Jina la Lowassa litatawala sana mijadala ya ufisadi Bungeni

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,857
Wabunge wa UKAWA watakuja na hoja nyingi za kuibua na kupinga ufisadi Bungeni na kutaka hatua zichukuliwe kwa wahusika na bila shaka wabunge wa CCM na serikali yao watazidiwa kwa hoja na pengine kukosa majibu sahihi.

Kitakachofuta baada ya hali hiyo kujitokeza katika mijadala ndani hiyo Bunge,ni wabunge wa fulani kuja na hoja mbona nyinyi mlimpokea Lowassa na huku mlidai ni fisadi na leo mnajidai kupinga ufisadi n.k.Wanaweza kumtaja moja kwa moja au kwa kumanisha japo hatakuwa na nafasi ya kujitetea kwani hayuko Bungeni jambo ambalo ni kinyume kabisa na kanuni za Bunge.

Niwaambie tu,tuhuma za ufisadi wa Lowassa ni "single" iliyochuja siku nyingi sana kiasi kwamba ni sawa na ..... ya kale ambayo hayuniki tena na single hiyo wala haina mvuto kwa sasa kwani mlishindwa kuimaliza wenyewe ndani ya Bunge na kuamua kufunga mjadal wake.

Single zinazo-hit kwa sasa ni Escrow,uchaguzu wa Zanzibar,bomoaboma,ubaguzi, n.k.ambazo hata mwananchi wa kawaida anaweza hata kuacha shughuli zake na kusikiliza kinachojadiliwa lakini kamwe sio Richomond.Single ya Richmond haiuziki kabisa siku hizi na ushahidi ni kura zaidi ya milioni 6 alizopata mh.Lowassa kwenye uchaguzi mkuu uliopita licha ya yote yaliyosemwa juu yake.

Itakuwa ni kutajana majina mwanzo mwisho kwa wengu watakaopewa nafasi ya kuongea na spika asipokuwa makini,mijadala itavunjika na vijembe kutawala na wanaweza hata kushindwa kufikia maamuzi au kuweka maazimio juu ya hoja za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

Tusubiri.
 
ni ngumu sana kwa CCM kupambana na ufisadi maana hiyo ndo biashara yenye faida wanawezaje kuipiga vita
 
Wamemkaribisha fisadi halafu wapinge ufisadi? Haiwezekani .

Ni sawa sawa na uwe na rafiki mwizi na unafahamu kuwa ni mwizi halafu eti uuchukie wizi Haiwezekani kamwe.

CHADEMA sasa ni Chama rasmi cha mafisadi.
 
Na kupajichikana majina km tumbili, nguruwe nk, tutegemee taarabu zaidi ya zile za mzee yusuph
 
kila chama kina miiko yake na miiko ya chadema kupambana na ufisadi na kutetea masilahi ya Tanzania na miiko ya ccm kutetea mafisadi na kuzalisha mafisadi wakubwa na wadogo na kufuja rasilimali za taifa
 
Hivi chadema na wengine kama wewe mnafaham mlipomkaribisha lowasa mlikuwa mnakaribisha nini.hapa sio muhimu kumjadili lowasa.tujadilianne lowasa anawakilisha nini symbolicaly kwenye jamii je ni uaminifu kwa mali za umma au wizi wa mali za umma.
kwangu mimi lowasa ni shujaa anayepaswa kupewa uwenyekiti wa chadema ili baadaye 2020 awe mgombea urais wa chadema na hatimaye rais.
kwa nini apewe uwe uwenyekiti jibu ni ili azue kubadili gia angani.
 
cdm wanaweza kuja na hoja za kuibua na kupinga ufisadi lakini kamwe hazitakuwa na nguvu kama wakati wa mwanaume wa shoka dr. slaa. huwezi mkemea mwizi wakati unae mwizi kunyumba na unafaidi matunda ya wizi wake.
unapoibua uovu wa mtu, unayeibua lazima uwe safi. hapa ndipo kauli za mwl. nyerere zilipokuwa na zinaendelea kuwa na nguvu dhidi ya waovu. nguvu ya pesa haiwezi kushinda nguvu hii.
cdm waliififisha nguvu hii iliyokuwa inawapeleka magogoni 2020 kwa kosa moja tu - kubadili gia angani. leo cdm wakiwanyooshea kidole mafisadi, ndani ya mioyo kidole hicho kinawarudia.
kubadili gia angani, kosa kubwa la kisiasa 2015.
vita dhidi ya ufisadi imepoteza ladha ikipiganwa na cdm lakini bahati nzuri tumempata tingatinga jpm anayepigana vita dhidi ya ufisadi nje ndani. anatosha, wabunge shughulikieni maendeleo ya wananchi.
 
Wakati wa kampeni walishindwa kuzungumzia ufisadi na namna ya kupambana nao, bungeni wataweza kuzungumza kweli? Sina uhakika ila tungoje!
 
Katika vitu ambavyo vimeshusha hadhi (credibility) ya CHADEMA ndani na nje na hasa nje ya nchi ni hilo la kumchukua Lowasa.Tundu Lisu alisema wako tayari kuingia hata na makubaliano na shetani kama ataweza kuwasaidia kuitoa CCM madarakani.Nadhani walifanikiwa kupata Shetani lakini huyo shetani akawa hana nguvu ya kuitoa CCM kwa kuwa CCM ina Mungu.

Sasa shetani yuko ndani ya CHADEMA na kazi ya shetani ni kuharibu na kuangamiza.Kaanza na kazi ya kuharibu credibility ya CHADEMA mengine yanafuata.Yaani wakiongelea ufisadi bungeni hata wananchi wala hawatakuwa wakiwachukulia maanani kama walivyokuwa wakiwachukulia kabla hawajamchukua Lowasa.

Na mtaji wa Chama ni Credibility.CHADEMA ilikuwa imejitahidi sana kwa kipindi cha miaka 20 kujionyesha mbele ya wananchi na jumuiya ya kimataifa kwamba ni chama credible na reliable na walikipa support kubwa ya namna mbali mbali.Hiki walichokifanya cha kumpokea Lowasa sio siri kimewabomoa hasa.Sababu watu wa nje wanajua kila kitu kuhusu Lowasa.Huwadanganyi huwambii kitu.Walipata mshtuko CHADEMA walipomchukua.
 
Kwa Wale Wote, Wanaosema Lowassa ni Fisadi Walete Ushahidi wa Ufisadi Wake, Kama Mh Lowassa Angekuwa ni Fisadi Mpaka Sasa Hivi Kwa Uongozi huu wa Mh Magufuli, Lowassa Angekuwa Mtu Wakwanza Kuonja Joto la Jiwe.

Ni Vyema Basi Watanzania Tukaacha Tabia ya Umbea, Nuafiki, Majungu, na Uzabi Zabina. Kuropoka Bila Kuwa na Ushahidi.
 
Kama Richmond hai-hit kwa sababu ya kura alizopata Lowassa basi Escrow nayo ishachuja kutokana na waliowajibishwa kurudi bungeni kwa kishindo.
 
KAMA CHADEMA WALIVYOAMUA KUACHANA NAYO KABISA HOJA YA UFISADI
 
Wamemkaribisha fisadi halafu wapinge ufisadi? Haiwezekani .

Ni sawa sawa na uwe na rafiki mwizi na unafahamu kuwa ni mwizi halafu eti uuchukie wizi Haiwezekani kamwe.

CHADEMA sasa ni Chama rasmi cha mafisadi.
Ndo vizur yeye alishaacha wizi Kwa hiyo anakusaidia kupambana na wezi anaowajua vizuri.
 
Ni vigumu kujadili ufisadi Tanzania bila kumtaja Lowassa huo ndiyo ukweli ipo hivyo hamna namna itabidi mvumilie tu wakati mnamkaribisha Chadema mlikuwa mnategemea nini.
 
Kama Magufuli tunayemwamini kuwa hamuangalii usoni MTU kwenye kuchukua hatua hajamgusa Lowasa popote hamuoni kuwa yuko clean? Magu mpaka sasa kesha mjeruhi JK tena kwa uwazi kabisa na huyo in Mwenyekiti wa chama chake kwa nini sio Edo?
Hii inadhibitisha tuu kuwa tuhuma dhidi ya Edo ni tamthilia ya Isidingo isiyo na mwisho lakini haina uhalisia au nyimbo za taarabu ili kujiburudisha tuu.
Kama kuna Mbunge anadhani kutumia jina la Edo kumkashifu itamjenga atakuwa anakosea sana. Yeye alikubali Yale maneno na matusi wakati wa kampeni sio sasa, hivyo wakae chonjo
 
Wewe una ushahidi wa Chenge ni fisadi?
 

kura milion 6 zilitoka wapi?Mbona viongozi wako wanakiri lowassa aliwahenyesha sana?Najua unaongea kujifurahisha ila sio jambo unaloliamini,CDM is getting stronger everyday na kuthibitisha hili angalia graph ya kukua kwa CDM,always going higher.
 
Wamemkaribisha fisadi halafu wapinge ufisadi? Haiwezekani .

Ni sawa sawa na uwe na rafiki mwizi na unafahamu kuwa ni mwizi halafu eti uuchukie wizi Haiwezekani kamwe.

CHADEMA sasa ni Chama rasmi cha mafisadi.

Watu wa Lumumba hebu tumieni kichwa japo kidogo. Kama CDM waliripoti na kulalamikia kwa kipindi chote UFISADI wa bw. Lowassa na serikali yenye DOLA haikuthubutu japo kumchukulia hatua!!!!!! ??????? Leo CDM wamempokea kwa sababu boss wa ikulu (JK) alimsafisha kwa kuita tukio hilo kama ajali ya kisiasa tu, leo serikali hiyo hiyo na wafuassi wake (CCM )wanalalamika nini kwa Lowassa kupata jukwaa la kuendelea na siasa zake???????????!!

AJABU AKINYA KUKU SAWA LAKINI KWA BATA UHARO waachwe wabunge wa UKAWA wafanye kazi yao ya kuikosoa serikali ili iwatumikie wananchi. NI KAZI YAO
 
Ni kweli maana Lowasa ndiyo muasisi wa ufisadi Tanzania lazima yeye atajwe mara nyingi zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…