JPM kafanya mabaya haya hapa na mazuri haya hapa wana ccm mnakubali??

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,120
Tanzania kama taifa tumegeuka kuwa wanafiki sana kias kwamba tunalitia aibu taifa letu . Na hii tabia ya unafiki haijawa upande mmoja japo wengine wana nafuu ila wana ccm wanaongoza kwa unafiki. Sasa naomba tuwekane sawa kama wewe hauko miungoni mwa wanafiki hebu kanusha kwa kuweka point zako katika uzi huu ukijibu swali hili hapa.

Je JPM rais wa Tanzania kama kiongozi na huku akiwa binadam katika uongoz wake hajawahi kukosea tangu aingie madarakan??

Nimeuliza hivi kwa vile wanaccm wanawaponda wapinzani kwamba kila kitu wanakosoa lakn huku wao hawajawahi kukosoa hata siku moja. Kipindi alipokuwepo JK na akawa anasafiri safiri wapinzani waliweka uzi wa kuponda safari hzo lakn wana ccm walikua wanaziunga mkono mia kwa mia. Alipokuja JPM akazipunguza wakashangilia na kufurahi kana kwamba kuna siku huko nyuma waliwahi kukosoa. Huku walikua wanatetea. Sasa kati ya wana CCM wanasifia kila kitu na wanaokosoa kila kitu nini tofauti zenu?? Sasa mwana ccm jitofautishe hapa chini kwa kukosoa baadhi ya utendaji wa JPM kumbuka haiwezekan kama binadam yeye atende mema tu.

Mimi namuunga mkono kwa haya machache lakn nampinga kwa mengi sana.

Namkubali kwa sakata la kubaini watumishi hewa .

Nakubali kwa kupunguza safari za nje

Namkubali kwa kubana matumiz.

Hayo yote hapo juu yana kasoro zake kiutekelezaji ila naunga mkono nia iliyokuwepo.

Mabaya yake haya hapa chini.

Nampinga kuleta ukandamizaji wa kuongea
( freedom of speech)

Nampinga kwa kuzuia mikutano ya kisiasa kinyume cha katiba.

Nampinga kwa kubariki ujenzi wa uwanja wa ndege chato.

Nampinga kwa kuona umuhim wa kununua ndege nyingi kuliko kuboresha huduma za afya na mikopo kwa wanafunz.

Nampinga njia aliyotumia kutatua tatizo la sukari imepelekea bei kuwa juu mpaka sasa.

Mwisho nampinga kwa utendaji wake wa kujiamulia bajet yeye pasipo bunge rejea ununuz wa ndege za nyongeza ujenz wa kota za wanafunz na magereza achilia mbali pesa za uhuru wa Tanzania na pesa za muungano .

Je wewe ukiwa mtanzania mzalendo una lipi la kukosoa na kusifia?

Kumbuka usipokosoa unamaanisha huyu JPM hakosei. Hivyo unaungana na wale wanaosema
JPM amekua kama Mungu maana pekee ndiye hakosei. Na wafuasi wake wanamwogopa kumkosoa. Binafsi makosa anayo mengi sana tunapaswa kumkosoa sana tu!!
 
Jpm kafanya mazuri machache yenye kasoro nyingi ambazo hataki kuzirekebisha.
Na kafanya mabaya mengiii, ambaye yana kosa hata chembe ya uzuri na pia hataki kujirekebisha.
Ni rais wetu ndio hivo tena lakin ki ufupi he is arrogant.
 
Nampinga kuzuia ajira kwa muda wa mwaka mzima,

Nampinga kwa kutosuply democracy wakati nchi anajua ya democratic,

Nampinga kuwa yy ndo mwamuz wa kila kitu wakati kuna wizara na taasisi alizoweka watendaji,

Napinga zoez la uhakiki watumishi kwa miez7 huku mambo yote yamesimama ktk utumishi,

Napinga kujifanya yy hakosei na kuona kila kitu afanyacho ni sahihi,

Napinga kutokusikiliza mawazo na maoni ya wasaidiz au wananchi kwa kudai hataki kumdrive!

Napinga masitisho yanayoumiza na kunyima haki za watu,MF amesitishia watu ajira, amesitsha mikopo kwa wanafunz waliopata scholarship nje, amestisha mikutano ya siasa nk, hv ni baadhi ya unyimaji wa haki za binadamu,

Napinga kutokutoa taarfa kwa umma na kuendesha nchi kama familia ya mtu,

Napinga ununuz wa ndege 6 wakat dawa,walimu hakuna na mashuleni,hakna ajira, watu wanakufa kwa upungufu watumishi hospt na dawa hakna, huwez kujenga Nyumba bila kuanza na msingi!

Napinga mfumo wa matumiz ya pesa ktk vitu visivyokuwa vimepewa/kupangiwa bajet! MF ujenz wa uwanja chato, ununuz wa ndege nk,

Napinga ongezeko la 15% kodi mkopo elimu ya juu pasipokuwa na ongezeko la mshahara,

PONGEZI NI HIZI HAPA,

kajtahd kuleta heshma kwa watumishi na nidhamu ya kazi maana siku hizi hakna ndama Mtoto wa ng'ombe,

Kajitahd kuwa na malengo makubwa japo hawez kufika 3 bila kuanza na 1,

Kajitahid kupunguza matumiz ya pesa za umma,

Kajitahd ktoa elimu bure japo walimu hawatoshi,

Jajtahd kufanikisha uwepo wa madawati,

Kajitahid kutekeleza maudhui ya wimbo wa ccm uliotumika kwenye kampeni, namba imesomeka kweli, ccm mbele kwa mbele, wanavimba ila hawapasuki,

Amejtahd kunyamazisha wapinzani japo hajui wanafkr nn 2020,

Kajitahd kuzuia dili japo njia za kupiga dili mpya znaandaliwa,

Kajitahd kuwa ndo msemaji mkuu kwa kila idara,

Kajitahid kutumia hela za tetemeko la ardhi kuelekeza kwenye miundo mbinu za serikali huku wananchi wakilia na njaa,

Mmmmh hivi hiz ni pongez au?
 
Dude Mbona,huulizi,je Tanzania,ni Buchato tu,au Rungwa tu? maana ziara zinafanywa buchato na Ruangwa tu,na hivi mtawala wa nchi ya nyumbu,alichaguliwa na buchato tu,kuingine hatukuchagua,mbona hatutembelewi? pm naye na Ruangwa tu,je watz wenye matatizo wako buchato na Ruangwa tu?,maana frequency ya kutembelea huko inaongezeka kwa geometrical progression,wakati kuingine inapungua kwenda O(Z)kwa arithmetrical progression,yup or nope,dude?
siyo hivyo tu sisiem,ni vipofu kwa mabaya yote yanayofanwa na watu wao,ila mimacho mikali na miwani mikubwa kwa yanayofanywa na cdm
hapo wako tayari kutumia mamilion ya fedha hata kuharibu uchumi wa nchi,hata wa kusikia milio ya nyau tu wa cdm na raia wasio na silaha,,kumbuka ukuta
haikuwepo kabisa,lkn mamilioni yaliyotumika,yangesomesha hata vyuo vikuu karibu vyote vya nchi nzima
cdm walichokifanya ulikuwa mkwara tu,hakuna mtu ambayeangeandamana,lakini laa,mijamaa ikajikunja barabarani,
watu wenyewe waliokuwa wanawazuia hata jiwe tu walikuwa hawana,
 
Huwezi ukabana matumizi halafu bajeti ikaongezeka kutoka 22 trilioni mwaka wa fedha 2015/2016 na kufikia 29 trillion 2016/2017. Huwezi kubana matumizi halafu unatumia trilioni moja kununua ndege bila matumizi hayo kuidhinishwa na Wabunge na pia kufuata taratibu za manunuzi ya Serikalini.

Namkubali kwa kubana matumiz.
 
Mimi namuunga mkono kwa kumaliza tatizo la madawati once and for all.
Pili kupunguza idadi ya wanao lala chini pale Muhimbili. Kukomesha dili Bandarini, kutoa tenda za ujenzi kwa TBA (Tz Building Agency) badala ya kuzipa kampuni za wahindi na wachina. Pia kuzima ufisadi na wizi uliokua unaendelea kwenye UDART.
Kasoro zake ni;
1.) Kuzuia Bunge live.
2.) Kuzuia mikutano ya kisiasa.
3.) Kuendeleza Chuki kule Zanzibar badala ya kuleta mshikamano.
4.) Kuendesha mambo kwa zima moto na kwa mizuka.
5.) Kutoshaurika, hasa suala la Kuweka VAT kwenye utalii na kuongeza kodi Bandarini na pia VAT kwenye usafirishaji wa mizigo.
6.) Kuwavumilia mawaziri mizigo kama waziri wa Viwanda na biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…