Jinsi ya kutumia feature mpya ya Nearby Share kwenye Android phones

racka98

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
1,041
1,538
Mnamo tarehe 4 August 2020, Google walizindua feature yao ya kushare mafile kati ya Android phones iitwayo Nearby Share ambayo ni kama Xender app na Airdrop ya iPhones. Nearby Share inafanana ufanyaji kazi wake kama airdrop ya kwenye iPhones kwamba unapata menu ya kushare kutumia njia directly utakapo bonyeza share button na ni kitu ambacho kipo tayari kwenye simu na haihitaji wewe ku download app nyingine yoyote. Feature hii ilikuja kupitia Google Play Services update hivyo haikuhitaji wewe kufanya update manually kwani tayari imeshakua installed.

Asimlimia kubwa ya watu hawajui kama simu zao zimepata hii feature hivyo leo nitawaelekeza jinsi ya kuitumia.
Cha muhimu ni kwamba simu yako ni lazima iwe na Android 6.0 (Marshmallow) kwenda juu ili kuwa na hii feature.

Step 1: Ingia settings kisha tafuta option ya Google na uingie hapo.
Screenshot_20210210-211836.png


Step 2: Scroll mpaka utakapo ona Devices connection na uingie hapo. Utaona Nearby share humo ndani nayo ibonyeze
Screenshot_20210210-211854.png


Screenshot_20210210-211913.png



Step 3: Ukishaingia hapo utaiwasha. Hapa inaweza ikaanza kukuuliza kuchagua Google Account utakayotumia. Fata maelekezo kama inavyokuuleza. Ukimaliza hapo utatakiwa kuchagua jina utakalo tumia kutambulisha simu yako na utabadilisha "Device Visibility" kuwa All contacts na utabadilisha option ya mwisho kuwa "Without internet" ili isije ikajaribu kutumia Data na kuhakikisha itatumia WiFi Direct & Hotspot ambayo ni fast zaidi.

Screenshot_20210210-211925.png


Step 4: Hapa utatiwa kuongeza icon kwenye Notification panel quick settings. Hivi ni vile vi icon unavyoona ukiswipe mara mbili kutoka juu ya simu, ndipo unapokuta icon za kuzima/kuwasha data, wifi, bt, nk. Mara nyingi ukiwasha Nearby share icon yake itajiweka yenyewe, ikitokea haija tokea fata maelekezo haya.

Fungua panel ya notification kisha swipe tena mara pili. Utaona icon kama ya kipeni hivi au maneno yaliondikwa "Edit", bofya hyo kisha scroll mpaka chini utaiona hyo icon ya Nearby share, bonyeza shikilia na uibebe uipandishe juu. Ukiikuta tayari ipo kwenye Notification quick panel settngs basi hii step haina umuhimu kwako

Screenshot_20210210-213504.png


Screenshot_20210210-213449.png




Tuje kwenye jinsi ya kuitumia sasa.
1. Nenda kwenye kitu unachotaka kushare (kama ni picha au video au document) kisha bonyeza icon ya kushare.
Screenshot_20210210-223601.png


2. Zikitokea zile option nyingi za kuchagua app bonyeza Nearby share
Screenshot_20210210-214340.jpg


3. Itakuja menu ya kuchagua ni simu unataka kuitumia. Hapa kuna notification itakuja kwenye simu iliyo karibu inayotaka kupokea file hilo ambayo unatakiwa kuibonyeza. Kma hii notification isipotokea unaweza kubonyeza ile icon ya nearby share tuliyoiongeza kule juu.

Reciever's phone:
Screenshot_20210210-214353.png

Screenshot_20210210-224215.png



Sender's phone:
Screenshot_20210210-214541.png



4. Hapa kwenye simu inayotuma utachagua jina la hyo simu na simu inayopokea itapata ujumbe ambapo unatakiwa kubonyeza Accept. Ita connect na file lako litatumwa vizuri kabisa.
Screenshot_20210210-214453.png

Screenshot_20210210-214556.png


File likishaingia unaweza lifugua kwa kuchagua app ya kufungulia. Ma file yote yanayotumwa kwa njia hii unayakuta kwenye folder la Downloads.

Hapo nimefikia mwisho, enjoy kutuma ma file bila maswala ya kuwa na xender na kuanza ku scan ma QR code yanayozingua ku connect sometimes.

Ijue simu yako, Ahsante!!
 
Asante kwa elimu nzuri kiongozi. Naomba unipe tofauti kati ya bluetooth na hiyo nearby share. Ni njia ipi rahisi na ya haraka kwenye kutuma mafaili?. Kuna moja iko limited?
 
Wakuu huwa napata shida kuhamisha movie niliyodownload kwenye phone kupeleka kwenye Pc sasa hii njia ya wireless naweza fanya hivyo au tu niendelee tumia waya maana bluetoos iko slow?
 
Back
Top Bottom