RWANDES
JF-Expert Member
- Jun 12, 2019
- 1,736
- 4,298
Nakumbuka tukio la utekaji wa mzee Ally Kibao, ambapo mtu wa kwanza kutoa taarifa kwa umma kuhusu tukio hilo alikuwa John Mnyika, kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Hatimaye, mzee Ally Kibao alikutwa ameuawa na watekaji.
Aidha, tukio jingine lililotikisa ni lile la Abdul Nondo, kiongozi wa Ngome ya Vijana wa ACT-Wazalendo. Katika tukio hilo, John Mnyika pia alikuwa wa kwanza kutoa taarifa za utekaji huo kwa umma.
Hata hivyo, pamoja na mfululizo wa matukio haya yanayohusisha taarifa muhimu kutoka kwa Mnyika, jeshi la polisi limeonekana kuwa na uzito kufanya mahojiano naye kuhusu vyanzo vya taarifa hizo.
Kinachoonekana ni kwamba Mnyika ana mtandao wa watu makini wanaompa taarifa za kweli na za haraka. Swali linabaki: nini hasa kinachokwamisha jeshi la polisi kumhoji?