Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,497
- 7,042
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vikali kile ilichokiita kukamatwa kwa Mwenyekiti wake Taifa, Tundu Lissu, kikieleza kuwa hatua hiyo ni matumizi makubwa ya nguvu na inalenga kuzuia harakati za kudai mageuzi ya kisiasa kupitia kampeni ya No Reforms No Election.
Akizungumza na wanahabari mjini Songea, mkoani Ruvuma, Aprili 10, 2025, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, amesema kuwa chama hicho tayari kimelifikisha suala hilo kwa mawakili wake wa ndani na nje ya nchi na kinatarajia kuchukua hatua za kitaifa na kimataifa.
“Mawakili wetu ndani na nje ya nchi, akiwemo Robert Amsterdam ambaye atashughulikia kimataifa, ameshapata taarifa kamili ya kwamba Mwenyekiti wetu amekamatwa, na yeye ataanza kufanya kazi kimataifa,” amesema Heche.
Heche ameeleza kuwa ndani ya nchi, wakili maarufu Peter Kibatala pamoja na Deogratius Mahinyila na timu ya mawakili waliopo Dar es Salaam wanafuatilia kwa karibu suala hilo kwa mujibu wa sheria.
CHADEMA imeeleza kuwa kukamatwa kwa Lissu kunakwenda kinyume na misingi ya haki na kwamba kiongozi huyo alipaswa kuitwa na kujiwasilisha mwenyewe kwa Jeshi la Polisi badala ya nguvu kutumika.