Jinsi ya kutoboa kupitia biashara ya mazao (nafaka)

ngara23

JF-Expert Member
Aug 31, 2019
7,113
16,992
Nitaelezea zaidi Kanda ya ziwa, hasa mkoa wa Kagera

Biashara ya mazao hasa nafaka ni biashara ambaya haimtupi mtu, yaani hapa faida inayoweza kuji double ni uhakika

Usichukue mtaji ukawekeza kulima kama kijana unayejitafuta maana kilimo kina risky zake Kwa sisi Africa tunaotegemea mvua ya Mungu pekee bila teknolojia za umwagiliaji, hapa mvua zinaweza kuonyesha nyingi zikaharibu mazao au kiangazi kikazidi,
Subiri walime, we andaa mtaji kama million 5 zungusha mara 3 hadi 5 msimu uje kuisha una si chini ya million 15

Kwasasa ndo tunavuna maharage,
Gunia ya maharage ya njano, ambayo ndo maarufu yanapendwa Kwa Sasa ni sh 300,000 gunia Lina kg kuanzia kg 250 ukifika mjini Gunia hilo utauza si chini ya 750k

Kwa wale matajiri ukiingia na pesa yako vijijini ni rahisi sana kutajirika, unanunua mazao na kupeleka Kwa wavivu Kenya tena unauzia Sirari border au Namanga unarudi na pesa

Au unapeleka Burundi, Rwanda na Uganda

Msimu wa mahindi unaingia January, Wakenya washapenyeza pesa, Kuna pesa za uhakika

Kwa wale wasukuma Kwa maana ya Geita, Mwanza, Simiyu na Shinyanga, mpunga umekubali hatari na utaiva mwezi wa 5

Humu kwenye mpunga Kuna mkwanja kama ulilima au unanunua, Japo Watanzania tumelala wanakuja wakenya kuulangau wote na pesa inapita Kwa wakulima na Bado mpunga upo shambani

Hapa sijaandika mikoa mingine ya ufuta, uwele, mtama n.k ila kimsingi pesa ipo kwenye kilimo na mazao

Kwa vijana mlioko mjini, tafuta mtaji mapema, wekeza kwenye biashara ya mazao
 
Kwenye mpunga kuna hela ila wasiwasi wangu ni pale ambapo mtu ananunua mpunga afu anaenda kuweka kwenye godown au mashineni. Huwa sikaamini hawa watuzanji. Mwenye experience atufahamishe.
 
Wale watunzaji ni wamiliki wa mashine za kikoboa watakupa tu sehemu ya kuhifadhia kikubwa ukobolee pale mpunga wako basi
 
Thread imeisha chief? Ama hukujiandaa na hili andiko ? Una mawazo mazuri ila umeandika simpo simpo sana ,,,, nilitegemea uje na idea yenyewe, mtaji, mikoa halisia , masoko, pilika pilika za madalali, usafiri from Bush to town ,,,,,namna ya kutunza mazao Store nk
 
Usumbufu wa madalali haupo sana vijijini labda sokoni
Usafiri Kwa upo huo itategemea mzigo wako na wapi unapeleka
Kama una mzigo kidogo mfano gunia 10, mnaweza makajitafuta wananunuaji kadhaa mkakodi Lorry, hapa itategea umbali mara nyingi gharama za kukodo lorry hianzia laki 4 na kuendelea kutokana na umbali
Store, Kwa vijiji store ni gharama ndogo tu, kukusanya mzigo sio siku nyingi
 
Nitaelezea zaidi Kanda ya ziwa, hasa mkoa wa Kagera

Biashara ya mazao hasa nafaka ni biashara ambaya haimtupi mtu, yaani hapa faida inayoweza kuji double ni uhakika

Usichukue mtaji ukawekeza kulima kama kijana unayejitafuta maana kilimo kina risky zake Kwa sisi Africa tunaotegemea mvua ya Mungu pekee bila teknolojia za umwagiliaji, hapa mvua zinaweza kuonyesha nyingi zikaharibu mazao au kiangazi kikazidi,
Subiri walime, we andaa mtaji kama million 5 zungusha mara 3 hadi 5 msimu uje kuisha una si chini ya million 15

Kwasasa ndo tunavuna maharage,
Gunia ya maharage ya njano, ambayo ndo maarufu yanapendwa Kwa Sasa ni sh 300,000 gunia Lina kg kuanzia kg 250 ukifika mjini Gunia hilo utauza si chini ya 750k

Kwa wale matajiri ukiingia na pesa yako vijijini ni rahisi sana kutajirika, unanunua mazao na kupeleka Kwa wavivu Kenya tena unauzia Sirari border au Namanga unarudi na pesa

Au unapeleka Burundi, Rwanda na Uganda

Msimu wa mahindi unaingia January, Wakenya washapenyeza pesa, Kuna pesa za uhakika

Kwa wale wasukuma Kwa maana ya Geita, Mwanza, Simiyu na Shinyanga, mpunga umekubali hatari na utaiva mwezi wa 5

Humu kwenye mpunga Kuna mkwanja kama ulilima au unanunua, Japo Watanzania tumelala wanakuja wakenya kuulangau wote na pesa inapita Kwa wakulima na Bado mpunga upo shambani

Hapa sijaandika mikoa mingine ya ufuta, uwele, mtama n.k ila kimsingi pesa ipo kwenye kilimo na mazao

Kwa vijana mlioko mjini, tafuta mtaji mapema, wekeza kwenye biashara ya mazao
Shusha nondo mkuuu
 
Si rahisi Kama unavyoongelea Kuna changamoto nyingi Kama hujui zao husika mf mpunga Kama huujui ukamunua kichwa kichwa siku ukikoboa utaukimbia mzigo...kwa hio chagua biashara fanya research ya kutosha ununuzi na soko yaani mashambani na mashineni...Kama NI mpunga.,Kuna Sina na mbegu zinapendwa na zinauzwa Bei kubwa nyingine hazipeneki na no Bei mdogo...Kuna suala la kumix thailand na chenga ukpata FAIDA...utajishangaa mbona sipati FAIDA kumbe hujui namna biashara ifanywavyo...utamaliza zaidi ya misimu 3 Hadi 4 kuijua biashara ya mazao
 
Una hoja nzuri
Changamoto zipo kwenye fursa zote
 
Kwenye mpunga kuna hela ila wasiwasi wangu ni pale ambapo mtu ananunua mpunga afu anaenda kuweka kwenye godown au mashineni. Huwa sikaamini hawa watuzanji. Mwenye experience atufahamishe.
Kuna msukuma mmoja mjinga(msimamizi wa mashine) aliuza upunga wa Watu akapita na pesa kelele zika Baki Kwa mwenye mashine na mwenye mpunga. Tuwe makini wazee
 
Thread imeisha chief? Ama hukujiandaa na hili andiko ? Una mawazo mazuri ila umeandika simpo simpo sana ,,,, nilitegemea uje na idea yenyewe, mtaji, mikoa halisia , masoko, pilika pilika za madalali, usafiri from Bush to town ,,,,,namna ya kutunza mazao Store nk
Yaani wewe unataka utafuniwe, fanya na wewe research ya hayo Sasa yaani unataka kyuma ijilete kitandani uile.
Mwanaume you've to exert force ili Mambo yako yaende.
Mbona unazo energy za kufukuzia kuuuma hata miezi unasotea hata mwaka mwafrika anaisotea k anasubiria masharti.
Mwishowe utataka uletewe faida umekaa tu
 
Hivi hizi akili za vijana wa sikuhizi zina nini?

Unashauri vipi watu kuuza mazao halafu unawakataza kulima?

Bila hao wakulima kuna hiyo biashara?

Kwanini usishauri wakulima, walime halafu wawe wafanyabiashara wao wenyewe, wasafirishe wakauze huko Border kama wanavyofanya wenzetu China na Marekani?

Hii itaondoa hata uvivu wa hao madalali, nao wataingia kupiga jembe.

Uchumi si utakua katika nyanja zote?
 
Hatuwezi wote kulima
Mkulima anahitaji mnunuzi wa mazao
Wakulima tunahitaji wanunuzi wa mazao na sio madalali.

Tunauwezo kuungana na kwenda kuwauzia wa Kenya sisi wenyewe.

Au kama mkulima ana mtaji, dalali wa nini?

Ilitakiwa utushauri watu kufanya hiyo biashara ila usituzuie kulima.
 
Nani akasema dalali
Haijalishi umesema au hujasema, madalali wapo.

Wanunuzi wa mazao ni wachache sana, Watu wenye uwezo wa kusafirisha mazao Outside the country ni wachache.

Madalali wanaowatafutia mazao hawa wanunuzi ndiyo wametapakaa, na hua wanaachwa wapange bei zao za hovyo zinazowaumiza wakulima ili wapige faida.

Nililima viazi mwakajana walau tukasikilizwa kidogo, walikuja wanunuzi wakaingiza magari yao shambani toka Kenya kupitia kampuni ya [Tanzanice Agro] direct bila madalali, Hata umuhimu wa mkulima ukaonekana.

Wewe hujui tu, yawezekana sio mzoefu, Mfano kampuni zinazonunua parachichi hazizidi 20, Ila madalali wako zaidi ya Elfu10, Imesababisha wawe na nguvu ya kupanga bei zao wenyewe.

Bei za kwenye kampuni ni Constant kama ni 2,000/= per Kg wote hivyo hivyo ila madalali wanaanzia 1,500/=per Kg - na kila mtu ana bei yake. Je mkulima angepata access ya kuiuzia kampuni direct, mngekidharau kilimo like you said?

Msikataze kilimo, Muwe mnashauri kufanya hizo biashara bila kukataza kilimo, sababu ndiyo mzizi mkuu wa biashara zenu.

Nimemaliza.
 
Nakuelewa sana mkuu
Kwa mapachichi Sina uzoefu
Nina uzoefu Kwa nafaka
 
Back
Top Bottom