Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,096
- 5,592
Wakuu,
Akiwa anazungumza leo, John Mrema amesema kuwa CHADEMA imeua ndoto za wanachama wengi waliotaka kugombea kwenye Uchaguzi ba kuongeza kuwa hana uhakika kuwa kama chama hicho kitakuwepo hadi kufikia mwaka 2030
"Jambo la pili ni chama chetu kutosaini kanuni za maadili ya uchaguzi na kukifanya sasa chama chetu kujiondoa rasmi kwenye uchaguzi. Jambo hili limeua ndoto za wanachama wa CHADEMA, wapo watu wapo CHADEMA kwasababu wanawiwa kuwa madiwani wawawakilishe wananchi kwenye kata zao, wapo akina mama wanawiwa kuwa madiwani wa viti maalumu wakakiwakilishe chama na wananchi wao kwenye kata zao, kina mama hawa ndoto zao zimekufa.
"Wapo watu wanataka kuwa wabunge, kwa kutosaini kanuni, ndoto za watu hawa zimekufa mpaka mwaka 2030, hatuna uhakika kama tutakuwepo , CHADEMA itakuwepo ama laa..lakini tunawasikia viongozi wetu wakisema bora chama kife, nimemsikia Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA bara John Heche."
"Wanafika mahali wanajaribu kuonesha kwamba bado kuna mlango wa kimiujiza unaweza kufunguka, tumemsikia mwanasheria mkuu wa chama akisema kuwa wanaweza bado kwenda kushiriki uchaguzi, kanuni kifungu cha 1.5 kinasema wazi chama kisichosaini maadili hakitakuwa na haki ya kushiriki uchaguzi, kanuni zimeshachapishwa kwenye gazeti la serikali, sasa ni rasmi kwamba CHADEMA haitashiriki uchaguzi mkuu wa 2025"
"Watu hawa waliokuwa na ndoto za muda mrefu na wengine wamekitumikia chama hiki kwa miaka mingi, ndoto zao zimeuawa kwasababu tu ya kiburi cha viongozi wetu"