Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,675
Hili jambo limkute jirani yako tu, likiikumba familia ni majonzi na mtihani mkubwa sana. Hatukuwa tumewahi kufiwa na mmoja wa wanafamilia, kwa maana ya kaka au dada wa tumbo moja na baba mmoja. Misiba mingi ilikuwa ni kwa ndugu na jamaa tu wa karibu. Msiba huu wa dada yetu aliyekuwa "kichwa" na msaada mkubwa kwa familia ulitokea mwezi March 1993 wakati huo mimi nikiwa nimemaliza kidato cha nne nikisubiri matokeo ya kwenda kidato cha sita.
Huyu dada aliugua kwa muda mrefu sana na hata mimi nilipokuwa narudi likizo kijijini kwetu baada ya kufunga shule nilikuwa namkuta anazidi kudhoofika. Miaka hiyo wengi hatukuwa na "uelewa" juu ya mambo ya UKIMWI, dalili zake na hata "uzoefu" wa kuuguza mgonjwa huyu. Homa za hapa na pale na kikohozi cha muda mrefu kilimsumbua dada. Alikuwa tayari na mtoto mmoja ambaye naye bahati mbaya alizaliwa akiwa na maambukizi.
Hivyo baada ya dada kufariki huyu mjomba wangu alidumu kwa miaka miwili naye tukazika. A young talented boy! Alitumia mkono wa kushoto kuandika na kucheza mpira. Ama hakika UKIMWI umeenda na wapendwa wetu wengi na umekatiza ndoto za watu wengi. Kwa maisha ya kijijini na elimu duni ya afya na huduma mbovu ya afya kijijini, dada aliishia kupewa dawa za yale magonjwa nyemelezi tu lakini haikufua dafu.
Maana Kituo cha afya kilichokuwepo hakikuwa na vipimo. Ilikuwa ni kituo kilichojengwa kwa msaada wa Masista wa kanisa katoliki. Ambao zaidi ya kujitolea kwao sbb ya "usista" wao na nadhiri zao za kutumikia jamii inayowazunguka, hawakuwa na elimu darasa ya mambo ya tiba. Kama ada ya maisha ya wengi vijijini wazo kubwa lilikuwa ni dada kurogwa. Haikuingia akilini mtu kuugua kiasi kile bila kupata nafuu na kudhoofu.
Sababu ya kukohoa sana, shangazi alitoa wazo kuwa inabidi dada akatwe "kilimilimi" maana mabibi pale bush wanasema hicho ndio kitakuwa kinamsababisha akohoe sana na baada ya kukatwa ili kidonda kile kipone haraka alitakiwa kunyweshwa maji yaliyopatikana kwenye pango la mti na hasa mbuyu. Siku kadhaa akaja bibi wa pale kijijini ambaye ni mtaalamu wa kukata vilimi. Dada, siku moja alfajiri na wembe mpya wa topaz alikatwa kilimilimi, maana ilisemwa ni lazima kikatwe kabla ya jua kuchomoza.
Hata baada ya kukatwa na kunyweshwa maji ya pango la mti, dada aliendelea kukohoa sana sana. Akodhoofika na kukonda mno. Tukiwa wenye imani ya dini ya Katoliki kila jioni nilipokuwa likizo ya kidato cha nne dada aliniita na kusali nae rozari ili Mungu ampe afya njema. Hata kwa elimu yangu ya kidato cha nne nami sikuwa najua kuwa ule utakuwa ni UKOSEFU WA KINGA MWILINI. Dada aliteseka, alikonda na kuisha sana. Ilifikia wakati nami nikimtazama ninatoa machozi. Ama hakika UKIMWI na mateso yake ya wakati huo ya bila ARV yasikie tu kwa jirani.
Ziliuzwa ng'ombe na mbuzi kuzunguka kwa waganga kujua hasa "mbaya wetu" ni nani? Huyu mlozi wa familia ni nani? Hakuna hata mmoja aliyekuwa na wazo la kwenda mjini kwenye vipimo vikubwa. Na waganga wote tuliopita hakuna hata mmoja aliyeacha kutuambiwa kuwa "huyu karogwa kwa kutupiwa jini". Madawa na mitishamba ilijaa ndani kwa wingi bila kuleta matokeo chanya. Siku zikaenda na hali ya dada inazidi kuwa mbaya na ya kukatisha tamaa. Tulisafiri mpaka Morogoro sehemu za Vidunda kufuata mganga, lakini hakukuwa na uafadhali.
Wakati wote huu dada yangu mdogo na Mama ndio waliokuwa wauguzaji, ama hakika waliuguza bila tahadhari sababu hawakuwa na elimu juu ya mgojwa na namna ya kumuuguza. Baada ya kipindi kirefu cha mateso Dada alifariki. Naukumbuka mchana ule, mchana mgumu kuwahi kuuona katika maisha yangu ya ujana, ama kweli roho itokapo katika mwili mwanadamu hujijua. Dada isivyo kawaida aliniita, niliitikia wito, akaniomba nikamate rozari na misale ya waumini, nifungue sala ya wagonjwa na tusali kwa moja.
Akiitikia kwa tabu na kwa kukoroma tulisali pamoja, baada kama ya dakika 15 niliona mtu amekaa kimya na baadae "kuhangaika" hapa na pale. Loooh! Kumbe ndio mwili ulikuwa unaacha roho na dada aliniita kuniaga, tuliagana kwa rozari na mishale ya waumini. Alasiri ya 08/03/1993. Upumzike kwa Amani. Baada ya kuzika maisha hayakuwa kama zamani, sehemu ya ng'ombe zilizotumika kunilipia ada zilipungua sana sbb ya mizunguko ya waganga na hali ya ugonjwa.
Hata anakufa hakuna aliyejua ulikuwa ni UKIMWI, wengi walilaani juu ya "uchawi" na jini lililotupiwa familia. Na ama hakika Waganga walisisitiza kuwa "jini" hilo bado linazungukazunguka..Litaondoka na mwingine. Bila kujua lolote Mama alianza nae kuugua, kwa dalili zilezile za Dada. Mama alikonda sana, nilirudi likizo ya kwanza ya kidato cha nne namkuta mama amelala nje juu ya mkeka amebaki kichwa tu, amekonda na kukondeana. Mtoto wa kiume nililia sana kwa hali ile ya Mama. Nikajisemea hili jini kweli litatumaliza wote. Baadae tena dada yangu aliyeshirikiana na Mama kumuuguza marehemu akaugua, dalili zilezile za Mama tukawa na wagonjwa wawili ndani ya nyumba... tuliuza mpaka ndama kuokoa maisha ya ndugu hawa. Hakuna wazo la hospitali, kila mtu ni kutegua mtego wa jini.
Siku moja akawa amefika Padre kigangoni kwetu, Padre huja mara moja kwa mwezi kusoma misa na kutembelea wagonjwa, baada ya misa ile nilimuomba Padre afike nyumbani kumuombea mama yangu na dada na hakika mama alistahili kuombewa sababu alikuwa mwanachama mzuri wa umoja wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA), hivyo ilikuwa rahisi kwa Padre kufika na kuwaona. Ndani ya nyumba ya nyasi yenye giza hata mchana wa jua kali Baba Paroko akaingia. Alipowatazama wagonjwa akatokwa na machozi.
Akahimiza waondolewe haraka na atawakimbiza yeye mjini kwa gari yake wakapate vipimo vikubwa...wachache sana waliokubaliana na padre wakijua kuwa ule ni ugonjwa wa kurogwa sio wa hospital, na kuwapeleka hospital ndio mwisho wa mchezo. Nguvu za paroko na ushawishi wake zikashinda, Mama na dada haraka mjini, hadi kufikia jioni majibu yakawa ni TB kwa wote wawili na baada ya udadisi wa madaktari ikabidi mtoto wa dada aende kupimwa, naye tukamsafirisha mpaka mjini.
Tobaaaa! Mtoto akakutwa na UKIMWI alioachiwa na mama yake, hivyo Mama na Dada waliambukizwa TB sababu hawakuwa na tahadhari ya kumuhudumia marehemu. Wakati huo hakukuwa na "Mpango wa kutokomeza Kifua Kikuu" wa kutoa dawa bure, hivyo ilihitaji kugharamia rundo la vidonge. Watu waliuza mifugo kununua dawa kwa shingo upande. Mama na dada wakawekwa hospitali na kunywa dawa kwa uangalizi mkubwa sana, baada ya miezi mitatu afya zao zilirudi kwa kasi.
Kumbe haikuwa jini kama wale waganga walivyosema, ulikuwa ni UKIMWI kwa marehemu na kwa mama na fada ilikuwa ni TB. Maisha yakaenda na mama akarudi katika hali yake ya afya njema. Nikiwa mbioni kuingia kidato cha sita nikaanza kuugua sana nikiwa shuleni. Kikohozi na jasho kali wakati wa usiku. Kula sana chakula lakini ndani ya nusu saa nasikia njaa. Shule haina vipimo zaidi ya zahanati unayopewa dawa kulingana na dalili za ugonjwa. Niliugua sana sana kumbe nami ilikuwa TB, maana wote hatukuchukua tahadhari wakati tukimuuguza dada, bahati nzuri shule ilinipeleka hospitali na kutibiwa mapema, ilibidi niahirishe mwaka mmoja ili nipate afya nzuri. Mwisho wa siku wote tukapona, haikuwa jini kwa dada wala kwa Mama, bali ni UKIMWI na TB.
Miaka miwili baadae mtoto wa dada akafariki,wakati huo hakukuwa na ujuzi wa kuzaliwa bila VVU hata kama mzazi anavyo, wala ARV haikwepo. Bwana mdogo alifariki katika mateso na mahangaiko makubwa sana. Tukamzika pembeni ya kaburi la Mama yake na juu ya kaburi tukaandika "YEYE ANIAMNIYE MIMI HATAKUFA, BALI ATAISHI MILELE". Ni miaka zaidi ya 20 sasa, Wapendwa wetu wametangulia mbele za haki.
UKIMWI ulikatisha maisha yao, ama hakika balaa la ugonjwa huu lisikie kwa jirani. Jamani UKIMWI ni chanzo cha umasikini, lakini elimu ya msingi ya afya ni muhimu kusambaa mpaka vijijini. Isingalikuwa mtumishi yule wa Mungu, basi "ujinga" wa kuamini jini ungeendelea. Hii hali ipo sehemu nyingi, kuona UKIMWI kama ugonjwa wa kurogwa. Wasichekwe wazee wetuu kwa kuamini ktk waganga na tiba mbadala. Tuwaelimishe na kuokoa jahazi. Ninawapa pole wale wote waliowahi kupoteza wapendwa wao kwa UKIMWI. Tuwaenzi kwa kuepuka gonjwa hili, kuwa waaminifu, kuacha kabisa au kutumia kinga kwa wasioweza kujizuia.
RAHA YA MILELE UWAPE EEE BWANA, NA MWANGA WA MILELE UWAANGAZIE, WAPUMZIKE KWA AMANI AMINA