Habari wadau,
Mimini kijana mchakarikaji hapa mjini. Katika kutafuta njia ya kuweka maish yangu na familia yangu level flani ambayo hata nikiondoka wasipate taabu. Elimu yangu ni ya kawaida. Nina advance diploma ya IT na diploma ya TAX ( maswala ya kodi). Lakini shughuli zangu zime base kwenye maswala ya kodi. Kwani nafanya biashara ya clearing and forwarding na nina wateja wangu binafsi ambao nawatolea mizigo bandarin na airport. Mpaka sasa nimeamua kufanya biashara hii kama ndio main stream ya kuendesha maisha yangu. Lakini still naona naifanya biashara hii kienyeji. Maana sina elimu yoyote kwenye maswala ya usimamiz wa biashara sasa nataka nisome BA lakini kwa nature ya kazi yangu sio rahisi kuingia darasan. Na kusoma.
Hivyo nilikuwa naomba kama kuna mdau yoyote anayefahamu jinsi gan naweza kusoma /ku apply online course ya BA anijuze tafadhali.
Shukrani tele & heri ya mwaka mpya.