Jinsi ya kuifanya Kampuni ya Tanesco kuwa Kampuni Bora na ya Kujivunia Tanzania na Afrika kwa Ujumla

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
14,461
22,837
Tanzania tumebarikiwa vyanzo vingi vya nishati, Na Tanesco ni kati ya Makampuni mama ya Tanzania ambayo yanaweza yakaitangaza nchi yetu Africa na Pote Duniani (Yaani mfano wa kuigwa) Sio tu kutupatia nishati hapa bali tuweze kuwapa hata majirani zetu na kutuingizia fedha badala ya sasa kutumia tozo zetu...

Uzalishaji wa Nishaji mkubwa Iwekanavyo
Kwa kutumia vyanzo mbalimbali hydro, gas, solar, upepo na gas tunaweza kuzalisha zaidi ya mahitaji yetu na kuwauzia majirani wote kwa bei nafuu kuliko wanavyoweza kuzalisha wenyewe Tuna natural geographic advantage mfano tukimaliza Bwawa la Nyerere, bila kusahau upepo na Jua la Kutosha....

Kutumia Jua na kufanya kila Mtanzania kuwa Mzalishaji
Tukiwa nchi ya Tropic tuna Jua la kutosha yaani Megawatts kwa siku zinazopotea ambazo zingeweza kuvunwa ni nyingi sana na kwa kutumia mfumo wa smart meter kila mtanzania mwenye bati / paa la nyumba anaweza kuvuna huu umeme na kuwauzia Tanesco kama credit... (Tanesco wataufanyia nini huo umeme nitaelezea hapo chini)

Kuifadhi umeme wa Ziada (Batteries / Storage)
Duniani kwa sasa tatizo sio upatikanaji wa nishati jua tu lingeweza kutupatia nishati ya kutosha tatizo ni kutunza hio nishati mpaka itakapohitajika...., (ukizingatia usiku hakuna jua wala sio kila wakati kuna upepo) kuna research nyingi zimefanyika kuweza kupata storage muafaka na bado zinaendelea kufanyika...., Ila kwa kutumia Pumped Storage Hydropower katika mabwawa yetu hii itakuwa a perfect storage na very efficient...

Yaani ule umeme wa solar na upepo na wowote utakauzalishwa na kuuzwa kwa Tanesco wakati matumizi ni madogo utatumika ku-pump maji kutoka kwenye bwawa la chini kule kwenye Hydro Electric Power Generation zetu na kurudishwa juu mpaka utakapohitajika tena ili hayo maji kuachiwa tena na kutengeneza umeme (a perfect battery)

Kuuzia Umeme Majirani zetu Wote
Kwakuwa tutakuwa na surplus kuliko tutaweza kuwauzia majirani zetu na kujipatia fedha, hence Tanesco badala ya kuonekana wanatumia Tozo zetu wataanza kutupatia fedha..., Yaani hadi watu mtaani wataanza kuvaa Tshirt za I Love Tanesco.....

Kupunguza / Kuacha matumizi ya LPG
Mitungi / Gas ya LPG tunanunua kutoka nje ambapo inatugharimu fedha za kigeni sasa kama units za umeme zitashuka kutokana na surplus production badala ya kupiga chepuo la kila nyumba iwe na mtungi wa gas badala yake kila nyumba itakuwa na jiko la umeme, oven, jug, rice cooker n.k.,

In short haya yakifanyika hili Shirika letu TANESCO litakuwa la kujivunia Tanzania na litaipeperusha Bendera yetu pote Duniani Yaani ukiwa Ulaya unasema nimetokea Tanzania the land of Serengeti, Kilimanjaro and Tanesco.... (Tanzania the Cradle of Humanity)....
1666992261021.png

Huyo Twiga ana Potential Sana akiwezeshwa atatutoa Kimaso maso watanzania..... Tafadhali tusimuue huyu Mtoto Wetu bali Tumuwezeshe aweze kutuangazia Pote Afrika na Duniani kwa Ujumla...... Tupate cha kusema kwamba na sisi tuna Made in Tanzania.....
 
Kwenye umeme wa jua wamesha chelewa wamesha toa vibali kwa baadhi ya makampuni wauza sola na wanauza set_up zao complete, wanakopesha kwa riba kubwa atakae kubali kulipa hizo credits kwa tanesco ni nani!!? Labda kwa ubabe
 
Huduma mbovu
Umeme kukatika bila taarifa
Mgao bila taarifa
Kutoa taarifa za uongo

Need I say more?
 
Tanesco inabidi nayo ipate reset button, hii kampuni iondolewe kwenye kuzalisha umeme, iwe ina sambaza tu umeme, serikali iruhusu na iweke mazingira rahisi ili umeme uzalishwe na watu au makampuni binafsi then wawauzie umeme Tanesco, pia metros na municipalities ziruhusiwe ziwe na vyanzo vyake vya umeme
 
Kwenye umeme wa jua wamesha chelewa wamesha toa vibali kwa baadhi ya makampuni wauza sola na wanauza set_up zao complete, wanakopesha kwa riba
Haujanielewa mfumo ninaosema utakuwa mtu ananunua panels pekee haitaji batteries (which are expensive and hard to manage) na hizo kampuni pia zikitaka hazitaangaika na wateja mitaani tu nazo zitawauzia Tanesco (so long as ni cheaper kuliko vyanzo vyao vingine)
kubwa atakae kubali kulipa hizo credits kwa tanesco ni nani!!? Labda kwa ubabe
Haujanielewa Mkuu kuna kitu kinaitwa smart meter and grids..., Yaani kinachofanyika kila mtu mwenye paa la nyumba anaweka solar panel (zake akitaka) sasa badala ya umeme wa ziada kutunza kwenye battery (which is expensive) umeme unabadilishwa na kuwa wa aina sawa na umeme wa grid (Tanesco) na kupelekwa / kutumika kwako na kwa wengine...., Na kwa mfano wangu unaweza kwenda grid ukatumika ku-pump maji juu kama storage ya baadae....

Credit Nazomaanisha ni Nini ?
Sasa kama Tanesco wanakuuzia umeme kwa unit moja inawezekana kila umeme utakaowauzia unaweza ukawapa kwa nusu au robo unit..., yaani mwisho wa siku kama ulitumia unit kumi na wewe kuwauzia unit ishirini utajikuna bil yako inasoma sifuri au luku hauhitaji kujaza (Yaani una Credit)

Kwahio nachosema kila nyumba yenye Paa kila Mtanzania anaweza akawa Mzalishaji wa Umeme na kupata Faida katika uzalishaji wake...
 
Huduma mbovu
Umeme kukatika bila taarifa
Mgao bila taarifa
Kutoa taarifa za uongo

Need I say more?
Naam na hapo wengi wanaipigia hilo Rungu ili waweze kuuza hili Shirika / Kulibinafsisha..., Mimi nasema kwa vyanzo tulivyonavyo na asset ilizonazo Tanesco inaweza ikawa darling company of Africa na dunia kwa kuwa environmental friendly...

Yaani tukajivunua Kampuni Yetu (Na sio Kampuni ya Wadau Fulani) Yaani ukienda ughaibuni una tshirt zako tatu moja picha ya Kilimanjaro, Nyingine Serengeti na ya Tatu Tanesco...... (Powering Africa) Hii Dark Content its about time iwe Bright Continent

Huyo Twiga ana Shingo Ndefu tumuache aangazie mbali sasa kama wa kwenye Ndege zetu Tumeshindwa kumfanya apae hata huyu pia tumuue

eti TANESCO ..., does it make sense !!!! (Tafadhari don't Give our Company a Bad Name)

1667026254884.png
 
Tanesco inabidi nayo ipate reset button, hii kampuni iondolewe kwenye kuzalisha umeme,
Moja kwani kina Dowans na wale Matapeli walikuwa wanafanya nini ?, Tatu sidhani kama umekatazwa kuzalisha umeme wa solar n.k. ila sio kwamba sababu unaweza ndio kila mtu achukue kila chanzo na kuweka Generators au Kusimika Minara ya Wind Generators (Huo utakuwa uharibifu wa Mazingira)

By the way kwahio unataka lile Bwawa la Nyeyere tume nani ? Tatu unadhani tukiwapa watu binafsi wazalishe kipindi hiki cha ukame wangefanya nini kutumia maji ya Bomba au ya Dasani ?!!! Au wangeagiza Wese kutoka nje na kukucharge accordingly (Kumbuka hapo itakuwa sio service tena bali ni for profit...)
iwe ina sambaza tu umeme, serikali iruhusu na iweke mazingira rahisi ili umeme uzalishwe na watu au makampuni binafsi then wawauzie umeme Tanesco, pia metros na municipalities ziruhusiwe ziwe na vyanzo vyake vya umeme
Kwahio kama vle tulivyokuwa tunanunua umeme kwa Dowans alafu Tanesco alafu sisi ?!!!

Yaani in short tuongeze madalali ?!!!!; Hivi unajua Bwawa la Nyerere likiisha (if it will ever will) tutakuwa tuna surplus ?!!!; Kwahio tuwape hio kazi rahisi watu Binafsi Tanesco iendelee kuhangaika na kazi ngumu ya kusambaza na kugharamia miundombinu wakati wewe average Joe ndio unalipia kila kitu ?

Narudia tena hivyo vyanzo vilivyopo vikitumika vinatosha hakuna haja wala sababu ya kuongeza overheads kwa kila municipality (overheads means costs); Pia kama umenisoma hapo Juu kwenye Point ya pili sio kila Municipality tu izalisha bali kila nyumba izalishe kwa kutumia solar na kuwauzia Tanesco kwa bei ya Robo ambayo wananunua.... (Na malipo yanakuwa Credit za Units)
 
Tanesco inabidi nayo ipate reset button, hii kampuni iondolewe kwenye kuzalisha umeme, iwe ina sambaza tu umeme, serikali iruhusu na iweke mazingira rahisi ili umeme uzalishwe na watu au makampuni binafsi then wawauzie umeme Tanesco, pia metros na municipalities ziruhusiwe ziwe na vyanzo vyake vya umeme
Bei ndo itapanda mara 1000. Utaambiwa tunanunua unit 1 kwa 10k inabidi tukuuzie kwa 15k.

Utakubali?

Transmission na Distribution ibaki kwa sekta zinginezo ila Tanesco inatakiwa ibaki na production tu.
 
Bei ndo itapanda mara 1000. Utaambiwa tunanunua unit 1 kwa 10k inabidi tukuuzie kwa 15k.

Utakubali?

Transmission na Distribution ibaki kwa sekta zinginezo ila Tanesco inatakiwa ibaki na production tu.
Yes/No mkuu, hii ni free market means kutakuwa na ushindani wa kibiashara, elewa China umeme mwingi unazalishwa kwa model hii,mfano huku lingusenguse pale monastery ya peramiho na Hanga wana uwezo wa kuzalisha umeme na kuwauzia tanesco au municipal ya songea ambayo itawauzia watumiaji directly, tanesco it's to big to go down ila tunaweza kuwafanya wawe distributors wa umeme tu, wasiwe wazalishaji
 
Bei ndo itapanda mara 1000. Utaambiwa tunanunua unit 1 kwa 10k inabidi tukuuzie kwa 15k.

Utakubali?
Kitu ambacho watu hawajui Kampuni kama Tanesco au inayotoa Huduma kama hii ni Too Big to Fail..., kwahio hata ikibinafsishwa alafu gharama za utengenezaji zikawa juu (hata kwa magumashi) ni kwamba Tozo zetu ndio atalipwa mtu binafsi kama Ruzuku ili tu waendelee kutoa huduma...

Binafsi kila awezaye kuzalisha efficiently na environmentally friendly na azalishe na Tanesco inunue at the cheapest price (hutaki acha, kafanya biashara nyingine za kulima nyanya au chochote kile)
Transmission na Distribution ibaki kwa sekta zinginezo ila Tanesco inatakiwa ibaki na production tu.
Transimission hao watu wakiamua kuleta bill kwa Tanesco ambazo hazieleweki ? (Tanesco watakataa kulipa ?) au wakiona wanalipwa ndogo hence kuacha kufanyia maintenance au kuweka vishoka na watu kuanza kupigwa shoti na kuangukiwa na nguzo unadhani nani atapay the price kama sio kina sisi huku kitaa ?

Pili watataka wafanye transmission mijini tu na sehemu nzuri nzuri unadhani ukiwaambia wapeleke huko mashambani in the middle of nowhere ambako kuna wateja wanne tena kwa elfu 27 watakubali ?
 
Moja kwani kina Dowans na wale Matapeli walikuwa wanafanya nini ?, Tatu sidhani kama umekatazwa kuzalisha umeme wa solar n.k. ila sio kwamba sababu unaweza ndio kila mtu achukue kila chanzo na kuweka Generators au Kusimika Minara ya Wind Generators (Huo utakuwa uharibifu wa Mazingira)

By the way kwahio unataka lile Bwawa la Nyeyere tume nani ? Tatu unadhani tukiwapa watu binafsi wazalishe kipindi hiki cha ukame wangefanya nini kutumia maji ya Bomba au ya Dasani ?!!! Au wangeagiza Wese kutoka nje na kukucharge accordingly (Kumbuka hapo itakuwa sio service tena bali ni for profit...)

Kwahio kama vle tulivyokuwa tunanunua umeme kwa Dowans alafu Tanesco alafu sisi ?!!!

Yaani in short tuongeze madalali ?!!!!; Hivi unajua Bwawa la Nyerere likiisha (if it will ever will) tutakuwa tuna surplus ?!!!; Kwahio tuwape hio kazi rahisi watu Binafsi Tanesco iendelee kuhangaika na kazi ngumu ya kusambaza na kugharamia miundombinu wakati wewe average Joe ndio unalipia kila kitu ?

Narudia tena hivyo vyanzo vilivyopo vikitumika vinatosha hakuna haja wala sababu ya kuongeza overheads kwa kila municipality (overheads means costs); Pia kama umenisoma hapo Juu kwenye Point ya pili sio kila Municipality tu izalisha bali kila nyumba izalishe kwa kutumia solar na kuwauzia Tanesco kwa bei ya Robo ambayo wananunua.... (Na malipo yanakuwa Credit za Units)
Mkuu hii ni debate let's discuss kama mada sip mtoa mada,China 🇨🇳 umeme mwingi unazalishwa na watu binafsi ambao wanautia kwenye national grid kwa makubaliano na kampuni mama,wenzetu hapo Capetown wameanza mchakato huu wa kuzalisha umeme na kuwauzia metro/eskom.
 
Yes/No mkuu, hii ni free market means kutakuwa na ushindani wa kibiashara, elewa China umeme mwingi unazalishwa kwa model hii,mfano huku lingusenguse pale monastery ya peramiho na Hanga wana uwezo wa kuzalisha umeme na kuwauzia tanesco au municipal ya songea ambayo itawauzia watumiaji directly, tanesco it's to big to go down ila tunaweza kuwafanya wawe distributors wa umeme tu, wasiwe wazalishaji
Alafu Bwawa la Nyerere tumpe nani ?

Mkuu haujakatazwa mpaka sasa au dakika hii kazalishe solar huko Mabwepande kama per unit gharama yako itakuwa ndogo wauzie wateja wako..., ila usitandaze nyanya kila sehemu ukatuharibia mandhari au kutuletea hatari.....

Kuwekeza sio lazima tukupe ofisi zetu na vyanzo vyetu ambavyo vipo tayari tengeneza vyako...., ila kumbuka economy of scale Tanesco anao uwezo wa kutengeneza unit moja cheaper kuliko mtu yoyote individual kwa dakika / sekunde hii; wengi wanataka wafanye udalali na kula huu mkate ambao ushaiva badala ya kukanda unga wao na kutengeneza wa kwao

Unasema China wanafanya hata huku wewe kafanye nenda sehemu ambapo hakuna miundombinu weka yako na invest from bottom up huone kama Tanesco watakaa au kama utaweza ku-break even...!!!
 
Mwaka wa pili huu hawataki kuunga umeme..

Nimewaambia kama ni rushwa nitawapa eti mpaka niende kuwabembeleza ofisini kwao....

Hii nchi ngoja niendelee na solar zangu hadi aje raisi wa kuwafukuza kuanzia wakurugenzi
 
Mkuu hii ni debate let's discuss kama mada sip mtoa mada,China 🇨🇳 umeme mwingi unazalishwa na watu binafsi ambao wanautia kwenye national grid kwa makubaliano na kampuni mama,wenzetu hapo Capetown wameanza mchakato huu wa kuzalisha umeme na kuwauzia metro/eskom.
Si ndicho nilichosema hapo ?, Tena mimi sijasema Kampuni tu nimesema kila mtu mwenye paa la nyumba aweze kuwauzia Tanesco umeme kwa bei ya kutupwa (apewe credit za units) na tanesco pekee ndio wana uwezo wa kutunza umeme huo efficiently kuliko mtu yoyote as well as kuwauzia wengine at any given instant....

Hatuhitaji kipindi hiki kuigawa hii keki ili tugawane faida wakati tuna uwezo wa kutoa surplus ya umeme cheaply....

Huko ni Kufilisi Shamba la Bibi...
 
Mwaka wa pili huu hawataki kuunga umeme..

Nimewaambia kama ni rushwa nitawapa eti mpaka niende kuwabembeleza ofisini kwao....

Hii nchi ngoja niendelee na solar zangu hadi aje raisi wa kuwafukuza kuanzia wakurugenzi
Naam tunahitaji uwajibikaji na transparency na watu waliopo kazini kupewa targets za kufanya wakishindwa warudi mtaani wengine waingia pale kufanya kazi..., Yaani Tanesco ni Kama Ferrari yenye injini ya Pikipiki..., kwahio mimi nasema badala ya kuuza hii Ferrari angalau tuiwekee hata injini ya Passo...
 
Fukuza wote anza upya iwe mali ya serikali
Mali ya UMMA kaka tuwe na uwezo wa kuwawajibisha hivi sasa ilivyo Serikali ndio inawafilisi kwa kutumia umeme bure na bila kulipa..., Nina uhakika wanaidai Serikali Pesa Lukuki...., na bado wanalazimishwa na Dowans Tuwalipe..., wewe unategemea Shirika kufanywa kama Kibubu cha wachache litaweza ku-survive
 
Mimi nasema waikabidhi serikali kwa sababu itakuwa salama na haitakuwa na kufirisika firisika sababu kuu ni RUSHWA.....na upigaji wakiisingizia wanaidai serikali, kumbe ni kakipengele wamekaongeza

WEZI NA WAVIVU HAWA USIWATETEE

LEGISLATION. TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY LIMITED (TANESCO Ltd) is a company limited fully owned by the Government of Tanzania under the Ministry of Energy and Minerals and hence was duly registered under the Companies Act Cap 12 [R. E.

Huenda hio Serikali yenyewe ndio Tatizo wewe hujajua..., Issue kuwe na transparency watu wapewe targets na wasifikishe na lisitumike kama Kibubu cha Serikali.....

All in all inabidi tubadilike kama wananchi tuwe wawajibikaji sio kuuza kila kitu sababu ya kutokuwajibika badala ya kuuza tuanze fukuza fukuza mtu akishindwa targets

Binafsi Nasema Shirika liwe letu sisi wananchi kila mtu akizalisha na kuliuzia na kutumia huku tukiuza East Africa Nzima na kuingiza Pesa za kutusaidia kwa mengine.., Vyanzo Tunavyo tuvitumie
 
Back
Top Bottom