hiyo kauli haipaswi kutolewa na mwanaume aliyekomaa labda iwe kama ni Kiki tuu.

Huruma za kijinga waachie Watu wajinga na wale vipofu wasioona mbele.

Kwenye ushauri ulioshauri ulipaswa kushauri mambo makuu mawili matatu;
1. Watu wasiachane kiholela ili kupunguza matatizo kama single mothers na Watoto kulelewa na mzazi mmoja.

2. Wanawake wakishughulishe na mambo ya uchumi ili hata wakiachwa iwe kwa Kifo au talaka au kuzalishwa waweze kujihudumia.

3. Wanaume wahudumie watoto wao.
Full stop na sio kuleta mambo sijui ya huruma ya mikojo ya watoto utadhani mikojo ni sumu au kemikali za nyuklia.
Pumbavu!

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Upo sahihi Sana.
 
Yule bwanamdogo huwa ana ulimbukeni flani hivi,angalia asilimia 90 ya comment zinazomsapoti pale ni za wanawake as if yupo sahihi.
 
Back
Top Bottom