Joseph Kusaga na ujio wa ‘Netflix’ ya Bongo

Nifah

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
33,536
76,855
IMG_5294.jpeg

Ni Joe Kusaga tena…
Waswahili husema mwenye nacho huongezwa, sio sahihi. Mwenye nacho hujiongeza ndipo huongezwa.

Mfanyabiashara na mwekezaji mkubwa nchini aliyejikita zaidi kwenye tasnia ya burudani, Joseph 'Joe' Kusaga yuko mbioni kuja na App itakayokuwa katika mtindo unaoshabihiana na App maarufu ulimwenguni, Netflix.

Ni App ya burudani…
Maudhui makubwa yatakayopatikana ndani ya App hiyo ni burudani. Zikiwemo series na movies za kibongo, habari za michezo na kutakuwemo pia na vipindi vya matukio ya wanamuziki wa Bongo Flava kama vile matukio wakati wa kuchukua video za nyimbo zao (behind the scenes)

Ni uwekezaji mkubwa!
Taarifa zinasema Joe Kusaga amefanya uwekezaji mkubwa sana katika App hiyo, kuanzia ununuzi wa vifaa vya kisasa vinavyosemekana kuwa na uwezo sawa na App nyingine kubwa za kimataifa kama Prime Video, Hulu, Netflix n.k

Pia itakuwa inapatikana kwenye TV za Smart na Android kama zilivyo hizo App nyingine.

Ni mradi wake binafsi.
Huu ni mradi binafsi wa Joe Kusaga nje ya miradi ya familia yake ambayo wanamiliki miradi mingi kwa pamoja ukiwemo Clouds Media Group.

Pia ni mradi wake bila ya ushirika kama ilivyo Wasafi n.k

Kuzinduliwa June mwaka huu
Mpango wa awali wa uzinduzi ulikuwa tarehe 9 June ambayo ni siku ya kuzaliwa ya Joe Kusaga, lakini kuna mambo yalitokea yakapelekea uzinduzi kusogezwa mbele.

Licha ya changamoto hizo zilizojitokeza, bado uzinduzi utafanyika tarehe yoyote ndani ya mwezi huohuo (June).

Kupitia chanzo changu nyeti,

Nifah.

UPDATES KUELEKEA UZINDUZI WA APP
Joseph Kusaga amewasilisha ombi rasmi kwa Rais kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa App yake, pia akipendekeza Rais awe mtu wa kwanza kulipia App hiyo.

APP ITAITWA AFROBOX
Jina rasmi la App limeshapitishwa, ni Afrobox.

PAMBANO LA HARMONIZE NA MWAKINYO LIVE…
Upo uwezekano mkubwa wa pambano la ngumi kati ya bondia Hassan Mwakinyo na Harmonze kuruka moja kwa moja kupitia App hiyo ya Afrobox, mratibu akiwa Joseph Kusaga.

Uptades kutoka kwa chanzo changu, tusubiri uzinduzi.
Nifah
 
View attachment 2975932
Ni Joe Kusaga tena…
Waswahili husema mwenye nacho huongezewa, sio sahihi. Mwenye nacho hujiongeza ndipo huongezewa.

Mfanyabiashara na mwekezaji mkubwa nchini aliyejikitika zaidi kwenye tasnia ya burudani, Joseph Kusaga yuko mbioni kuja na App itakayokuwa katika mtindo unaoshabihiana na App maarufu ulimwenguni Netflix.

Ni App ya burudani…
Maudhui makubwa yatakayopatikana ndani ya App hiyo ni burudani. Zikiwemo series na movies za kibongo, habari za michezo na kutakuwemo pia na vipindi vya matukio ya wanamuziki wa Bongo Flava kama vile matukio wakati wa kuchukua video za nyimbo zao (behind the scenes)

Ni uwekezaji mkubwa!
Taarifa zinasema Joe Kusaga amefanya uwekezaji mkubwa sana katika App hiyo, kuanzia ununuzi wa vifaa vya kisasa vinavyosemekana kuwa na uwezo sawa na App nyingine kubwa za kimataifa kama Prime Video, Hulu, Netflix n.k

Pia itakuwa inapatikana kwenye TV za Smart na Android kama zilivyo hizo App nyingine.

Ni mradi wake binafsi.
Huu ni mradi binafsi wa Joe Kusaga nje ya miradi ya familia yake ambayo wanamiliki miradi mingi kwa pamoja ukiwemo Clouds media.

Pia ni mradi wake bila ya ushirika kama ilivyo Wasafi n.k

Kuzinduliwa June mwaka huu
Mpango wa awali wa uzinduzi ulikuwa tarehe 9 June ambayo ni siku ya kuzaliwa ya Jose Kusaga, lakini kuna mambo yalitokea yakapelekea uzinduzi kusogezwa mbele.

Licha ya changamoto hizo zilizojitokeza, bado uzinduzi utafanyika tarehe yoyote ndani ya mwezi huohuo (June).

Kupitia chanzo cheti,

Nifah.
Hilo wazo nzuri ila malipo kwa wasanii yawe mazuri ili wakimbilie huko..
 
Napenda sana unavyotoa taarifa sio kama wale wapumbavu wengine wanajifanya kuweka code ili waonekane wa maana.

But....
Streaming channel ya kibongo itakayokua sawa na Hulu, Netflix, Amazon Prime au Disney+ hapo anatupanga. Bado sana... Kwa bongo. Na kwa content zipi tulizonazo??
 
Issue ni content hata Netflix yenyewe ipo mbioni kufeli baada ya competitors kuanzisha VOD zao hivyo kuzinyofoa Netflix..., mteja aki-subscribe anataka as much content as possible under one roof..., sasa hapo utakuta competition inakubania content zao

Dunia ishakuwa kijiji ndio maana ni vigumu kuna na Youtube ya Bongo per see sababu kule Youtube kuna content zaidi

Anyway all the best
 
Back
Top Bottom