Kutunza taarifa za biashara ni eneo la muhimu kwa kila mfanyabiashara. Hii husaidia kujua mali ilyotoka, iliyoingia, mali zilizopo, madeni, mauzo na faida au hasara iliyopatikana.
Wengine hutunza taarifa zao kwa kutumia vitabu maalum na wengine hutumia digital tools kama computer au simu.
Binafsi napendelea zaidi mifumo ya kwenye computer kwasababu yenyewe hurahisisha kazi huku ikiongeza ufanisi. Inarahisisha kazi kwasababu ukishaingiza mauzo yako, yenyewe itakokotoa faida iliyopatikana na inatengeneza ripoti.
Lakini pia inakokotoa mzigo uliobaki dukani baada ya kuuza, ukikaribia kuisha inakupa taarifa mapema.
Inaweza kutoa mchanganuo wa mauzo kuonyesha bidhaa inayopendwa zaidi au isiyonunuliwa na nyingine.
Inaweza kutengeneza report mbalimbali iwe kwa siku/wiki/mwezi.
Kwa anaehitaji kujua zaidi kuhusu hii mifumo ya computer , karibu kwenye comments.