The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 746
- 2,098
"Ahsante sana kwa kukumbusha watu kuwa nilizungumza kwa Kiswahili kule Umoja wa Afrika, na ile ilikuwa tu kuwakumbusha watu kwamba Kiswahili ilikuwa ni lugha rasmi ya Umoja wa Afrika kipindi kile na watu wakaamini kuwa nilikuwa nafahamu Kiswahili vizuri. Lakini si kweli kwamba nafahamu Kiswahili kwa kiasi hicho, na kwahiyo siwezi kutoa hotuba yangu kwa Kiswahili. Niruhusu nizungumze Kiingereza."
Rais Mstaafu wa Msumbiji Joaquim Chissano amezungumza hayo leo Julai 14, 2022 katika Kongamano la Pili la kumuenzi aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa.
Kwa miaka mingi imekuwa ikiaminika kuwa Chissano anazungumza vizuri Kiswahili. Na watu wengi wanaounga mkono mafanikio ya Kiswahili wamekuwa wakitoa mfano wa Chissano na hotuba yake ya mwaka 2004 ambayo, kwa mujibu wake leo, si kama ambavyo tumekuwa tukiamini.
Kwa kumbukumbu: Julai 6, 2004, Mzee Joaquim Chissano ambaye wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), aliamua kutumia lugha ya Kiswahili kutoa hotuba yake muhimu ya kuaga kiti akimuachia kijiti cha uenyekiti Rais wa Nigeria wa wakati huo, Olusegun Obasanjo.
Joaquim Alberto Chissano ni mwanasiasa ambaye alikuwa Rais wa pili wa Msumbiji, kuanzia 1986 hadi 2005. Anasifiwa kwa kuibadilisha Msumbiji iliyokumbwa na vita kuwa mojawapo ya nchi za Afrika zenye demokrasia yenye mafanikio makubwa.