Jinsi ya Kujenga Mashine ya Kunasa Wateja

Dr. Said

Senior Member
Nov 16, 2010
125
531
Nikikwambia kuwa unaweza kumiliki mashine yenye uwezo wa kukuletea wateja kwenye biashara yako utaniamini?

Wateja wenye pesa mkononi tayari kununua bidhaa/huduma unazotoa?

Wengi nikiwaambia hili jambo nyuso zao zinakunjika kwa mshangao na kuona kama jambo lisilowezekana kabisa.

Wakati wanashangaa na kutoniamini, wanafunzi wangu wengi wameweza kumiliki mashine zinazowaingizia faida ya kati ya shs. 3,000,000 hadi shs. 30,000,000 kwa mwezi baada ya kuhaingika kwa kipindi kirefu.

Kama bado una mashaka na ukweli wa taarifa hizi unaweza kuangalia mahojiano na wanafunzi wangu 16 tuliowasaidia kumiliki mashine zao hapa:

View: https://www.youtube.com/playlist?list=PLLOg8s26qj-YMos8or0O428soi_z0Poa8.

Lakini kabla sijaanza, tuanze na swali la msingi...

Mashine ni nini?

Mashine ni chombo chochote chenye kurahisisha kazi zako.

Unatumia nguvu ndogo kupata matokeo makubwa.

Mifano ya mashine ni kama:
  1. Mashine ya kufulia nguo: inakurahisisha kazi ya kufua nguo.
  2. Gari: inakuokolea muda wa kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyengine.
  3. Pampu ya maji: inakurahisisha kuteka maji kutoka kisimani hadi kwenda katika tenki la maji.
  4. N.k.
Na ili mashine ifanye kazi inatakiwa kupitia hatua 3:
  1. Input (nguvu yako)
  2. Process (nguvu ya mashine)
  3. Output (matokeo)

Hatua ya 1: Input

Hii ni hatua za awali za kufanya kuandaa mashine yako kufanya kazi.

Input ni hatua anazochukuwa binaadamu kuiambia/kuielekeza mashine ifanye kitu gani.

Bila ya input mashine itashindwa kufanya kazi.

Kwenye gari input inakuwa:
  1. Kutia fungua na kuwasha gari
  2. Kubadilisha gia
  3. Kukanyaga excelerator
  4. Kuzungusha usukani
Mambo yote anayofanya dereva ndio input.

Kwenye mashine ya kufulia nguo, input inakuwa ni:
  1. Kutia maji
  2. Kutia nguo
  3. Kutia sabuni
  4. Kubofya swichi ya kuwasha mashine
Hatua ya 2: Process

Hii ndio sehemu ambayo mashine inafanya kazi kwa 100%.

Kwenye gari, process inakuwa kama ifuatayo:
  1. Umeme unaenda kwenye spark plug na kuchoma mafuta
  2. Ingini inawaka na kuzungusha crank shaft
  3. Crank shaft ikizunguka intake valve inafunguka na kunyonya mafuta
  4. Mafuta yanachanganyika na hewa na kuchoma mafuta na kusababisha piston kusogea
  5. N.k
Nafikiri umeelewa point yangu.

Kuna vitu vingi vinavyojitokeza tusivyovielewa (wala hatuhitaji kuelewa) vyenye kukusaidia kufika safari ya kilomita 80 ndani ya saa moja badala ya siku 3 kwa miguu.

Process (ambayo ndio mashine yenyewe) hujengwa na wataalamu na hakuna ulazima wa mtumiaji kuelewa process inaenda vipi kuweza kuitumia.

3: Output

Output ni matokeo yanayopatikana kutokana na process nzima ya mashine.

Output ya gari ni kufika sehemu unayotaka kwa wakati unaotaka.

Output ya mashine ya kufulia ni kutakatisha pamoja na kukausha nguo.

N.k.

Lengo siku zote output iwe ni kubwa kuliko input.

Na kama output ni ndogo kuliko input, hapo huna mashine au mashine yako haifanyi kazi kama inavyotakiwa.

Mfano wa input kuwa kubwa kuliko output ni kusukuma gari lako ukiwa unaenda kazini.

Nguvu unayotumia ni kubwa kuliko ungetembea mwenyewe.

Mashine ya kunasa wateja.

Ni kitu gani na tunaijenga vipi?

Ni chombo chenye kurahisisha upatikanaji wa wateja katika biashara yako.

Na kama mashine nyengine, nayo inakuwa na
  1. Input
  2. Process na
  3. Output
1. Input: Utengenezaji wa Traffic

Traffic ni mtiririko wa wateja watarajiwa kwenye duka/ofisi lako (kama una duka/ofisi), tovuti yako (kama upo mtandaoni) au simu yako.

Lengo la input ni kuwafanya walengwa wako watarajiwa wakutambue.

Zipo njia nyingi za kufanya hivi.

Kwa vile taalum yangu ni kujenga biashara mtandaoni, nitatoa mifano ya kufanya hivi kwa njia ya mtandao:
  1. Content Marketing: Kuandika makala kama hii kwenye tovuti/blog yako

  2. Forum Marketing: Kuingia katika forum kama hii ya jamii forum kuongea na walengwa wako. Makala hii ni mfano halisi ya forum marketing.

  3. YouTube: Kutengenezea video kupitia YouTube zenye kuzungumzia namna ya kutatua matatizo ya walengwa wako. Sisi tunafanya hivyo katika channel yetu ya ofisi na channel yangu binafsi.

  4. Social Media Marketing: Kutumia mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram na Tiktok.
Japokuwa njia hizi 4 ni nzuri za kutengeneza traffic, hauna control ya watu wangapi watakuja kwako.

Njia ambayo tumeiona ni ya rahisi na ya haraka kujenga traffic ni kubandika matangazo ya kulipia ya Facebook na Instagram.

Uzuri wa Facebook na Instagram ni kuwa:
  1. Ina umati mkubwa mno wa watu
  2. Ina uwezo wa kuonyesha tangazo lako mbele ya macho ya walengwa wako tu na kutolionyesha kwa wasiohusika.
  3. Gharama zake ni nafuu (hususana kama tangazo lako ni zuri)
Lakini matangazo nayozungumzia hapo sio matangazo ya kuuza bidhaa/huduma zako (sales ads).

Hapana.

Ni matangazo ya kuwakaribisha walengwa kwenye jukwaa lako (lead ads).

Unafanya hivyo kwa sababu hao walengwa wako hawakujui, hawakupendi na hawakuamini na ukikimbilia kutangaza utaonekana kama mmachinga anayewalazimisha kununua bidhaa zao.

Kama unalenga wagonjwa wa kisukari unaweza kubandika tangazo yenye kichwa cha habari ifuatayo...

"Jinsi ya Kutokomeza Ugonjwa wa Kisukari Sugu"

Unaandika makala kwa muhtasari ikisha unawakaribisha katika jukwaa lako kwa kuwaambia...

"Kama wewe ni mgonjwa wa sukari sugu uliyehangaika miaka mingi bila ya kupata mafanikio basi nina habari nzuri mno.

Nimekuandalia darasa BURE kabisa kupitia WhatsApp/Email/Skool yenye kukuonyesha jinsi ya kutokomeza ugonjwa huo kwa kutumia lishe tu.

Kuhudhuria hiyo darasa bofya hapa >> (Link ya kuingia ndani ya jukwaa lako)
".

2. Process: Jenga uaminifu

Process ndio mashine yenyewe.

Hili ndilo jukwaa utakalotumia kuwaandaa kisaikolojia walengwa wako kununua bidhaa/huduma yako.

Unaweza kujengwa jukwa la email, WhatsApp au jukwaa la kisasa kupitia skool.

Faida ya jukwaa la email ni automation; yaani unaweza kuziseti email zako kutoa darasa kila baada ya siku kadhaa pamoja na kuwafuatilia walengwa wako jambo ambalo litakufanya uokoe muda kwa kiasi kikubwa.

Faida ya jukwaa la skool ni leverage ya wanachama wengine: yaani wanachama wengine wanakuwa mabalozi wako na kukusaidia kufanya mauzo kwa ku share shuhuda zao.

Japokuwa WhatsApp inayo sifa hii kwa kiasi fulani, utajikuta unafanya kazi zaidi japokuwa process yako ikikaa vizuri unaweza kumweka mtu kusimamia group lako.

Toa thamani ya kufa mtu ndani ya jukwaa lako:

Kabla ya kuzungumzia bidhaa/huduma unayotoa, lazima ujenge uaminifu kwanza.

Na hakuna njia rahisi ya kujenga uaminifu kama kumuelimisha mlengwa wako kuhusu changamoto yake pamoja na namna ya kutatua hilo changamoto.

Unafanya hivyo kwa njia ya darasa la siku 3, kozi za bure, ushauri wa bure, kitabu cha bure n.k.

3. Output: Uza Kama Wazimu

Baada ya kujenga uaminifu, sasa upo tayari kufanya mauzo kama wazimu.

Utaweza kufanya hivyo ikiwa utamalizia kwa kusuka ofa zenye ushawishi wa hali ya juu.

Ofa zitakazowafanya watokwe na udenda, kutafuta pesa haraka na kukubembeleza upokee pesa zao.

Ikiwa pesa ulizowekeza kwenye matangazo ni ndogo kuliko mauzo yako basi mashine yako tunaweza kusema imefanya kazi.

Kama utakuwa unakula hasara, utafanya maboresho katika mashine yako hadi ikae sawa.

Mie huwashauri wanafunzi wangu kulenga returns za mara 3 au zaidi.

Yaani kama unawezeke $50 kwa siku basi hautakiwi kuingiza chini ya $150 kwa siku.

Ukiweza kufanya hivyo basi kazi yako ya msingi baada ya hapo itakuwa ni kuongeza bajeti ya matangazo tu.

Tunamshukuru Mungu wanafunzi wangu wengi tumewasaidia kupata returns za hadi mara 10, yaani kwa kila $50 wanazowekeza kwenye matangazo kwa siku zinarudi wastani wa $500.

Yenye kukulete wateja wengi ni ubora wa mashine yako na sio ubora wa tangazo lako

Ukishakuwa na mashine nzuri inayofanya kazi, kukuza biashara yako haraka linakuwa jambo rahisi mno.

Ndio maana baadhi ya wanafunzi wetu kama:
  1. Deogratius ameweza kukuza biashara yake kutoka shs. Milioni 2 hadi shs. Milioni 11 kila mwezi
  2. Zacharia kutoka shs. Milioni 5 kwa mwezi hadi shs. Milioni 36.
  3. Khalfan kutoka kuhaingika hadi zaidi ya shs. Milioni kwa siku
  4. Na wengine wengi
Wamewezaje?

Wametumia muda wao mwingi kuboresha mashine yao.

Natumai umefaidika na makala hii.

Dr. Said Said,
Mkurugenzi - Online Profits
 
Kumbe machine ya Kuhifadhi taarifa..
unajua nilivyoona kunasa wateja nikajua machine hiyo unaiweka inanasa na kuwavuta wateja popote waliko na kuwaleta kwako 😅😅
 
Mimi nimeelewa
Hongera sana na asante kwa mada nzuri
Nitaendelea kukufuatulia
Nimewekeza effort kwenye biashara mpya hivyo nitahitaji usaidizi wako katika kufikia malengo

Asante sana
 
Karibu sana. Unaweza ku connect na community yetu hapa: Wazo Fasta
 
Ndefu sana nimeshindwa kusoma naweza kupata mtambo huo unaotumia Solar ?
 
Back
Top Bottom