Pre GE2025 Joshua Msigwa: Kanisa na Msikiti visiwe upande wa wavunja sheria kwa namna yoyote ile

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
1,124
2,194
Kiongozi wa kiroho na Mratibu wa Tanzania Peace Foundation (TPF) Kanda za Juu Kusini, Joshua Msigwa ameshangazwa na matamko yaliyotolewa hivi karibuni na baadhi ya Viongozi wa Dini kutaka kuachiliwa huru kwa mmoja wa Mahabusu ambaye ni Kiongozi wa Chama cha Siasa.

Ameongeza kuwa, Serikali ipo makini haijakurupuka na kumweka ndani Kiongozi huyo bila sababu.

Amewasihi Viongozi wa Dini kuheshimu mamlaka za Utawala kwani pindi Vyama hivyo vitakapoingia madarakani vitatakiwa kupewa heshma vilevile.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Kanisa na Msikiti visiwe upande wa wavunja sheria kwa namna yoyote ile" amesisitiza Msigwa.

Anaishi dunia gani huyu? Serikali ya CCM imeanza lini kuwa makini?
 
anajipendekeza na anajitoa ufahamu, mbona kama vile ni mpuuzi fulani hivi? Watu wanataka haki kwenye chaguzi halafu yeye anasema wanavunja sheria, huo si ni upuuzi? Mbona hata akili ndogo tu inang'amua vitendo vya hovyo kwenye chaguzi? Anataka kutetea wavunja haki, makanisa hayawezi kukakaa kimya yakiona haki zikivunjwa
 
Kiongozi wa kiroho? Anaongoza watu gani hao walio wapuuzi kiasi hicho, ina maana hao watu anaowaongoza huwa hawaoni matokeo ya chaguzi zisizo za haki yanayotoka? Hata bunge lililopo anashindwa kutambua ni bunge la aina gani lile, bunge gani lile linakuwa la chama kimoja wakati kuna vyama vingi vilivyoshiriki uchaguzi ukavurugwa ili tu kusiwepo na wapinzani bungeni? Kiongozi huyo ajenge hoja maridhiwa asilete upuuzi kwenye mambo muhimu yenye afya kwa taifa. Makanisa hayawezi kuwa ya kipuuzi si wajibu wake kukaa kimya haki zinaposiginwa
 
Aache ujinga.
Atazame mbele zaidi.
Kama tutaendelea kuwa na katiba hiihii na tume ya uchaguzi hiihii, tutaweza kufika salama mwaka 2040?.
Jibu ni hapana.
Kila mtu kwa upendo wake kwa taifa letu, ajishauri kutamani kuwa na tume huru, tena na katiba mpya kwa manufaa ya vizazi vijavyo na taifa endelevu.
Mungu Ibariki 🇹🇿.
 
Watu kama hawa wanaojiita viongozi wa kiroho ndio hutufanya wengine kuanza kuhoji imani zetu! Kutafsiriwa kwa biblia kutoka kiebrania kwenda kiingereza na hatimaye kiswahili kumesababisha hata wenye uwezo mdogo wa kufikiri kama huyu bwana kujiita manabii na mitume na kufungua makanisa ya kujipatia mlo.
 
Kiongozi wa kiroho? Anaongoza watu gani hao walio wapuuzi kiasi hicho, ina maana hao watu anaowaongoza huwa hawaoni matokeo ya chaguzi zisizo za haki yanayotoka? Hata bunge lililopo anashindwa kutambua ni bunge la aina gani lile, bunge gani lile linakuwa la chama kimoja wakati kuna vyama vingi vilivyoshiriki uchaguzi ukavurugwa ili tu kusiwepo na wapinzani bungeni? Kiongozi huyo ajenge hoja maridhiwa asilete upuuzi kwenye mambo muhimu yenye afya kwa taifa. Makanisa hayawezi kuwa ya kipuuzi si wajibu wake kukaa kimya haki zinaposiginwa
Hana tofauti na yule kimbaumbau wenu askofu mtia nia mwenye kichwa yenye crack MWAMAKULA
 
Kiongozi wa kiroho na Mratibu wa Tanzania Peace Foundation (TPF) Kanda za Juu Kusini, Joshua Msigwa ameshangazwa na matamko yaliyotolewa hivi karibuni na baadhi ya Viongozi wa Dini kutaka kuachiliwa huru kwa mmoja wa Mahabusu ambaye ni Kiongozi wa Chama cha Siasa.

Ameongeza kuwa, Serikali ipo makini haijakurupuka na kumweka ndani Kiongozi huyo bila sababu.

Amewasihi Viongozi wa Dini kuheshimu mamlaka za Utawala kwani pindi Vyama hivyo vitakapoingia madarakani vitatakiwa kupewa heshma vilevile.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Kanisa na Msikiti visiwe upande wa wavunja sheria kwa namna yoyote ile" amesisitiza Msigwa.

Huyo Msigwa naye atakuwa ni wale matapeli wanaotumia dini.

Anasema eti wanaovunja sheria, ni sheria gani iliyovunjwa?
 
Back
Top Bottom