Hello wanachama wa jamiiforums leo ningependa niweke mkasa wangu baada ya kuwa msomaji wa humu ndani kwa muda mrefu.
Niliwahi kuwa na mke hapo miaka ya 2018 hadi 2021, pia nina mtoto moja ambae hadi sasa yupo kwa mama yake japo huwa naenda kumcheki.
Ni mwaka 2017 nilipokutana na huyu binti nikiwa mhitimu wa chuo tangu 2014, sikupata ajira ikanibidi nihamie kwenye biashara, mishe zangu zilitosha kuniingizia kama laki 5 hivi kwa mwezi hivyo kimtindo kwa mbali nilijiweza na kuwa na kagetho kangu, nilimpata binti flani aliemaliza diploma katika moja ya chuo karibu, alikuwa na miaka 20 hivi huku mimi nina 28, penzi lilikolea nikaenda kutoa posa kwa binti nikakubaliwa tukaanza Maisha ya mume na mke.
Tulifanikiwa kupata mtoto mwaka 2018 mwishoni, na muda sio punde biashara nayo ikachanua ile mbaya kwa chimbo nililopata bidhaa kwa beii rahisi, nilipata wateja wa uhakika constant supply kila wiki napata faida si chini ya milioni 1, hakika mambo yalianza kwenda vizuri mno, wateja nakuwa nawafanyia delivery mimi nanunua mzigo katika chanzo cha bei rahisi sana in bulk.
Tukahamia nyumba ya kupanga laki 5 kwa mwezi, niliweza kununua usafiri aina ya brevis, nae nikamfundisha gari nikanunulia carina ti, kiwanja nacho niliweza kununua ujenzi japo nilipiga fenzi tu.
JINSI JINAMIZI LA PESA LILIVYOHARIBU MAHUSIANO
haya mambo yalianza 2020
Mafanikio yangu yamecheza sehemu kubwa sana katika kumpagawisha huyu binti mpaka kutia dosari mahusiano yetu ya ndoa
Okay, kitu cha kwanza ni kwamba pesa zikiwepo kuna wanawake wakijua kwamba mkiachana kuna kugawana mali pasu kwa pasu huwa wanaona ndio silaha yao ndani ya ndoa kukufanya uwatii au kukufilisi, tulipopishana kauli kidogo tu ama kugombana, mwenzangu basi hasira zikimpanda akawa anatishia tutaenda mahakamani kugawana mali pasu kwa pasu na ataondoka na mtoto kumlea mtoto kivyake, ikabidi niwe natulia tu.
Hapa ndipo nilipokuja kugundua kwanini watu wenye vipato vya kawaida wanadumu zaidi, hata sisi kipindi bado sijatoboa hii jeuri haikuwepo, tukipishana kauli kulikuwa hakuna hio button kwamba hata akiniacha atanufaika kiuchumi, hali hii ilitufanya tuwe tuna stick together kujifunza kuishi pamoja kutatua tofauti zetu na kuyaimarisha mahusiano kwa changamoto tulizopitia pasi kuwa na exit strategy ya fasta.
Ni kama vile kupanda mlima Kilimanjaro kama wewe ni masikini ama una uwezo wa kawaida inabidi wote mpande mlima mpaka kileleni lakini kama mna uwezo na moja wenu kachoka basi anaweza pigia simu helikopta ije kumchukua, yani akichoka kidogo tu tegemea anakuacha upande mwenyewe huo mlima.
Kitu kingine ni kwamba pesa ikianza kuingia, ni ngumu kumridhisha mwenzako kwa zile zawadi za elf 20 ama elf 50 za zamani, hizo zinaanza kuonekana taka taka sio level zake, tulizoea kwenda out mara chache sana siku special mgahawa flani hivi lakini nilivyompeleka pale aliona nimemdharau, yeye akawa analalamika kwamba kwa uwezo wangu wa sasa inabidi twende hoteli, birthday nilizoea kumpa zawadi kama ya elf 30 hivi lakini akaanza kuona namshusha thamani inabidi ninunue hata simu mpya ya milioni, yani kiufupi matendo ya utu wa kimapenzi yanaanza kupimwa kulingana na level ya mafanikio mapya. Badala ya kuangalia mtu anakujali unaanza kupima hiki kitu nimetumia asilimia ngapi kukipata katika pesa nilizonazo, inaanza kuwa ngumu san ahata kuomba msamaha ama kumu impress kwasababu tayari kwake vitu unavyomfanyia kwa upendo anaanza kupiga hesabu kwamba hiki kitu kimenigharimu elf 30 tu kati ya million 6 nazoingiza kila mwezi. Yani maneno ndio kabisaaa!! Yanakuwa hayana thamani.
Kitu kilichoanza kunitambulisha kwake kilikuwa ni uwezo wangu wa kiuchumi kuzidi mahusiano yetu ya mke na mme, well to be honest siwezi kusema kwa mba mke wangu alikuwa na tamaa ya pesa hapo nyuma lakini nilivyoanza kuzipata sasa akaanza kuwa na interest ya kutaka kunijua kifedha zaidi, niliiweza kumpata huyu binti kwa yeye kuvutiwa na uchangamfu wangu, ucheshi wangu, swaga zangu, navyo mhandle, n.k. lakini ghafla hivi vitu ni kama vikapewa upili na utatu huku kipaumbele kikuu kikaanza kuwa mkwanja, yani jinsi nilivyo na mafanikio ndio ikawa turn on yake mpya kwangu. Vitu kama good times tulizopitia na kumbukumbu katika penzi letu zikazikwa namafanikio.
To cut the story short mke wangu aliingia tamaa ya mafanikio, ilibidi nichekeche kichwa nikamzidi akili na divorce settlement aliambulia milioni 40, gari yake na kiwanja kile chenye fenzi aliuza. Mtoto yupo kwake nampa laki 3 kila mwezi na wala sijutii maana sitaki kimdomo kwamba situnzi mtoto.
Katika zile pesa alizopata kwenye mgao aliingiza kwenye mtaji wake afanye biashara kama nayofanya, hii ni biashara unayodeal na watu wa vijijini tena waswahili, hata ukipewa connection na mbinu kama hauna uzoefu utapata taabu na nilishamuonya, mwishowe mwenyewe akaifunga biashara kwa aibu. katika tukio moja nilitonywa kwamba alipigwa milioni 5, niliona pesa zake zinaenda kizembe nilimshauri afungue hata mgahawa lakini hashauriki, baada ya muda hapa mjini nilisikia aliweka pesa kwenye michezo yao huko hata sijui inaitwaje ila ni maarufu, nilipata taarifa kwamba ule mchezo wajanja walikuwa wanalipa watu wanaowajua tu kuvutia wageni na mwisho wa siku walikimbia na pesa za wageni, nilimshangaa sana maana alikuwa na diploma ya mambo ya business sasa ni vipi aliamini kuna pesa rahisi rahisi umpe mtu eti akurudishie na faida kubwa ndani ya muda mfupi.
biashara hii iliyonipa neema na majonzi ilianza kuwa na upinzani mwaka jana, niliyumba kidogo kwa stress za miezi miwili hivi, biashara iliyoniingizia milioni 6 kwa mwezi ikaanza kuingiza milioni 2, nilipata stress kwasababu huku kwenye ulimwengu wa biashara faida ikipungua basi kuna uwezekano wa biashara yako kuingia shimoni ukaanza kuambulia faida ya sifuri na kuanza kufilisika.
ilibidi nijiongeze nikafungua biashara zingine, ile ya zamani ya mwanzo hadi sasa ipo lakini kiukweli inasua sua kiasi kwamba hata kupiga mti (milioni) kwa mwezi "ni kwa mbinde". nilichofanya nilifungua biashara 3, moja ina uwezekano mkubwa wa kurudisha faida baada ya miaka minne kwa sasa bado ni mapema, mbili zilizobaki kuna moja niliifunga baada ya miezi mitatu baada ya kuona haina mwelekeo lakini kuna hii moja iliyobaki nashukuru imetiki ndio inanichapishia pesa, hadi sasa ndio imeshika usukani.
ex kwa sasa mawasiliano huwa ni kidogo labda sana sana ni kuhusu mtoto, huku kufatiliana labda ni yeye huwa anapenda kucheki status zangu anabaki tu kawa mpenzi mtazamaji na wala siwezi kumkataza, hata akihitaji pesa ya maji mi nampa lakini kurudiana ni NO! NO! NO!
We had it all, we had the life. Money, family, home, health, time, you name it! All we had to do was enjoy it, lakini tamaa zake zikamzidi.
Kwa sasa nipo kwenye mahusiano na binti flani kwao iringa i think ni muhehe ama mubena kitu kama hicho, nipo nae mwezi wa sita huu, kaishia form 4 lakini kwangu hicho si kigezo tena maana ananiheshimu, anayajua majukumu yake ya nyumba na kwangu mwanaume, vi mitihani kidogo kidogo vya uvimilivu anapita, lakini ndio hivyo tena moyo wa mtu kichaka huwezi jua kila kitu ila ni matumaini yangu nimepata mwanamke ataekuwa mke bora kwangu.