JKCI kushirikiana na Hospitali ya Medanta kuwanoa wataalamu wa magonjwa ya moyo na kutoa huduma za kibingwa

informer 06

Member
May 11, 2024
47
26
Katika jitihada za kukuza mashirikiano yenye tija, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) imeanza kushirikiana na Hospitali ya Medanta iliyopo nchini India katika kubadilishana ujuzi wa fani mbalimbali za kutoa huduma za matibabu ya moyo.

fa7c7b3c-8e82-425e-adc9-184a9e994c46.jpeg

Ushirikiano huo meanza rasmi kwa mara ya kwanza September 23, 2024 baada ya daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali ya Medanta kufika JKCI.

Baada ya Daktari huyo Bingwa kufika alishirikiana wenyeji kuanza kutoa huduma za upasuaji wa tundu dogo kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.

Akizungumza September 24, 2024 kufuatia ujio huo, Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.Tatizo Wane alisema ujio wa daktari huyo umedhamiria kufanikisha masuala mbalimbali ikiwemo kuwajengea uwezo wataalamu wa JKCIna kushirikiana kwa pamoja kubadilishana ujuzi kwa kuwafanyia upasuaji wa tundu dogo wagonjwa kadhaa.

"Dkt. Chandra amefika jana na kushirikiana nasi kutoa huduma za upasuaji wa tundu dogo kwa wagonjwa wawili na leo ataendelea nasi kuwafanyia upasuaji wa tundu dogo wagonjwa wengine watatu", alisema Dkt. Waane

IMG_6382.jpeg

Pia Dkt. Waane alisema Medanta ni moja ya Hospitali kubwa zinazotoa matibabu ya moyo kwa utaalamumkubwa na sasa imeanza kushirikiana na JKCI katika kutoa huduma mbalimbali bingwa bobezi za moyo katika upasuaji wa moyo pamoja na kuonesha nia ya kupokea wataalamu kutoka JKCI kwenda kuongeza ujuzi ambao utasaidia kuboresha zaidi huduma.

Aidha Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali ya Medanta iliyopo chini India Preveen Chandra amesema amekuwa akifanya upasuaji wa tundu dogo kwa utaalamu wa juu hivyo amedai kuwa ameona vyema kwa sasa kukutana na wataalamu wenzake kutoka hospitali ya JKCI kushiriki upasuaji na kubadilishana ujuzi na wataalamu waliopo katika hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya mashirikiano.

IMG_6378.jpeg

"Wagonjwa tunaowatibu India wanatoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Afrika, wagonjwa hawa tumekuwa tukiwatibu kwa kutumia utaalamu mpya kila tunapopata ujuzi mpya kama vile upasuaji wa Tavi wa kubadilisha valvu ya mshipa mkubwa wa damu bila ya kufungua kifua (Transcatheter Aortic Valve Implantation procedure - TAVI)", alisema Dkt.
Chandra

Kufuatia kushiriki kufanya upasuaji na wataalamu wa JKCI, ametoa pongezi kwa uwekezaji wa vifaa tiba vya kisasa vinavyotumika kutoa huduma za upasuaji wa moyo, jambo ambalo amesisitiza kuwa ni muhimu katika kufanikisha huduma za upasuaji.

Itakumbukwa kwa siku za hivi karibuni JKCI imekuwa ikiweka bayana kuwa inashirikiana na wadau mbalimbali katika kusogeza karibu huduma za magonjwa ya moyo, jambo ambalo kupitia Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dkt.Peter Kisenge amekuwa akinukuliwa kuwa tija ya mashirikiano hayo pamoja na uwekezaji unaoendelea kufanyika kwenye hospitali hiyo umeokoa mamilioni ya fedha ambayo yangetumika haswa kwa wagonjwa kusafiri kwenye nje ya Nchi kwa ajili ya huduma za kibingwa, pamoja na wataalamu wa ndani kusafiri kwenda nje kupata ujuzi.
 
Magonjwq yas8yoambukiza kama sukari yanatesa na kuuwa watu kimnya kimnya, hivi wataalamu hawajapata ufumbuzi wa kutibu kisukari na kikaisha kabisa? Watu wanateseka sana, unakuta mtu anaishi duniani wakati huwohuwo anauraia wa mbinguni, mtu anakatazwa asile kila kitu, mbona ni shida na nusu!
 
Back
Top Bottom