Joe Biden ajichanganya, asema anajivunia kuwa mwanamke mweusi

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,274
3,562
Joe Bide mwenye umri wa miaka 81, alijikanyaga wakati wa mahojiano jana 4/7/2024 Alhamisi na WURD ya Philadelphia, akionekana kujichanganya na Makamu wake Kamala Harris.

'.... hata hivyo, ninajivunia kuwa, kama nilivyosema, makamu wa kwanza wa rais, mwanamke wa kwanza mweusi ... kuhudumu na rais mweusi. Ninajivunia kuhusika na mwanamke wa kwanza mweusi kwenye Mahakama ya Juu. Kuna mengi sana ambayo tunaweza kufanya kwa sababu, tazama ... sisi ni Marekani.'




Biden alionekana kuangazia uteuzi wake wa Kamala Harris kama Makamu wa Rais wa kwanza mwanamke mweusi wa Marekani.

Kwa kuchanganya, yeye mwenyewe hapo awali alikuwa Makamu wa Rais, ambayo inaelekea ni kile alichokuwa akirejelea katika 'kuhudumu na Rais Mweusi.'

Ikumbukwe jaji wa kwanza wa kwanza wa kike mweusi, aliteuliwa kwa mara ya kwanza Biden mwaka 2022.

Kumekuwa na maoni kadhaa yakimtaka bideni ajitoe kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Urais kwa ungwe ya pili, huku michango ya kwaajili ya kampeni yake ikitazamiwa kushuka wengi wakiongelea suala la umri ambao unaonekana kumtumpa mkono kutokana na matukio mfululizo ya kusahau baadhi ya taarifa kuendelea kutokea.

===

Pia soma:
Rais wa Marekani Joe Biden aanguka jukwaani
 
Huyu Mzee mwishowe ataiangukia Button ya ku launch Nuclear na kuiangamiza Dunia.

Apumzike tu amuachie Kamala Harris.

be5dcf78-27d9-474d-95bd-dc04a5df9f57-medium3x4_AP23152689144818.jpg
biden-stumble-03-ht-jt-210319_1616181267869_hpMain_2_16x9_992.jpg
 
Biden alisha jifia zamani sana hilo mnalo liona ni roboti. Fuatilieni mtagundua kitu.
Wamarekani wenyewe wanaanza kukiri kwamba huyu mzee alishajichokea muda mrefu ila vyombo vya habari vikaficha, vikasadia kuficha madhaifu yake.

Sasa mambo hadharani, hata cnn, msnbc na legacy media zote ambao ndio washirika wake wakubwa wamemgeuka, wanasema apumzike.

Biden mwenyewe anakiri kwamba kuna muda ni mzima na kuna mda sio mzima kiakili.

Wanaotaka aendelee ni wale wanaofaidika nae, ambao ndio wanaiongoza Marekani kwa mgongo wa nyuma kwa sababu Biden hakuna kitu anafanya, wanamfanyia na kumpa asaini tu kama mhuri.

Trump anajipigia Biden anavyotaka.
 
Back
Top Bottom