Jinsi ya kutongoza mwanamke msiyejuana (Barabarani, kwenye daladala au popote)

Mcqueenen

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
6,837
11,685
Wakuu vipi?
Baada ya kusoma Points za huyu jamaa hapa

Na baada ya kuona Malalamiko kama haya


Nimeona namimi nidondoshe hapa baadhi ya visarafu vichache nilivyoviokota katika maisha yangu ya kutongoza.

Muhtasari
Kumpata mwanamke kuna hatua nyingi ambazo inabidi ziende kwa mtiririko (hakuna kuruka).

1.Approach (Kumtokea)
2.Intrigue (kumfanya kuwa intrested nawewe hasahasa KIMAPENZI, ili aendelee kukusikiliza)
2.Rapport (Kumfanya aendelee kukusikiliza na kukuambia mambo yake/Kuwasiliana nawewe ili kujuana zaidi)
3.Attract (Kumvutia sasa ili awe wako kupitia hiyo raport hapo juu)
4.Capture/Enslave (Kumteka akili awe chini yako)

Namba 1-3 zinahausu kumpata mwanamke ila kama unataka kum'keep inabidi uende mpaka namba 4.

Kwahyo kama unataka kupiga na kusepa unaishia namba 3

Content
Sasa kwasababu ya muda mimi leo nataka niongelee namba 1 tu, Approach.

Hapa naongelea kuapproach pale unakutana na dem katika mazingira yoyote yale, iwe Hotelini, Barabarani, Club,Washroom popote pale.

kwa miaka mingi nilikuwa mhanga sana wa kufeli hapa, ila kwasababu ya "Ego" niliishia kuwalaumu wao bila kujitafakari mimi 'mademu washamba', 'wanaringa', 'Malaya tu' etc. Etc. Ndiyo nilisema hayo. Sikujua kuwa tatizo ni mimi mwenyewe.

Hii mbinu yenyewe ni somo kubwa ila nataka nigusie gusie tu sehemu za muhimu kwa kifupi ili tusichoshane.

Ukimuapproach Mwanamke anaangalia hivi vitu vikuu vitatu
1.Mwonekano
2.Maneno unayosema
3.Body Language

1.Mwonekano.
Hapa siongelei mwonekano wa hela, magari, (hapa siongelei jinsi ya kuapproach malaya au mdangaji, naongelea hawa wanawake wa kawaida wa mtaani ambao ndio wake zetu wa baadae).Mwonekano ni Usafi, Nywele, Mavazi, Viatu (Nimeitofautisha na mavazi maana wengi wanafeli hapa, unakuta miguu imepauka umevaa ndala) Kinywa, nk. Nk.

Hapa sitaongea sana maana wakubwa washaelewa hapa haihitaji maelezo mengi labda kama unasoma hili bandiko huku unajianda na mitihani ya darasa la 7. Ila imebidi niiseme tu hii point maana wengi tunafeli apo pia.

2.Maneno unayosema.
Watu wengi wanajuaga kwamba hii ndio sehemu ya muhimu kuliko zote kwenye approach. Nakuapia, hata huyo dogo hapo juu aliyekuwa anaomba ushauri wa kutongoza alitaka mmpe maneno gani akiyatumia atawanasa warembo.

Kiuhalisia, hapa hii sehemu haimati sana, hakuna maneno special ya kutongozea inategemea na muktadha na mazingira (It doesnt matter what you say, it's how you say it). Maneno yanaweza kuwa ya kawaida tu au kama wabongo wengi wanavojifanya yakawa yakikomedi. It doesnt matter.

Cha muhimu kwenye maneno ni kuhakikisha katika sentesi zako UNAMSIFIA kidogo (usizidishe sasa) ila usimsifie kinafiki, kiwaziwazi, kijinga/pasipo heshima, jaribu kumsifia indirectly. Siyo unakutana na mwanamke hamjuani kabla hata hujabuild rapport unaanza kusema ana mapaja mazuri unatamani ukamgegede.

Ni vizuri ukawa Subtle, yani chini kwa chini yani unamsifia bila yeye kujua umemsifia. Unaweza pia (sio lazima) ukampa maudhui za kukinzana yani kama unampondea kama unamsifia. Mfano wa kutunga: Mmeshasalimiana na kadhalika afu umejifanya kama unamuulizia Saluni ya Mama kimbo ilipo, akasema haijui wewe ukasema "Nimecheki nywele zako zilivyo nzuri nkajua utakuwa unashinda saluni za kijanja, Kumbe nawewe haujui kitu".

Cha muhimu kwenye maneno usitumie maneno ya ukali, ya king'ang'anizi, direct sana. Tumia maneno ya kipole, ya heshima, kulingana na muktadha. Lakini pia usiache kusema azimio lako. Usiishie kupiga story kama unavyoongea na dada yako, inabidi umchombeze mahaba kumuonesha dhumuni lako (Ukifeli hapa, hata akikupa namba atakuwa anakupa kama braza tu na kumpata itakuwa mlima mkubwa sana kwako).

Unatakiwa ujue ndani ya sekundd 20 mwanamke atakuwa ameshakuweka kundi gani (potential mchumba, fala fulani, danga au brother material). Ni heri ukamuonesha dhumuni mapema akakutolea nje (fungu la kukosa) kuliko kuficha dhumuni akakuzungusha miezi 6 akakupiga pesa na bado akakutolea nje.

3.Body Language
Huko juu nilisema mwenyewe nilikuwa mhanga wa kuapproach, baada ya kukaa kujitafakari nafeli wapi nikagundua hii siri na ndiyo kiini cha hii mada. Wakuu maneno hayamati sana kuliko Body language. Kutongoza ni sayansi inabidi uielewe, unapomtokea mwanamke usilenge sana physical interaction ya conscious things kama maneno na hela.

Wewe dili sana na Subconscious things ambazo ndio huwa zinawateka wanawake. Vitu subconscious vinavyowateka cha kwanza ni muonekano wako (nishaongelea hapo juu) cha pili ni body language. Hapa kwenye body language dili na hivi vitu;

a) Confidence - Usiwe muoga maana hawa viumbe wana akili za haya mambo kuliko sisi, Yani ukiogopa wanasense sana huyu jamaa anatetemeka au ananiogopa..Pambana sana kuondoa uoga, meditate, practice sana, do whatever ila ondoa uoga
Na body yako iweke position ambayo itaonekana una ujasiri kama hizi picha zinavyoonesha

images-2.jpeg images-3.jpeg
b) Be calm - Hapa sasa inabidi ujaribu kuonesha kwa body yako kuwa uko calm na hili tukio(la kumtokea) ni la kawaida tu, mfano kama una chupa ya maji unaweza ukawa unashushia kabisa (kwasababu viumbe wote wanaweza kuwa na hasira lakini muda wa kula (kama chakula sio cha kupigania) lazima wapoe..na misuli yote irelax.

c) Smile - Hii ni muhimu sana, na hapa ndo mwenyewe ilikuaga nafeli, Yani unakuta unaongea na demu upo siriaz kama unaongea na baba mchungaji...Hata kama una maneno mazuri kiaje ila kama unayasema na body language mbaya huwezi kufua dafu. Never underestimate the power of a good smile...Lakini pia smile mahala husika, Sio kufosi smile (madem wanajua fake smile) Fake smile mdomo tu ndio utasmile ila macho yatabaki kuwa makavu.

d) Patience - Hapa usioneshe sign yoyote ya desperation, yani haraka fulani (mfano haraka ya kupata namba), Hapa jaribu kuonesha kuwa huna shida saana na hata akizingua wewe unasepa haina shida, Hii inaendana na kurelax lakini zinapishana kidogo kimantiki, usichanganye..Unaweza ukawa umerelax ila unang'ang'aniza kitu fulani. Patience is key bro.

e) Eye contact - Nilisubiria E for eye contact😅...Hii wakuu ni muhimu, ila usifanye sasa kama mashindano yani wewe huangalii pengine (utamuogopesha), make sure unamuangalia machoni maana communication ya kwanza kati ya binadamu wawili huanzia machoni na sio mdomoni au sikioni.

F) Kujifix -Hii naongelea aina yoyote ya marekebisho kama kurekebisha nywele, kufunga kifungo cha shati, kuchomekea, kujifuta na leso, kupandisha suruali, kulamba lips, kukohoa, n.k. Hizi siyo kwamba usifanye lakini kama imetokea fanya mbele yake siyo kusubiria amegeuka wewe ndiyo unapandisha suruali fasta (wako makini sana), Lakini pia usifanye too much sasa, Kama haikulazimu Unaweza kujirekebisha mara 1 tu katika maongezi yote (Sio kila dakika unalamba lips, kuchomekea na kupandisha suruali).

g) Uchangamfu - Usiwe mnyonge kama umenyeshewa mvua, usitie huruma, kuwa charismatic kama vile huyo dem ushamzoea na mnajuana tokea kitambo.

h) Touch - Ukipata chance touch her, kwa baadhi ya wanawake Touch is more powerfull than all words you can say.

Conclusion
: Usizidishe sana maongezi hata kama ametiki (enzi zile, kuna kipindi niliapproach mwanamke pale Kimara darajani akatiki nikaanza mpaka kumsindikiza kununua samaki napiga naye stori😂). Always muoneshe kuwa upo interested na yeye lakini pia na wewe una mambo yako yanayokukeep busy. Be neutral, Be cool, kila kitu fanya kwa wastani.

Na mwisho kabisa akili gumkichwa, za kuambiwa changanya na zako😅.

Okay, One last thing, hizo mbinu zote ni kwaajili ya approach tu ya kujitambulisha kwake na kupata namba, au kama ni bar ni ile kumtokea na kumvuta ili ukae naye.

Ukishapita huo mtihani wa stage 1 sasa inabidi ujue namna ya kumfanya akuone upo interesting na aendelee kukusikiliza ili mtengeneze Rapport, kama ni bar umeshamleta sasa kwenye meza yako..ili aendelee kukusikiliza inabidi utumie tena mbinu zingine na ili kumuattract KIMAPENZI(Ngono) kuna mbinu zake na ili umteke akupende kabisa (true love) kuna mbinu zake.

But kwa leo tuishie hapo, hope itawasaidia vijana wadogo wanaoanza hii sana. Kwa maneno ya humu 'Tuzichakate, zipo nyingi, tusitegeane hata kidogo'.

Goodluck & Godspeed.
 
Nmeishia hapo kwenye kumsifia😁
Mkuu amini kwamba Dem yeyote anapenda sifa hata kama umeshamuoa...Usichoke kumsifia mwanamke wako mkuu..

Kuna ule uzi unahusiana na watu wanaofeli vitu vidogo kama hivi huuhapa.
 
Back
Top Bottom