Jimbo la Kiteto Lapewa na TAMISEMI Shilingi 180,000,000 Ujenzi wa Madarasa Shule Kongwe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,591
1,191

MBUNGE MHE. EDWARD KISAU - TUMEPOKEA FEDHA ZA MIRADI YA UJENZI WA MADARASA KATIKA SHULE ZA MSINGI KONGWE

JIMBO LA KITETO - TAARIFA KWA WANANCHI WA KITETO

Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mhe. *Edward Ole Lekaita Kisau anapenda kuwafahamisha wananchi wa Jimbo la Kiteto kuwa jimbo limepokea fedha Shilingi 180,000,000 kwaajili ya Ujenzi wa Madarasa katika shule Kongwe katika Jimbo la Kiteto.

Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Angellah Kairuki amemfahamisha leo kuwa fedha hizo zimeshatumwa na Mbuge amempigia simu Mkurugenzi wa Halmshauri na amenithibisha kupokelewa kwa fedha hizo.

1. Shule ya Msingi Kijungu iliyoanzishwa (1948) itajengewa Madarasa 2 Tsh. 40,000,000

2. Shule ya Msingi Kibaya iiliyoanzishwa (1950) itajengewa Madarasa 2 Tsh. 40,000,000

3. Shule ya Msingi Sunya iliyoanzishwa (1954) itajengewa Madarasa 3 Tsh. 60,000,000

4. Shule ya Msingi Dosidosi iliyoanzishwa (1957) itajengewa Madarasa 2 Tsh. 40,000,000

Kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo la Kiteto, Mbunge amemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote Serikalini kwa kuendelea kuboresha maisha ya WanaKiteto kwa kuendelea kuleta miradi mikubwa ya maendeleo na kushughulikia changamoto za wananchi katika Wilaya Ahadi za CCM zinaendelea kutekelezwa.

Mhe. Kisau ametoa wito kwa watumishi wote kuhakikisha kuwa miradi hii inasimamiwa vizuri na kwa ufanisi mkubwa ili wananchi wapate huduma hizi kwa wakati.

Kiteto yetu inaendelea Kung'ara !

Mungu Ibariki Kiteto!
Mungu Ibariki Tanzania!
Mungu ambariki Mhe. Rais wetu Mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge
Mhe. Edward Ole Lekaita Kisau (Mbunge wa Jimbo la Kiteto)

Kazi Iendelee

WhatsApp Image 2023-05-01 at 15.21.40.jpeg
WhatsApp Image 2023-05-01 at 15.35.35.jpeg
 
..wakati huohuo Makamu wa Raisi ametumia bilion 1.7 kukarabati ofisi na makazi yake.
 
Back
Top Bottom