SoC01 Jinsi jamii inavyopata athari kwa kupuuza tatizo la Saikolojia

Stories of Change - 2021 Competition

Digitalman1tz

Member
May 17, 2015
91
216
Wanasaikologia mpo wapi? Na kama mpo mnafanya nini? Jamii inahitaji msaada kutoka kwenu. Wanasaikolojia ni watu ambao ni muhimu sana katika afya ya kila mtu na hapa nchini huwa tunapokea wahitimu wapya kila mwaka wa masuala ya saikolojia lakini mimi sijawahi waona.

Hivi kwanini tusiwatumie wataalamu wa saikolojia kama tunavyowatumia walimu kwenye taaluma yao hii taaluma. Mimi kama kijana nimesoma sehemu mbalimbali pia nimepata kufanya kazi sehemu mbalimbali lakini sijawahi kutana na hawa watu.

Mfano:

SHULENI
Kila mwaka huwa tunapata idadi kubwa ya wanafunzi wanajinyonga na kunywa sumu sababu ya kuogopa mitihani ya taifa ya kidato cha nne na sita. Hivi mnadhani hawa watoto wanapenda? Jibu ni hapana ni kwa sababu ya matatizo ya kisaikolojia. Kila shule ilitakiwa kuwa na mwana saikolojia mmoja au zaidi kama ilivyo taaluma ya ualimu maana wanafunzi wanakutana na changamoto mbalimbali ambazo wanahitaji usaidizi wa wanasaikolgia maana wanafunzi wametoka mazingira tofauti tofauti na wanapitia changaoto mbalimbali.

1626788386532.png

Chanzo: Mwanafunzi ajinyonga

Vyuoni pia kuna changamoto mbalimbali ambazo wanafunzi wanahitaji usaidizi wa kisaikologia juzi juzi nimekutana na habari ya mwanachuo mmoja mkoani Iringa kukamatwa kwa tuhuma za kumnyonga mpenzi wake.Nimeona komenti nyingi za wana jamvi waki mshutumu kijana huyo kuto fanya kitende cha kiungwana. Lakini hapo sio kusaidia kuondoa tatizo ni sawa tu na kelele cha chura hazi mzui tembo kunywa maji.Nazani hapo chuoni kungekuwa na wana saokolojia wa mahusiano huyo kijana angeenda kuongea nae na kutatua changamoto zake hayo yote yasinge tokea taarifa kutoka habarileo blogspot.com

HOSPITALINI
Nimewahi kufanya kazi katika hospitali moja ya wiliya ya moja ya majiji yaliyopo hapa nchini na katika kufanya kazi nilibahatika kufanya kazi katika wodi ya mogonjwa ya kawaida(Medical ward), katika wodi huwa kuna utaratibu wa kuanisha magonjwa kumi yanapokea wagonjwa wengi Zaidi nilikuta wodi hiyo inapokea wagonjwa wengi wanaokunywa sumu. Katika magonjwa kumi wagonjwa wanakunywa sumu wapo namba tatu na nilibahatika kupokea wagonjwa kadhaa walikunywa sumu na asilimia 98 ni vijana lakini cha ajabu mgojwa akisha patiwa matibabu anatakiwa apewe ushauri wa kisaikolojia kutoka kwa mtaalamu wa saikolojia lakini hospital haina mtaalamu wa saikolojia hivi ndivyo tatizo linazidi kuwa kubwa


KWENYE VYOMBO VYA USALAMA
Kila mwaka tunapokea taarifa ya idadi ya wafanyakazi wa vyombo vya usalama kuwapiga risasi wenza wao na wengine huchukua mamuzi ya kujiua pia sababu hawapati huduma sahihi ya ushauri wa kisaikolojia. Hivi kwanini kila ofisi ya usalama isiwe na wataalamu wa saikoligia kwa ajili ya wafanya kazi na watu wengine sio hivyo kila ofisi ata ikiwa na mtu wa saikolojia si vibaya


MAHUSIANO
Watu wengi wanapitia changamoto kwenye mahusiano mpaka kupelekea kuathirilika kisaikologia lakini huwezi kuta mtu anatafuta mwanasaikolojia kwa ajili ya changamoto ya mahusiano.mahusiano ni engo ambayo inahitaji sana msaada wa kisaikologia pale mtu anapopata matitizo ya mahusiano.mfano Juzi nimekutana na taarifa ya Neema aliye mchoma mpenzi wake nadhani alikuwa na uhitaji wa suala la kisaikolojia Zaidi yasingetokea hayo pili kuna taarifa ya yule jamaa aliye muua mwenzie sinza angepatiwa matibabu ya kisaikolojia mapema tusingepata matokeo haya ya sasa Jamii tuache kupuzia hili swali lina madhara makubwa sana katika maisha. Hivi unajua kwamba suala la upungufu wa nguvu za kiume asilimia kubwa limekuwa limejikita sana kwenye sikolojia? Watu wengi wanashindwa kufanya vizuri kwa sababu ya uoga,msongo wa mawazo na matatizo ya kiakili ambayo yanayotibika kisaikolojia

BIASHARA
Mara ngapi umeamua kuanza kufanya biashara na imefeli na kupata msongo wa mawazo? Wangapi wameingia katika hatari ya kukopa fedha kwenye mabenki mbalimbali kwa ajili ya biashara lakini wamepoteza zote na wameanguka kiuchumi na wameshindwa kuinuka tena na kuishia kupata msongo wa mawazo. Hivyo kupitia hali mbaya sana kisaikolojia lakini hamna mtu anajali kila mtu anapuuza kuna mtu akaniambia huo sio utamaduni wetu ivi aliyekuambia kwa sababu sio utamaduni ndo tuache watu wanapotea tu.



KIJAMII
Siku za hivi karibuni vijana wengi wamekuwa wakijihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya,Ulevi wa kupindukia sababu ni msongo wa wawazo kwasababu ya matatizo yanayo wakabili mfano ukosefu wa ajira,ukatili wa kijinsia,matatizo ya kiafya n.k hawa ndo taifa la kesho wanahitaji msaada wa kisaikolojia lakini bahati mbaya hawa watu wa saikolojia sijui wanajificha wapi kutoa msaada katika jamii au mnadhani jamii inahitaji msaada wa kisheria tu? ata wa kisaikologia

Unakuta watu kwenye jamii wamefanyiwa ukatili mbalimbali wanapewa msaada wa kisheria baada ya sauti kupazwa wakisaikoloJia mna muachia nan? Leo nimeona taarifa ya naibu wazira ya afya akionyesha idadi ya watoto 981 wamefanyiwa ukatili wa kijinsia kibaya Zaidi hawajapewa msaada wa kisaikologia sijui hili jambo tunalichukuliaje. Wazee wangapi huko mtaaniwamestaafu wamepewa mafao ya uzeeni na wameingia katika biashara kilimo mwisho wa siku wanafeli wanaishia kupata presha, kiharusi kutokana kupata msongo wa mawazo inampelekea kupata matatizo ya kisaikolojia wangepata msaada wa kisaikologia wasingefika huko

MWISHO
Naomba kila mtu achukue hatua na kupambana na athari zitokanazo na kupuuza suala la saikolojia pia ningeomba wizara ya elimu ijaribu kuingiza kwenye mtaala wa elimu angalau tupate elimu ya msingu kuhusu saikolojia kama ilivyo katika masomo ya afya pia naomba wizara la afya iweze kusaidia wananchi kuwa karibu na ha watu na kupata huduma saikolojia mfano kwenye vituo vya afya kutoka zahanati

1626788885102.png


1626788673378.png
 
Mkuu nilikuwa nasikiliza kipindi leo kwenye moja ya redio unaweza kunipa tofauti kati ya matatizo ya saikolojia na matatizo ya akili.
 
Ni vizuri kumpongeza mtoa mada ila nadhani jambo la muhimu sana kwa sasa ni kutoa njia za kutatua tatizo hili maana limekuwa kubwa na tunaoathirika ni sisi.

Kwa mfano mim pia ni mhanga wa hili tatizo natamani sana kukutana na mwanasaikolojia.
 
Elimu, elimu, elimu

Kwa kifupi elimu yetu tulionayo sio rafiki wa enzi hizi za science & technology. Bado tupo kwenye matumizi ya kuni kwenye dunia inayotumia hadi nyuklia kama chanzo cha nishati.
 
Hongera sana mimi ni candidate mwenzio lakini kwa uzi huu kura yangu nimeona nikupe wewe hili nitatizo kubwa sana kwenye jamii na Serikali yetu imelipa Kisogo.
 
Bonge moja ya topiki. Kwenye vyuo vikuu ofisi za Dean of Students wanakuwepo hawa jamaa.

Pia Dr. Chris Mauki anatoa huduma hii
 
Ni kweli kabisa, Private schools nyingi haswa International hizi wana utaratibu wa kuajiri wanasiakolojia.

Ila kwa shule za serikali bado sana.
 
mkuu nilikuwa nasikiliza kipindi leo kwenye moja ya redio unaweza kunipa tofauti kati ya matatizo ya saikolojia na matatizo ya akili
Ulichouliza hapo ni sawa na kusema unaomba kuambiwa tofauti ya matizo ya afya na matatizo ya magonjwa.

Matatizo ya akili ni topic ndani ya saikolojia.
 
Back
Top Bottom