Jimbo la Buhigwe linaliwa kama mchwa

mwanzo wetu

JF-Expert Member
May 4, 2014
1,581
461
Habari wakuu,. Poleni na majukumu ,

Nianze Kwa kusema kuwa Jimbo la Buhigwe ni Moja ya Jimbo ambalo linapokea Miradi mingi ya maendelo Kuliko wilaya nyingi za hapa Tanzania, na Hii ni kutokana na Jimbo Hilo kuwa eneo analozaliwa makamu wa Rais hivyo Hii imechangia sana kupata maendeleo haraka,

Kwa mda mfupi Wana benki ya NMB, chuo Cha Tehama Kiko mbioni kujengwa , stend kubwa ya mabasi ikiwemo barabara za mji wa Buhigwe kutandikwa lami.

Jimbo la Buhigwe Liko chini ya CCM na linaongozwa na Kavejuru licha kuwa anaupinzani mkubwa kutokana na Jimbo Hilo kuwa na viashiria vya kuwepo kwa watu wanaoonekana kulitaka Jimbo Hilo kwa nguvu Zote.

Zaidi nacho taka kusema juu ya Jimbo la Buhigwe ni tatizo la viongozi wengi kutokuwa waadilifu kwa kutumia pesa vibaya zinazofika ktk wilaya ya Buhigwe

Matumizi mabaya ya fedha Kwa wilaya hiyo kumepelekea baadhi ya mambo kukwama ,
viongoz wengi wa jimbo Hilo siyo wazalendo Bali wanawaza kuwaibia wananchi tu na pesa za Miradi kutumika vibaya .

Jimbo la Buhigwe linakila sababu za kupata mabadilko makubwa ya uongozi hapa na imaana wapate viongozi waadirifu na wenye utu Ili kulinda Rasilimali za wanabuhigwe na pesa Za maendeleo zinazofika ktk Maeneo ya Jimbo.

NB. Mpango awe makini Jimbo linaharibiwa kumchafua Ili ionekane hajali maendeleo ya nyumbani jambo ambalo siyo sahihi.

Wananchi wa Buhigwe wabutuke watetee maendeleo Kwa kuwa na viongozi wazuri wenye uchungu na maendeleo.
 
Kuna madudu Buyenzi secondary madudu ya mkuu mpya aliyeletwa achunguzwe maana yeye anajikita kwenye kula Hela ya shuletu, ndani ya miez michache ashatoa Hela nyingi Sana kwenye akaunt ya shule kutekeleza upigaji, mfano ishatolewa karbia ml1.6 kutekeleza ukarabati wa viti na meza lakn hakuna hata kimoja kimetengenezwa,

Hela ya fungus la maabara inapogwa, watoto wanahimizwa kujihusisha na utovu wa nidham ikiwemo ngono kwa watoto wa kike, mkuu wa shule anakimbia kituo kila muda anazurura kilasiku badala ya kutulia kituoni ijumaa asubuhi huyoo kashasepa, kama alikotoka kafelisha shule imekuwa ya mwisho alaf kaletwa kwenye shule ya kwanza kiwilaya nectar 2023 maana yake mwaka huu2024 tutegemee shule kuwa ya mwisho, kiufupi mkuu wa shule kaletwa kimkakati kutekeleza wizi
 
Back
Top Bottom