Katika hali ya kushangaza mambo yanayoendelea nchini Congo DRC, chini ya rais Joseph Kabila ni kulichezea Kanisa Katoliki na bila kujua ni kwa namna gani linaweza kumuweka au kumwondoa mtu yeyote kwenye utawala.
Ni juzi kati nchi ya Congo DRC ilipatwa msibwa mkubwa wa kiongozi mkuu wa upinzani bwana ETIEN CHISEKEDI huyu alikuwa kinara na mtu mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za upinzani na kitaifa nchini DRC.
Kabla ya kifo cha bwana CHISEKED mgogoro wa kisiasa juu ya mhula wa tatu wa rais ambao ni kinyume na katiba ya nchi, mgogoro huu ulikuwa unatafutiwa ufumbuzi wa kusiasa kwa njia ya amani kwa msaada wa kimataifa chini ya uratibu wa KANISA KATOLIKI. Kufuatia Kanisa Katoliki kuwa mstari katika masuala kupatanisha migogoro ya kisiasa duniani chini ya kamati yake HAKI NA AMANI huwa halina upendeleo na mara nyingi limeonekana kuwa mwiba kwa viongozi wasiopenda Demokrasia duniani.
Rais Joseph Kabila ni miongoni mwa marais wenye utata barani Africa. Kitendo cha rais kabila kukataa kufanyika uchaguzi baada ya mhura wake wa pili ambao alitakiwa aachie madaraka. Kanisa katoliki halikupepesa macho katika kukemea hulka ya rais Joseph Kabila kutaka kukanyaga katiba ya nchi. Kufuatia msimamo KANISA KATOLIKI kuonekana kumpinga waziwazi rais J. Kabila sasa naona kaamua kuliandama Kanisa Katoliki kwa kutumia vyombo vya dola hasa jeshi anasahau nguvu ya Kanisa Katoliki ambazo huwa linaushawishi mkubwa wa mataifa yote yenye nguvu duniani kama MAREKANI, UJERUMANI, UFARANSA, ITALIA na URUSI. Hapa unaweza kuona jinsi kanisa lilivyo na nguvu ata kuwaleta maadui pamoja linapokuja suala la kumuandama adui wake kitendo cha rais J.Kabila kufanya dhuluma kwa Kanisa Katoliki kitamtokea puani.
Hizi ni picha za baadhi ya matendo ya dhuluma kwa Kanisa Katoliki huko nchini Congo DRC...
View attachment 473980View attachment 473982View attachment 473983
Kwa Kanisa Katoliki kuchezea YESU WA EKARISTIA ni udhalilishaji wa kiwango cha juu mno. Hakika maombi, sala na dua zitakazopigwa kuunganisha na rasimali ya akili (elimu) na mali (baraka za mikono ifanyayo kazi) zitatumika mpaka huyu kiongozi dhalimu aliyekosa heshima hadi kwa Mungu.
Dunia inatakiwa kumpinga J.Kabila na vibaraka wake na pia viongozi wengine wa kariba yake wanaoibuka hasa katika Afrika. Tukiendelea na upuuzi huu tutakuwa na akina NKRUNZINZA kibao, mifano ni mingi sana, Rwanda, Uganda, Zimbabwe, Gambia tumeshuhudia, hii tabia inaendelea kuota mizizi.
AMERIPOTI RAIA MMOJA WA CONGO
Eklesia is going through pesecutions and humiliation.I Democratic Republic of Congo after the death of one prominent Opposition Leader the Government Troops went and demolish the Catholic Church in which he was congregating because they feel the Church is opposing Kabila's third term bid. Below are some of the scene photos. It's sad for our Church. We need to pray for them and our Church