Jinsi Mwonekano wako unaweza kuwa na athari chanya au hasi wakati wa Usaili wa kazi

Wild Flower

JF-Expert Member
Jul 20, 2023
336
696
Unapokwenda kwenye Usaili wa Kazi, Mwonekano wako wa mwanzoni tu, unaweza kuwa na athari kubwa wakati wa mahojiano. Na hiyo ni kwasababu tafiti mbalimbali zinaonesha baadhi ya Waajiri hufanya maamuzi kuhusu ajira ndani ya sekunde 30 za kwanza wanapokutana na mwombaji kazi.

Hata kama Usaili si wa kazi rasmi, (kazi za kiofisi) inashuriwa kuvaa Mavazi ya heshima kwa muktadha wa Mahojiano. Ni muhimu kuhakikisha mwonekano wako ni Nadhifu.

Hata hivyo, Tofauti na wengi tunavyodhani, Usaili huanza mara tu unapoingia kwenye Ofisi iliyokuita. Hakikisha unaonesha Heshima kwa uliowakuta kwa kusalimiana nao vizuri.

Jitahidi kuwa na Uso wa tabasamu na wakati wa Mahojiano na Waajiri hakikisha unawaangalia Usoni. Kuangalia chini au pembeni kunaweza kutoa ishara ya woga au kutokuwa na ujasiri.

Epuka kuzungumza vibaya kuhusu sehemu ya kazi ulipotoka wala changamoto ulizokutana nazo katika kazi yako ya awali. Hata kama uzoefu wako wa kazi uliopita haukuwa mzuri, Jikite kwenye kuonesha ujuzi wako na sifa chanya ulizozipata.

Kitu kingine muhimu sana, Kumbuka kuzima au kutoa muito wa Simu kabla ya kuingia chumba cha mahojiano.
 
Asante kwa maarifa haya. Ukiingia kwenye chumba cha interview unapaswa usalimiaje kwa kuwa kunakuwa na watu wa rika fofauti na jinsia tofauti.
 
Asante kwa maarifa haya. Ukiingia kwenye chumba cha interview unapaswa usalimiaje kwa kuwa kunakuwa na watu wa rika fofauti na jinsia tofauti.
Goodmorning/Goodafternoon every one.

Lkn sio lazima. Unaweza kuta ukaanza kusalimiwa wewe 😀
 
Back
Top Bottom