Job Ndugai Na Madiwani wa Kongwa Aibukia Jijini Tanga Kujifunza Namna ya Utekelezaji Wa Miradi ya Maendeleo.Apokekelewa Na Ummy Mwalimu.

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
25,485
18,914
Ndugu zangu Watanzania,

Speaker Wa Bunge Mstaafu Mheshimiwa Job Ndugai Ameibukia Jiji La Tanga akiwa Ameongozana na Madiwani Mbalimbali kutoka halmashauri ya Wilaya ya Kongwa .

Ambapo yeye pamoja na Waheshimiwa Madiwani ,mkuu wa wilaya na mstahiki meya wa halmashauri ya Kongwa wamefika jijini Tanga katika lengo la kujifunza namna ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Ambapo Mheshimiwa Job Ndugai na waheshimiwa Madiwani wameweza kupokelewa na Mheshimiwa Ummy Mwalimu Waziri Mstaafu wa Afya na TAMISEMI na Aliyehudumu kwa Muda mrefu katika Baraza la Mawaziri kwa Moyo wa Uzalendo,Upendo,kujitoa na kujitolea na Uchapakazi uliotukuka Mpaka pale Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan alipoamua kumpumzisha kwa kuteua mtu Mwingine jambo ambalo ni la kawaida katika uongozi.

kwa sababu cheo ni Dhamana na pia siyo Ajabu pia siku moja pia akaweza kumrejesha tena ndani ya Baraza lake la Mawaziri katika wizara mojawapo kama tulivyoona kwa Mheshimiwa profesa palamagamba Kabudi pamoja na Mheshimiwa William Lukuvi ambao walitolewa na kurejeshwa tena Baadaye.

Au kama ambavyo tuliona pia Mheshimiwa Dkt Mwigulu Lameck Nchemba au waweza kumwita Mr Clean alivyotolewaga kwenye Baraza la Mawaziri na kurejeshwa tena wakati wa utawala wa Hayati Mwalimu Daktari John Pombe Joseph Magufuli ,Kama ilivyokuwa pia kwa Mheshimiwa George Simbachawene. Kwa hiyo hata Mheshimiwa Ummy Mwalimu naye anaweza kurejeshwa Barazani na Mheshimiwa Rais wetu kipenzi Sana na anayependwa na watanzania wa makundi yote kutokana na uchapakazi wake uliotukuka ambao umekuwa gumzo Duniani Kwote mpaka kufikia hatua ya kualikwa katika Mkutano wa G20. lakini pia kuongoza kikao cha nishati safi ya kupikia Nchini Ufaransa kama Mwenyekiti Mwenza.

Lakini pia katika mapokezi hayo Pia Alikuwepo Mstahiki Meya wa jiji la Tanga ambaye pia aliambatana kwa Pamoja na Msomi huyu wa sheria Mheshimiwa Ummy Mwalimu. ambaye Licha ya kuondolewa katika Uwaziri lakini bila kuchoka wala kupoa wala kutulia wala kusita Ameendelea kuchapa kazi kuwatumikia wana Tanga,kumsemea Kwa nguvu zake zote na kwa Upendo mkubwa Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan juu ya Mambo makubwa aliyoyafanya kwa wana Tanga pamoja na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM
Screenshot_20241215-160842_1.jpg
Screenshot_20241215-160900_1.jpg
Screenshot_20241215-160851_1.jpg
Screenshot_20241215-160833_1.jpg


Kazi iendelee , Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Back
Top Bottom